NAAMINI uamuzi hutolewa na upande wa tatu, kwamba mlalamikaji na
mlalamikiwa (upande wa kwanza na wa pili) wanasikilizwa kisha jaji,
hakimu au mwenyekiti wa baraza (upande wa tatu) ndiye anasuluhisha au
kutoa uamuzi.
Natambua kuwa mtu anapolalamikiwa anatakiwa kujivua uhakimu. Lakini sasa, kumbe unaweza kumdai hakimu, ukampeleka mahakamani halafu huyohuyo hakimu akapangiwa hiyo kesi dhidi yake kisha akaitolea hukumu.
Nafahamu mantiki ya upande wa tatu kutoka wenye kutuhumiana ni ili haki itendeke. Siyo hadithi ya kesi ya tumbili kumpelekea ngedere, upande wa tatu lazima uwe hauna maslahi (hauna upande) katika pande mbili zinazosigana.
Nimeiona ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni wanamlalamikia Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kuwa anapokalia kiti chake hatendi haki, anawaburuza.
Uamuzi wao umekuwa ni kuingia bungeni lakini naibu spika huyo akiwepo kwenye kiti, wanaondoka. Na walianza kufanya hivyo mara tu walipotoa tangazo lao. Hawakusema wanasusa vikao vya bunge, bali wanamsusa naibu spika.
Msingi wa kwanza ni kuwa katika mfumo wa utoaji haki ni lazima malalamiko ya mlalamikaji yapewe nafasi ya kusikilizwa kisha yakionekana hayana maana yanatupiliwa mbali. Wabunge wa Kambi ya Upinzani walistahili kusikilizwa.
Kwamba ni kipi kinawafanya wamuone Dk Tulia hatendi haki? Je, Dk Tulia alifanya nini na nini ambacho kimewaonesha kuwa vikao vya bunge vimekosa usawa kati ya Chama Tawala na Upinzani? Je, malalamiko yao yana msingi au ngonjera? Waikilizwe tu, halafu ipo hoja ya kwamba Dk Tulia anaibeba serikali katika misimamo yake na uongozi wake, ukweli ni upi?
Kwa kipindi hiki ambacho Spika wa Bunge, Job Ndugai hayupo, bila shaka naibu wake, yaani Dk Tulia ndiye mkuu wa Bunge. Ingekuwa kuna makosa ya naibu yanafanyika, basi malalamiko yangeelekezwa kwa spika. Tatizo hayupo!
Hata hivyo, bunge lina kamati zake. Na zipo kikanuni kwa ajili ya kuhakikisha majukumu ya kibunge yanatekelezwa kwa usawa. Ndiyo maana kwenye kamati zote, wapo wabunge wa CCM na wapinzani pia. Weka pembeni hoja ya idadi, mchanganyiko uliopo unakuwa na maelezo yenye kuridhisha kwamba angalau haki inakuwa inaonekana ikitendeka.
Dk Tulia ni mwanasheria na suala la pande tatu lipo katika tamaduni za kisheria. Hivyo basi, kwa vile analalamikiwa yeye, alipaswa kuonesha weledi wake katika nyanja ya sheria, kuliacha suala la wabunge wa upinzani liamuliwe na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.
Mathalan, uamuzi wa kuzuia posho za vikao kwa wabunge wa upinzani, ungetolewa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, usingekuwa na ukakasi, maana ni uamuzi wa upande wa tatu.
Uamuzi wa Dk Tulia kuwaadhibu wabunge wa upinzani kwa kuwakata posho, unaweza kutafsiriwa tu kwamba ukishindana na aliyeshika mpini, wewe ukiwa kwenye makali, lazima utaona matokeo ya makali uliyoshika.
Kitendo cha Dk Tulia kinaweza kutafsiriwa kuwa ametumia mamlaka yake kuwakandamiza mahasimu wake. Uamuzi huo unazidi kuwapa wabunge wa upinzani hoja za kuzungumza na unashamirisha chuki.
Dk Tulia ameshindwa kutumia utaalamu wake wa sheria vizuri, vilevile ameonesha hajawa na ufundi wa kucheza mizungu ya siasa za bunge. Angetumia mipango ya taaluma yake na siasa za bunge kuwakabili wapinzani na adhabu hiyo ingetoka bila ubishi.
Wabunge wa CCM ndiyo wengi, na kwa wingi wao, tayari walishaonesha kutofurahishwa na kitendo cha wapinzani kutoka nje ya bunge kila Dk Tulia alipokalia kiti.
Hata Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, wajumbe wake wengi ni wa CCM. Dk Tulia alitakiwa kufanya siasa, angelipeleka suala la wabunge wa upinzani kutoka nje kwenye kama hiyo kisha ingekuja na majibu. Isingeonekana kuwa mlalamikiwa ndiye hakimu.
Wala haikuwa kuzunguka au kumwonesha kuwa hana uamuzi, la hasha! Ilikuwa ni kujivua uhakimu wakati yeye mwenyewe ndiye analalamikiwa. Kwamba Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, ingekwenda bungeni na mapendekezo ya kuondolewa posho kwa wabunge wa upinzani kisha wabunge wote wa CCM wangeunga mkono, uamuzi ungekuwa wa bunge zima, siyo wa Dk Tulia.
Dk Tulia ni mwanasheria, anayajua haya. Tatizo ni kuwa kinachoendelea bungeni sasa hivi siyo ujenzi wa taifa linaloitwa Tanzania, ni kuoneshana umwamba. Siyo jambo jema hata kidogo. Wala halijengi afya ya demokrasia. Mashindano ya siasa yawe nje ya bunge, ndani ya bunge ni hoja kisha kanuni zifanye kazi, zaidi hekima na busara vitamalaki.
Ipo shida kubwa kwamba malalamiko ya wabunge wa upinzani ni Dk Tulia anaibeba serikali. Kasoro ya kwanza, Dk Tulia ni mbunge wa kuteuliwa na Rais John Pombe Magufuli. Yaani ni mteule wa mkuu wa serikali.
Kazi ya bunge ni kuisimamia serikali. Na ili bunge litende kazi yake vizuri ni lazima liwe huru. Lisiwe na sura ya kuingiliwa na serikali. Bunge linatakiwa kuwa na uongozi huru ambao hautatetereka kwa chochote pale ambapo kutatokea hali ya kusigana kati ya serikali na bunge.
Dk Magufuli alikuwa sahihi kumteua Dk Tulia kuwa mbunge. Ni haki yake kikatiba. Ukakasi ambao umeonekana ni kuwa mteule huyo amekwenda kuwa kiongozi wa bunge. Mhimili ambao unatakiwa kuisimamia serikali, kiongozi wake ni mteuliwa wa kiongozi mkuu wa serikali.
Haivutii kuwa na spika wa bunge, naibu spika au mwenyekiti yeyote wa vikao vya bunge ambaye ni mteuliwa wa rais katika nyanja ya ubunge. Lazima itie shaka utendaji kazi wake dhidi ya serikali.
Kiuhalisia ni kuwa bunge halipaswi kuichekea wala kuibeba serikali. Bunge linatakiwa lioneshe ukali wake dhidi ya serikali pale inaposhindwa kutekeleza majukumu yake sawasawa. Hivyo, hawahitajiki viongozi wa bunge ambao ni mbeleko ya Ikulu.
Nyakati hizi ambazo Dk Tulia analalamikiwa kuwa anaibeba serikali, inakumbusha pia aliwezaje kupata nafasi ya unaibu spika. Aliteuliwa na Rais Magufuli ambaye ndiye mkuu wa serikali. Unaweza kuona kosa la kiufundi ambalo lilifanyika.
Sasa umwamba unaendelea, niliona juzi Naibu Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango, David Silinde anagoma kumwita Dk Tulia mheshimiwa. Wakati huohuo Dk Tulia anamlazimisha Silinde amtamke kama mheshimiwa. Mashindano ndani ya bunge, jeuri na kiburi!
Wabunge wa upinzani wanaweza kuwa wanakosea, lakini waadhibiwe katika sura ambayo inaonesha kuwa haki inatendeka. Siyo kutumia nguvu ya wingi na mamlaka.
Ni mshangao kuwa tangu Kambi ya Upinzani Bungeni ilipotangaza kuwa hawatashiriki vikao vya bunge kama Dk Tulia atakuwa amekalia kiti cha Spika wa Bunge, basi imekuwa kukomoana, kila siku ni Tulia tu ndiye yupo kitini. Hana udhuru wala afya haitetereki, tofauti na zamani.
Ni kama kufikisha ujumbe “mtanijua mimi ndiye Tulia, kwangu mtatulia tu”, wala haiumizi kichwa kujua kuwa kutokosekana kwa Dk Tulia kwenye kiti cha Spika wa Bunge tangu litoke tamko la wabunge wa upinzani ni mpango mahsusi ambao ama upo kwa Tulia mwenyewe au chama chake (CCM).
Ni jukumu la kila upande kuhakikisha upinzani unaimarika ili kuifanya serikali iwe imara. Upinzani dhaifu huifanya serikali kujiona malaika na matokeo yake ni kuibuka kwa udikteta au watawala kufanya makosa mengi yasiyo na mkosoaji wala mwenye kuyasemea.
Mfumo wa vyama vingi uliruhusiwa kisheria, kwa hiyo unapaswa kulindwa kwa mujibu wa sheria. Watanzania hawanufaiki chochote kwa malumbano na maonesho ya umwamba ndani ya bunge. Watanufaika kwa bunge kutimiza wajibu wake. Dk Tulia ajiondoe kwenye vitendo vyenye ukakasi, wapinzani nao waheshimu kiti, kisha tusonge mbele kama taifa.
Ndimi Luqman Maloto.

Juma Hassan Jaka Asante mkuu. Nimekuelewa sana kamanda. Na hapo ndipo ninapomuona mwalimu Luqman Maloto, mtu ambae mimi hupenda kila siku kujifunza kwake. Big up bro hukupepesa macho ktk hili.
Daniel Geophrey Weka wazi sheria za bunge ambazo zimetungwa na bunge ambazo zinatakiwa kufuatwa na wabunge wote wakiwepo hawoo chadomo
Baraka Kashushu Wanye akili timam wanaelewa yote yanayo endelea ndani na nje ya Bunge.
Ukifuatilia nchi inavyo endeshwa utaweza kutambua kama serikali ina dhamira ya kweli ya kuondoa maovu yanayo itafuna nchi au ni ghiliba za maneno mazuri kutuhadaa kwa kisingizio cha kuwatetea wanyonge.

Pazi Salehe Hoja
yako ina mantiki na inafikirisha, binafsi zivutiwi na zile nafasi 10
anazopewa Rais kuteuwa Wabunge na wala sivutiwi na viti maalumu,
ukiangalia kwa makini binadamu huwa tunakumbuka fadhira ni ngumu kweli
kweli kwenda kinyume na aliyekufadhili ingawa mwenye msimamo anaweza
kupingana na aliyemfadhili....
Nuran Zubail Daniel
hatuwezi kuishi kila siku kwa kufuata sheria kuna upande mwingne Wa
kusikilizana na kufikia makubaliano mfno ni Kenya upinzani unaandamana
kuilazimisha serikali ibadilishe wajumbe Wa tume ya uchaguzi ukiangalia
katika sheria hakuna sheria inayo...See More
Latifa Juma Hivi
mnakumbuka kwenye kampeni Dr Magufuli alivyokua akitolea mfano chama
cha kijamaa cha nchini China? Kwamba nichama kimoja but nchi Inaenda
vzr? Nahisi anataka wabaki wao tu, ili tuwe kama China. Thank you
brother umefunguka vizuri.
Suddy Ally Unazidi kunifanya nizidi kujifarihisha kwawatu kuwa nimekuomba urafiki fb kiukweli sijawahi kujutia madayako yoyote BG UP
Mukolelanda Nyamwero Huyu
Daniel inafikia sehemu apimwe akili na pia nafikiri anataka kuleta
mabishano yasiyokuwa na sababu atueleze sheria za bunge zinasemaje? Au
naenda mbali zaidi uenda ni sehemu ya familia ya DK tulia yupo kubishana
asilolijua
Stewart Mbesela Awamu
zifuatazo ni lazmia tuwe tunawapima watu wanaotaka kugombea uraisi wana
milengo gani?? Na tuwachunguze ipasavyo toka alipozaliwa ili tujue
anaipeleka Tanzania tunakotaka au anakotaka yeye maana huwa hatuchagui
mungu au mtawala bali kiongozi wa kuisimamia dira ya majority katika
ukweli na uwazi sambamba na demokrasia iliyotukuka
Mpalule Shaaban Naunga
Mkono Hoja kwa hilo, na Pia Katika Bunge kuna Viongozi wa Bunge
wanaosimamia shuguli za kila siku za Bunge, ambao wapo chini ya Katibu
wa Bunge, Tunapozungumzia Bunge hatumaanishi wale Wabunge wanaoingia na
kutoka kila Siku ikiwa ni Pamoja na Spika
hapana, Bunge ni Muhimili ambao Kisheria unasimamiwa na Uongozi wake
uliopo hapo na ndiyo Waendeshaji wakuu wa shuguli zote Kikatiba, Spika
yeye wajibu wake pale ni kama mwajiliwa tu anayekwenda kufanya kazi yake
kisha aondoke, na anatakiwa pia kuheshimu hilo Bunge kwa kufuata kanuni
na taratibu za Bunge na siyo Wabunge, hapo kuna utofauti maana Bunge na
Wabunge ni vitu tofauti, na kwa kuwa Bunge ni Muhimili unaojitegemea
nadhani kuna Makosa mengi tu yamefanyika hapo, kwanza tunatakiwa pia
kufahamu Katibu wa Bunge ambaye ndiye Mwenye ofisina msimamizi mkuu wa
Utawala hapo Bungeni, je haoni wala kusikia jambo hili? maana kama ni
kupangwa mtu wakusimamia Vikao vinapangwa na Bunge msimamizi mkuu akiwa
ni katibu wa Bunge, wakati mwingine unaweza kukuta Dkt Tulia yeye
mwenyewe anapangiwa kuhudhulia kwenye uendeshaji wa siku awezi kukataa,
na hata maamuzi ya Suala la kutoka na kuingia Wabunge pia mwenye jukumu
la kwanza alitakiwa kuwa katibu wa Bunge, na ndiye ambaye angetakiwa
kupeleka lalamiko la kutaka kujenga hoja zote ikiwa ni katika kutaka
kupata Mantiki ya Wabunge kutoka ndani na pia kuwakata posho hilo
lilikuwa ni jambo la Katibu wa Bunge, ndani ya Bunge wabunge wao
wangejenga hoja kujadili hayo kisha sisi wananchi tungeona Bunge
limeendeshwa Kisheria, lakini kwa Mfumo huo mwisho wake unaonekana
utakuja kuwa Mbaya sana, na Pia hapo ni lazima Serikali, Bunge, na
Wabunge wanatutafuta Ubaya sisi Wenye nchi yaani Wananchi, Mheshimiwa
Rais Magufuli RAIS WETU 2015-2025,
Mheshimiwa Naibu Spika wa Bunge letuTukufu la JAmhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Katibu wa Bunge letu Tukufula Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Waheshimiwa Wabunge wetu Wateule, mliochaguliwa kwa kura
zetu sisi Wananchi mwende kutuwakilisha hapo Bungeni, Tunawaomba Wote
kwa pamoja sasa kutafakari jambo hili, je Mheshimiwa Rais unafurahishwa
na hayo yanayoendelea huko Bungeni? Mheshimiwa Rais je unadhani huu
Upinzani ukifa yaani ukiwa haupo ndiyo nchi itakuwa Salama? kwamba Rais
ama Serikali inaweza kuijenga nchi vyema pasipo wa kuwakosoa? Kwani
wewe Rais na Serikali yako autaki kukosolewa kwa yote mnayoyafanya? Je
umejiuliza chanzo cha Baba wa Taifa kuanzisha huo Upinzani wa kuikosoa
Serikali, Mheshimiwa Rais kwanza wewe ni Rais unayekubalika kwa Wananchi
wa Taifa hili, wewe unatakiwa ndiye uwe chachu ya kuwapa nguvu na Moyo
Wapinzani ili wakusaidie katika kufichua Mengi maovu yaliyojificha,
Wapinzani ndiyo Watu pekee wanaoweza kukupa taarifa ya mambo hatarishi
na yanayobomoa uchumi Wa Taifa, waliopo ndani ya Serikali yako kamwe
awawezi kuthubutu kukueleza udhaifu wao, ni kweli umejaribu kurudisha
Heshima ya Nchi lakini kumbe unataka kubomoa Bunge la Watanzania, kwani
baada ya Utawala wako Watanzania wanatakiwa Wakukumbuke kama
anavyokumbukwa hadi leo Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere,
Mheshimiwa Rais wewe Tayari umeshakuwa Rais je nini tena utataka kutoka
kwa Watanzania kama siyo kutaka tu Utukufu wa Milele? yaani ukumbukwe
Daima na Milele kwa wema na Uadilifu wako? kumbuka Mheshimiwa RAis
katika Ahadi zako uliwatangazia Wananchi kuwa utakuwa Rais wa wananchi
wote kwamba Wakuamini na hata Wapinzani wakupe kura zao Utowaangusha, je
Ulikuwa unawadanya wananchi wa Upinzani kama ukiwa unataka kushiriki
kwenye njia za Kuua Wakuu wao katika Siasa za Upinzani? je kuna haja
gani ya kuwa na Uchaguzi mkuu kama Wapinzani hawashiriki kwenye Vikao
vya Bunge kujadili Mipango ya Maendeleo ya Wananchi wako? Wewe ni Baba
wa Taifa bila kupepesa Macho Rudi tena angalia Suala hili la Bunge, kuna
Sehemu hapako Sawa rekebisha ambapo pamekaa vibaya kwa ajili ya kuzidi
kujijengea HEshima yako iliyotukuka, Binafsi naamini kwamba ni Wewe
ambaye unatakiwa kurekebisha, mimi Mwenyewe nipo Upande wako na ni
Shabiki Wako Namba moja kwa ajili ya Utendaji wako Bora, lakini naliona
hili kuwa ni Tatizo ambalo litakuja kuleta Madhara makubwa katika Tafa
Letu. Sijisikii Vizuri Moyoni Mwangu kila kukicha Chukua Maamuzi Magumu
hapo siyo jambo la kuiachia Siasa bali ni wewe unatakiwa kuhusika katika
utatuzi wake. Mungu Akubariki sana kwani naamini utafanya na kuendelea
kuwa Rais Bora wa Watanzania Wote. Asante Luqman Maloto,
kwa hoja yako Naunga Mkono Hoja na kuweka Neno langu hapo. Mungu
Ibariki Tanzania, Wabariki Viongozi Wetu na Wananzania Wote kwa Ujumla.
AMINA:
Merick Luvanda kiburi
dawa yake ni jeuri sijajua nani ataibukababe japo zama zile watu
wangekua washaitwacikulu kunywa chai alafu basi lakin sahv hamna chai
wala mkate mkigoma mkuu nae anakomaa na propaganda za maendeleo mwisho
wasiku tutaona mengi sana ila huu ushauri wa wa pinzani kufuata mawazo
ya zito hawajui anafikiria nn kile
No comments:
Post a Comment