TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 4, 2015

Establish an inclusive multi-stakeholder Education

ft1Mr. Bertin Mushi, Marketing Manager, Promasidor Tanzania Ltd and Ms. Fatma Fernandes from Abel & Fernandes Company Ltd exchanging ideas with primary school children at the Launch of Hatua Jithamini TV show.
ft2Children from different primary schools at the launch of Hatua Jithamini Show which will be aired on Star TV every Saturday at 7.30 pm to 8pm and TV1 at 11.30am.

PINDA AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA DINI

p4Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa viongozi wa dini wa mashauriano uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha  Kimataifa cha  Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es slaam Februari 3, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu)p5 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika kikao cha  mashauriano cha viongozi wa dini kilichofanyika kwenye Kituo cha  Mikutano cha Kimataifafa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 3, 2015. Kulia ni ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam ,Alhad Salum Musa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MULTICHOICE YAZINDUA KING’AMUZI KIPYA CHA DStv HD

DSC_0100

Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (Katikati) akifafanua jambo kwenye mkutano na wanahabari  (hawapo pichani), wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa king’amuziki kipya cha  DStv HD  leo jijini Dar. Kulia ni kwake ni Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo na kushoto ni Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu.

Na Andrew Chale
KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania wasambazaji wa ving’amuzi vya DStv, leo imezindua king’amuzi kipya cha DStv HD ambacho kitaanza kutumika kwa mara ya kwanza hapa Nchini.
Akizungumza  na wandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam,  Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo, akielezea umuhimu wa huduma hizo alisema king’amuzi hicho kina ubora wa hali ya juu ikiwemo kuonyesha picha zenye ubora mzuri zaidi.
Pia alieleza kuwa, DStv HD mteja atapata kuona picha zenye mvuto zaidi pamoja na kiwango cha juu cha sauti Dolby Digital 5.1.
“Wateja wa DStv watafurahia ving’amuzi hivi kwa ubora wa hali ya juu  hivyo ni wakati wa kuchangamkia  ofa kwani ndio mara ya kwanza kuingia kwa Tanzania” alisema Ronald Shelukindo.
DSC_0239
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akielezea ubora wa king’amuzi hicho cha DStv HD wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari leo jijini Dar.
Ronald Shelukindo akielezea kwa kina, alisema DStv HD, mteja anaweza kufurahia vipindi mbalimbali ikiwemo mifumo na mipangilio ya kila vipindi kwa kupendekeza atazame kipi gani, muda gani na wakati gani?.

Bunge laridhika na hali ya ulinzi na usalama wa raia

hussein
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi akijibu swali la mbunge Bungeni Dodoma.

Wamiliki wa shule za sekondari watakiwa kuzingatia viwango vya ufaulu

kilango
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Anna Kilango Malecela akijibu swali la Mh. Joseph Selasini Mbunge wa Rombo.
selasini
Mbunge la Mbunge wa Rombo Joseph Selasini, akiuliza swali.

Serikali yajenga barabara zenye urefu wa kilometa 42 mji wa Dodoma

jeni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama akijibu swali  Mbunge Bungeni.
………………………………………………………………………………..
Na Lorietha Laurence-Maelezo , Dodoma SERIKALI kupitia mradi wa uendelezaji miji (TSCP) imefanikiwa kujenga barabara zenye urefu wa kilometa 42 kwa mji wa Dodoma kwa msaada wa mfuko wa Benki ya Dunia. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama ameeleza hayo Bungeni Dodoma, kuwa ujenzi huo wa barabara umehusisha pia ujenzi wa mifumo ya maji ya mvua ,dampo la kisasa kwa kijiji cha Chidaya pamoja na mitambo y usombaji taka.

Serikali ya Tanzania yapokea takribani shillingi bilioni 15.5 kutoka Uganda

malima
Naibu Waziri wa Fedha  Adam Malima.
………………………………………………………………………………………….
Na Lorietha Laurence-Maelezo Dodoma
Serikali ya Tanzania imepokea takribani shillingi bilioni 15.5 kutoka Serikali ya Uganda ikiwa ni fidia itokanayo na athari za vita vya Kagera.
Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima ameeleza hayo Bunge mjini Dodoma kuwa fidia iliyokuwa inatakiwa kulipwa ni Dola za Marekani milioni 18.4 ingawa Uganda imelipa Dola milioni 9.7 zilizoingizwa kwenye mfuko mkuu wa Hazina.
“Kiasi hicho cha fedha kilipokelewa na kuwekwa katika Mfuko Mkuu wa Hazina kwa ajili ya matumizi ya maendelao ya wananchi ” alisema Malima.
Alibainisha kuwa taratibu za fidia zitokanazo na hasara za vita hiyo zinaongozwa na sheria na kanuni za kimataifa pamoja na utaratibu wa kutathmini kiwango cha hasara kitokanacho na vita.
Aliongeza kuwa licha ya kwamba vita hivyo viliathiri taifa zima la Tanzania ,mkoa wa Kagera umepokea fedha kutoka Mfuko Mkuu wa serikali ambayo imesaidia kusukuma maendelao ya wananchi.

Tanzania Early Childhood Development Network (TECDEN) Your partner in child Care, Parenting and Support


tecden 

This Network was established in year 2000 and officially registered in 2004. The headquarters of the Network are based in Dar es Salaam. To date 2015, the Network has a total of more than 200 members’ organizations in 14 Administrative regions of Tanzania Mainland and Zanzibar.
1. Goal:
The Network aimed at improving the livelihood of young children in Tanzania through provision of various services to enable them grow to their full potentials.
2. Objectives.
2.1 Advocating for rights of young children and other issues that affecting young children in Tanzania
2.2 Mobilizing community members to actively participate in promoting early Childhood development in Tanzania through National campaign which is investing to a young child for National Development 2.3 Coordinating information sharing among stakeholders on issues affecting young children in Tanzania 2.4 Conducting research and situational analysis for the purpose of generating evidence based facts to feed Advocacy work to issues affecting young children in Tanzania.

Ujumbe wa Taasisi ya Kijerumani ya Hanns Seidel Foundation watembelea Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma

unnamedKO1Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb) akiwakaribisha ofisini kwake Mkuu wa Taasisi ya Ujerumani iitwayo Hanns Seidel Foundation kwa Afrika na ukanda wa Sahara Bw. Claus Liepert (wa pili kushoto) pamja na mwakilishi mkazi wa taasisi hiyo hapa Tanzania Bi. Julia Gabler (wa kwanza kushoto).
unnamedKO2Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb) akiwa katika mazungumzo na wawakilishi wa Taasisi ya Hanns Seidel Foundation Bi. Julia Gabler (wa kwanza kulia) na Bw. Claus Liepert (wa pili kulia).

ZIARA YA RAIS WA UJERUMANI ZANZIBAR

RAIS KIKWETE AONGOZA SHEREHE ZA SIKU YA SHERIA NCHINI LEO JIJINI DAR ES SALAAM

unnamedjk1Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika sherehe za Siku ya Sheria nchini katika viwanja wa Mahakama barabara ya Chimala jijini Dar es salaam leo February 4, 2015 PICHA NA IKULU unnamedjk2

RAIS JAKAYA KIKWETE AMUANDALIA RAIS WA UJERUMANI DHIFA YA KITAIFA YA CHAKULA CHA USIKU, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete(wa pili kutoka kulia) na mgeni wake Rais wa Shirikisho la Ujerumani, Joachim Gauck (wa tatu kutoka kulia) wakifurahia wakati wa dhifa ya kitaifa ya chakula cha usiku aliyomwandalia  kiongozi  huyo jana usiku, Ikulu jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mke wa Rais wa Tanzania, mama Salma Kikwete na Mke wa Rais wa Ujerumani Bi. Daniella Schadt.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete(wa pili kutoka kulia) akiwa na mgeni wake Rais wa Shirikisho la Ujerumani, Joachim Gauck (wa tatu kutoka kulia) wakiwa wamesimama wakati wimbo taifa wa Tanzania na ujerumani ulipopigwa wakati wa dhifa ya kitaifa ya chakula cha usiku aliyomwandalia  kiongozi  huyo jana usiku, Ikulu jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mke wa Rais wa Tanzania, mama Salma Kikwete na Mke wa Rais wa Ujerumani Bi. Daniella Schadt.

Tuesday, February 3, 2015

WAMILIKI WA VIWANDA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADADISI WA SENSA YA VIWANDA.

 Mkuu wa chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo eneo la Changanyikeni jijini Dar es salaam Prof.Ngalinda Innocent akizungumza na wadadisi watakaokusanya takwimu za Sensa ya Viwanda mwezi huu wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku 14.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Maria Bilia akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya wadadisi 200 wa Sensa ya Viwanda itayofanyika nchi nzima  mwezi huu. Mafunzo hayo yanafanyika chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilichopo eneo la Changanyikeni jijini Dar es salaam.














MWISHO.

CLUB84 ENTERTAINMENT LTD, INAKULETEA USIKU WA WAPENDANAO-MJINI DODOMA

wote mnakaribishwa sana.

Msanii wa Muziki Juma Nature, Aomba Msaada Wa Kuwanusuru Wasanii

Nyota na msanii mkongwe wa muziki wa bongo flava nchini Tanzania, Juma Nature amesema kuwa wasanii wakongwe wa muziki huo watapotea kabisa katika ramani ya muziki kama wadau wa muziki pamoja na vyombo vya habari havitawapa nafasi ya kutosha kama wanavyopewa wasanii wengine wa sasa.
Nature amesema kuwa zamani kipindi yeye yupo Bongo Records wasanii wote walikuwa kitu kimoja na kazi zao walikuwa wanafanya kwa kushirikiana na kwa umoja kitu ambacho kilifanya wote kuwa na mafanikio sawa kwani hata maonesho yao walikuwa wanagawana fedha sawa kitu kisichowezekana kwa sasa.
Nature amesema kuwa kwa sasa wasanii kama yeye watapotea kutokana na wadau wa muziki kuwatumia wasanii wachache katika shughuri zao za kila siku huku akitolea mfano jinsi Diamond anavyopewa kipaumbele katika maonesho na kazi nyingine huku wasanii wazuri kama Rich Mavoko na Ali Kiba wakisahaulika kitu kinachosababisha kuwa na matabaka kwani wanaopewa nafasi ndio wanaofanikiwa.
Katika hatua nyingine Juma Nature amewaasa wadau wa muziki kutowasahau wakongwe wa muziki nchini kwani wao ndio walioufikisha muziki huu hapa ulipofika.

Monday, February 2, 2015

RAIS WA UJERUMANI JOACHIM GAUCK AWASILI NCHINI USIKU HUU.

 Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck  akiwa ameambatana na mkewe Bibi Schadt akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere usiku huu jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akiwa mwenye furaha mara baada ya kumpokea Rais wa Ujerumani Mh. Joachim Gauck  na Mkewe Bibi Schadt (walioshika maua), uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

WAZIRI WA UJENZI DKT. MAGUFULI AKAGUA BARABARA MKOANI MBEYA NA RUKWA.


Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia wakazi wa mji wa Tunduma mkoani Mbeya kuwa Serikali itajenga barabara ya njia nne katika mji huo ili kupunguza msongamano wa magari na kuuwezesha mji huo kuwa wa kisasa na kibiashara.

Amesema hayo katika ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya barabara inayoendelea katika mikoa ya Mbeya na Rukwa ambapo akiwa mjini Tunduma amekutana na wananchi wanaofanyabiashara katika mji huo.

“Dumisheni umoja,amani na mshikamano ili mfanye biashara zenu na kukuza uchumi nasi tutahakikisha tunajenga barabara ya njia nne ili kupunguza msongamano wa magari na kuuwezesha mji wa Tunduma kuwa wa kisasa na kibiashara na hivyo kuwa mahali pazuri pa watu kuishi”,amefafanua waziri Magufuli.

Katika ziara hiyo waziri Magufuli amekagua mizani ya Nkangamo na barabara ya Tunduma –Sumbawanga KM 225, iliyojengwa kwa kiwango cha lami na kuwataka wananchi wa mkoa wa Rukwa kutumia barabara hiyo kukuza uchumi wao na wa mkoa wao kwa kufanyakazi kwa bidii.

Akihutunbia wananchi wa Sumbawanga Waziri Dkt. Magufuli amewataka wananchi kutambua kuwa barabara za lami zinajengwa kwa gharama kubwa hivyo wazitumie kwa manufaa na wale walioko kwenye hifadhi ya barabara wabomoe nyumba zao mapema ili kuwezesha ujenzi kufanyika kwa wakati.

Waziri Magufuli amesema Serikali iko katika hatua za awali kujenga barabara ya Matai-Kasesha KM 50 kwa kiwango cha lami ili kuunganisha mkoa wa Rukwa nan chi ya Zambia na hivyo kuvutia wawekezaji wengi kuwekeza mjini Sumbawanga na hivyo kutoa fursa za ajira na uchumi kwa wananchi.

Waziri Magufuli yuko katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya barabara katika mikoa ya Mbeya,Rukwa,Katavi na Tabora ambako kuna miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara za lami inayoendelea.

Imetayarishwa na kitSengo cha habari na mawasiliano serikalini wizara ya ujenzi.

RAIS WA UJERUMANI KUWASILI LEO USIKU , MAANDALIZI YA MAPOKEZI YAKE YAKAMILIKA.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiki amewaomba wakazi wa jiji la Dar es salaam kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Rais wa Shirikisho la Ujerumani Mh.Joachim Gauck  anayetarajiwa kuwasili nchini Tanzania leo usiku kwa ziara ya kikazi ya siku tano.

Akizungumzia ujio wa rais huyo ofisini kwake  leo jijini Dar es salaam Mh. Meck Sadiki amesema kuwa rais Joachim Gauck na msafara wake atawasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere majira ya saa 2.30 usiku na kulakiwa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete.

Ameeleza kuwa mapokezi rasmi ya rais huyo yatafanyika kesho katika viwanja vya Ikulu majira ya saa 3 asubuhi ambapo rais huyo akiwa na mwenyeji wake atapata fursa ya kukagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa ajili yake na Jeshi la Wananchi wa Tanzania na kupigiwa mizinga 21.

Amesema kuwa akiwa nchini Tanzania Rais Joachim Gauck atakuwa na mazungumzo ya faragha na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es salaam na baadaye kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Vyama vya hiari, uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani pamoja na kukutana na wafanyabiashara wa Dar es salaam.

Amefafanua kuwa Februari 4, 2015, Rais huyo ataelekea Zanzibar ambapo atakutana na kuwa na mazungumzo na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na viongozi wengine wa Serikali.

Aidha kabla ya kuhitimisha ziara yake nchini Tanzania  Februari 6, 2015 rais huyo wa Shirikisho la Ujerumani atatembelea mbuga ya wanyama ya Serengeti ,Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  na Mahakama ya Kimataifa ya Haki za Binadamu jijini Arusha.

Wageni wabainika wakitengeneza Filamu bila Kibali

 Katibu Mtendaji  Bodi ya Filamu Bibi Joyce Fisoo( wakwanza  kushoto) akitoa ufafanuzi kuhusu filamu hiyo iliyokuwa ikirekodiwa na raia wa Norway katika Ofisi ya Bodi ya Filamu mwishoni mwa wiki.
 Raia hao wa Norway katika picha wakiwa katika kikao kuhusu filamu waliyokuwa wakirekodi  kwenye Ofisi  ya  Bodi ya Filamu hivi karibuni.

BODI YA MICHEZO YA BAHATI NASIBU YAKABIDHI LESENI KWA KAMPUNI YA MURHANDZIWA KUENDESHA MICHEZO HIYO

 Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya bahati nasibu , Bw Abbass Talimba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhi leseni ya kuendesha bahati nasibu ya Taifa kwa Kampuni ya Murhandziwa.
Bodi ya Michezo ya bahati nasibu ya Taifa leo imetoa leseni ya kuendesha Bahati nasibu ya Taifa kwa Kampuni ya Murhandziwa ambayo itakuwa ikiendesha bahati nasibu hiyo hapa nchini ambapo Bahati nasibu hiyo itaanza mnamo tarehe 4 Julai 2015.Bei ya tiketi zitakazouzwa itagharimu shilingi za Kitanzania shilingi 500 kwa kila tiketi.
 Baadhi ya viongozi wa Kampuni ya Murhandziwa pamoja na viongozi wa Bodi ya Michezo ya Bahati nasibu ya Taifa wakitazama video ya Mwenyekiti wa kampuni ya Kampuni ya Murhandziwa amaye hakuweza kufika kwenye hafla hiyo