TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Saturday, March 19, 2016
UCHAGUZI KATIKA JIMBO LA KIJITOUPELE UTAFANYIKA KESHO KAMA ULIVYOPANGWA
Na Clarence Nanyaro - NEC
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema Uchaguzi katika jimbo la Kijitoupele utafanyika kesho kama ulivyopangwa,licha ya Chama cha Wananchi (CUF) kujitoa katika uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva,amesema licha ya CUF kuandika barua ya kujitoa katika uchaguzi huo,bado kuna taratibu nyingine kadhaa hazikufuatili wa ikiwa ni pamoja na kula kiapo kwa Mwanasheria cha kutoshiriki katika uchaguzi huo.
Hali kadhalika Jaji Lubuva amesema kuwa,Wananchi watawapigia kura Wagombea wa Chama hicho na baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika,kura zitahesabiwa na matokea kutangazwa kwa wananchi.
Jaji Mstaafu Lubuva ametoa rai kwa Wananchi wote waliojiandikisha,kujitokeza kwa wingi hapo kesho katika vituo vya kupigia kura ili kutimiza haki yao ya kikatiba kwa kuwachagua viongozi wanaowapenda kwa ajili ya kushirikiana nao katika kujiletea maendeleo.
Aidha,Jaji Luvuba amebainisha kuwa Daftari la Wapiga Kura litakalotumika katika Uchaguzi wa Jimbo la Kijitoupele ni lile liliotumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na taratibu nyingine zote zinazosimamia upigaji kura zitatumika pia.
Naye Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bwana Kailima Ramadhani amesema kuwa vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa moja kamili asubuhi na kufungwa saa kumi kamili jioni ba baada ya hapo hakuna mtu atayeruhusiwa kupiga kura.
Vilevile,ameongeza kuwa,kila Mpiga kura lazima abebe kadi yake ya kupigia kura, hakuna atayeruhusiwa kama jina lake halipo katika orodha ya Wapiga kura ambao majina yao yamebandikwa vituoni.
Bwana Kailima amesisitiza kuwa,Wazee,akina mama wajawazito,Wenye ulemavu wa ina mbalimbali watapewa kipaumbele katika vituo vya kupigia kura kwa kupewa nafasi ya kupiga kura mapema.
Uchaguzi katika jimbo la Kijitoupele unafanyika hapo kesho kufuatia wa ule Oktoba 25,2015 kuahirishwa kutokana na hitilafu katika karatasi za kupigia kura.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment