TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, January 23, 2015

Waziri Saada afanya ziara ya kushtukiza Kariakoo na Mtaa wa Namanga

unnamed (39). Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (wa pili kulia) akiongoza na viongozi wa mkoa wa kodi wa Ilala kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) pamoja na maafisa wa Serikali alipofanya ziara ya kushtukiza leo jijini Dar es salaam katika soko la Kariakoo kujionea namna wafanyabiashara wanavyozingatia na kusimamia matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD ambazo wanazopaswa kuzitumia mara wanapouza bidhaa zao ili kusaidia Serikali kukusanya mapato na kuboresha utoaji wa huduma za jamii nchini. Wa kwanza kulia ni Kaimu Msaidizi wa Meneja wa mkoa wa kodi wa Ilala kutoka TRA Hamidu Athmani, wa kwanza kushoto ni Kaimu Meneja wa mkoa wa kodi wa Ilala Elias Balongo na kushoto mwa Waziri ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof. Adolf Mkenda. unnamed (40)Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof. Adolf Mkenda (wa kwanza kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (wa pili kushoto) katika ziara ya kushtukiza katika soko la Kariakoo kujionea namna wafanyabiashara wanavyozingatia na kusimamia matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD ambazo wanazopaswa kuzitumia mara wanapouza bidhaa zao ili kusaidia Serikali kukusanya mapato na kuboresha utoaji wa huduma za jamii nchini. Aliyevaa tai kulia ni wa kwanza kulia ni Kaimu Msaidizi wa Meneja wa mkoa wa kodi wa Ilala kutoka TRA Hamidu Athmani.
unnamed (41)Wananchi wakifuatilia ziara ya kushtukiza ya Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum aliyofanya leo jijini Dar es salaam katika soko la Kariakoo kujionea namna wafanyabiashara wanavyozingatia na kusimamia matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD ambazo wanazopaswa kuzitumia mara wanapouza bidhaa zao ili kusaidia Serikali kukusanya mapato na kuboresha utoaji wa huduma za jamii nchini. (Picha na Eleuteri Mangi- MAELEZO) ……………………………………………………………………….
NA Eleuteri Mangi- MAELEZO

Uelimishwaji bado unahitajika kwa wafanya biashara nchini katika na kuhakikisha wazingatia na kusimamia matumizi sahihi ya mashine za kielektroniki za EFD. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum alipofanya ziara ya kushtukiza katika soko la Kariakoo kujionea namna wafanyabiashara wanavyozingatia na kusimamia matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD ambazo wanazopaswa kuzitumia mara wanapouza bidhaa zao ili kusaidia Serikali kukusanya mapato na kuboresha utoaji wa huduma za jamii nchini. “Nasisitiza wafanyabiashara wote nchini kutumia mashine za kielektroniki za EFD katika biashara zao, niwaombe muwe na mwamko wa ulipaji kodi kwa maendeleo ya nchi yetu ” alisema Waziri Saada. Zaidi nya hayo, Waziri amesisitiza kuwa wafanyabiashara wajisajili katika mfumo wa VAT ili kuokoa mapato yanayopotea ambapo ameeleza kuwa nchi zilizoendelea wanatoa misaada kwa nchi zinazoendelea kutokana na makusanyo ya wananchi wa nchi hizo kujali na kuthamini kulipa kodi kutoka wafanyabiashara na watumishi wengine. Pia Waziri Saada aliuagiza uongozi wa TRA kuwa karibu na wafanyabiashara kwa naq kutoa namba zao za simu ili wateja waweze kuwasiliana nao mara mashine zao zinapokuwa na hitilafu na kutoa taarifa kwa haraka badala na kuwa na ufanisi wa haraka nan wenye tija kwa taifa. Naye Kaimu Meneja wa mkoa wa kodi wa Ilala kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Elias Balongo amesema kuwa wataendelea kutoa elimu kwa wananchi wote kutambua umuhimu wa kudai risiti baada ya kununua bidhaa na kwa wafanyabiashsra kutoa risiti baada ya kuuza bidhaa. Kwa upande wake mfanyabiashara wa Namanga jijini Dar es salaam Saleh Kassim Seif alisema kuwa wanaishukuru Serikali kuanzisha mfumo wa matumizi ya mashine za kielektroniki za EFD kwani unamanufaa kwao ambapo unawasaidia kujua mauzo yao ya siku, wiki, mwezi hadi mwaka ili ambapo wameweza kuboresha bishara zao kwa kuwa na kumbukumbu sahihi ya mauzo yao. Aidha, mfanyabiashara huyo alisema kuwa wanapata changamoto ya mashine hizo kuharibika wanaomba zitengenezwe ndani ya saa 24 ili waweze kutoa huduma yenye kuzingatia sheria, kanuni na taraibu za buiashara nchini. Katika ziara hiyo, Waziri wa Fedha aliandamana viongozi wa wa mkoa wa kodi wa Ilala kutoka TRA, waandishi wa habari na baadhi ya maafisa wa saerikali.

MAMA GRACIA MACHEL AKUTANA NA WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO, MHE. SOPHIA M. SIMBA

unnamed (37)Mke wa aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini Bi. Gracia Machel akiwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Sophia M. Simba (Mb) alipofika kutambulisha progamu ya ulinzi wa watoto kwa Mhe. Simba jijini Dar es salaam, tarehe 21/1/2015.
unnamed (38)Mke wa aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini Bi. Gracia Machel akiwa na mazungumzo na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Sophia M. Simba (Mb), na Katibu Mkuu Bibi Nuru M. Millao (wa pili kulia) na baadhi ya wakurugenzi wa Wizara.
………………………………………………………………………………
By: Erasto T. Ching’oro- Msemaji wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia an Watoto
  Mke wa aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini (Bi Gracia Machel) yuko katika ziara fupi nchini Tanzania kusaidia kuhimiza Serikali na wadau kutokomeza tatizo la ndoa za utotoni hapa nchini kupitia programu na miradi mbalimbali atakayoifadhili ili kuwawezesha watoto wa kike kupata haki ya elimu ambayo ni nyenzo muhimu katika kujikomboa dhidi ya umaskini. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Wizara ya Maendeleo ya Jmaii, Jinsia Na Watoto, jana tarehe 21 Machi, 2015; Mama Machel aliipongeza Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maendeleo ya jamii, Jinsia na watoto kwa jitihada zake kubwa inazozifanya kupambana na tatizo la mimba na ndoa za utotoni. Aidha, ameshauri Wizara, asasi za kiraia na wadau mbalimbali hususan viongozi wa mila/jadi na dini kushirikiana naye na kuwa mstari wa mbele katika kuleta mabadiliko chanya kupitia programu hizo anazotarajia kuzianzisha. Alifafanua kuwa mkoa wa Mara ndio utakaokuwa wa kwanza kunufaika na uanzishwaji wa programu hiyo kwani mkoa huo ni miongoni mwa mikoa iliyo na mila gandamizi dhidi ya wasichana na wanawake; na ukiwepo mfumo dume. Akitoa akimshukuru Bi. Machel kwa jitihada zake za dhati anazozifanya, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mheshimiwa Sophia Simba (Mb) amesema ni kweli tatizo hilo lipo nchini lakini Serikali kwa kushirikiana na wadau wa haki za watoto yakiwapo mashirika yasiyo ya Kiserikali, asasi za kiraia na vyombo vya habari kwa pamoja wanashirikiana kupambana kikamilifu na tatizo hili kupitia mipango shirikishi jamii ili kufikia ufumbuzi endelevu.

SMZ yasaidia nyumba za kurekebisha tabia (Sober House)

indexNA ALI ISSA/MAELEZO ZANZIBAR 

Waziri wa nchi Ofisi ya Mkamu wa pili wa Rais Fatuma Abdullhabibi Fereji amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzbar imekuwa ikizisaidia nyumba za kurekebisha tabia (Sober house) kwa kuzipatia ruzuku ya fedha kila mwaka ya kuendesha nyumba hizo ili kuona vijana wao wanabadilika kitabia.
Hayo ameyasema leo huko Baraza la Wakilishi Zanzibar wakati akijibu suali la Mjumbe wa Wawi Saleh Nassor Juma alietaka kujua kama Serikali inajua kuwepo kwa nyumba za kurekebisha tabia kwa miongozo ya dini ya kiislamu na vipi Serikali inazisaidia nyumba hizo.
Fatma Ferej alisema kuwa Serikali inajua kuwepo kwa nyumba hizo na wanazipatia ruzuku ijapo kuwa kwa kiwango kidogo kulingana na bajeti inayopatikana.
Alisema uendeshaji wa nyumba hizo hufuatia hatua kumi na mbili za kiislamu ambapo hutambulika kuwa ni “Milat Islam”na hatua hizo zimeletwa hapa Zanzibar kuazia mwaka 2009 baada ya wafanyakazi wa tatu wa na kijana mmoja aliepata nafuu baada ya kupata mafunzo huko Marekani.
Waziri huyo aliziomba Taasisi za kiislamu kuzitembelea nyumba hizo kwa kutoa michango yao na daawa itakazowapelekea vijana wanaoishi nyumba hizo kujitambua na kubadili tabia
Alisema vijana hao wanahitaji kila aina ya huduma kwani ni watoto wao ambao walijiingiza katika tabia zisizo nzuri, hivyo kuwasaidia na kuwaelimisha ni kulijengea taifa mstakabali mwema wa vijana hao..
Alisema kuna baadhi ya wazzee kuwatupa watoto hao na kuwazarau kwa vile walitumbukia katika janga baya, lakini alisema kufanya hivyo ni kosa na jambo linalohitajika ni ushiriiano wa pamoja kati ya wananchi, Serikali na Taasisi nyengine wakiwemo wakilishi na wabunge.

POSHO ZA POLISI KWA AJILI LIKIZO ZIONGEZWE

indexNa Ali Issa Maelezo Zanzibar

WAZIRI wa n Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Muhamed Abuod Mohamed amesema atamuandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mathias Chikawe kuongeza fedha za usafiri kwa askari wa Jeshi la Polisi mara baada ya kustaafu na kurejea makwao.
Hayo ameyasema leo huko Baraza la Wawakilishi Chukwani wakati akijibu suali la nyongeza la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi Saleh Nassor Juma alietaka kujua sababu za askari polisi anapostaafu kulipwa shilingi 66,000 kwa ajili ya nauli yake na kusafirisha mizigo kwa masafa ya kilomita 20 kiwango ambacho ni kidogo na hakikidhi haja.
Waziri Aboud amesema kutokana na kadhia hiyo atalazimika kuandika barua kwa Waziri Nchimbi kuliangalia suala hilo ili kulitafutia ufumbuzi na kuwaondoshea shida asikari hao wanapostaafu.
Aidha Waziri huyo alisema kuwa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar jukumu lake ni kuratibu masuala ya Muungano na kazi ya usimamizi iko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.`
Waziri Aboud akitoa ufafanuzi wa madai ya askari watatu waliostaafu kutoka Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo ilielezwa kuwa walipewa milioni 16 ili kurudi makwao kwamba taarifa hiyo sio kweli.
Alisema ana elewa kuwepo kwa askari hao na kusema askari anapostaafu hutaarishiwa usafiri wa mizigo pamoja na familia zao hadi makwao jambo ambalo hufanyika kwa kutegemea mstaafu alikuwa na cheo gani.
Baada ya ufafanuzi huo alisema kuwa Kamishna wa Polisi aliwaita askari hao ofisini kwake na kuwafahamisha utratibu ulivyo,na askari hao baadae waliridhika.

RAIS DK.SHEIN AWAALIKA CHAKULA MATAKTARI BINGWA KUTOKA UINGREZA.

 unnamed (33)  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamaed Shein (kushoto) akiwa na madakatari Bingwawa maradhi yanayohusiana na mfumo wa utoaji wa haja ndogo  kutoka Uingereza alipowaalika chakula cha mchana Ikulu Mjini Zanzibar leo madaktari hao wapo nchini baada ya kuhudhria mkutano maalum uliofanyika juzi katika Hoteli ya Breezes Hotel Bwejuu Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja,[Picha na Ikulu.] unnamed (34)Baadhi ya Madaktari Bingwa wa maradhi yanayohusiana na mfumo wa utoaji wa haja ndogo  kutoka Uingereza wakiwa katika  chakula cha mchana walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamaed Shein Ikulu Mjini Zanzibar leo, madaktari hao wapo nchini baada ya kuhudhria mkutano maalum uliofanyika juzi katika Hoteli ya Breezes Hotel Bwejuu Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja,[Picha na Ikulu.]
unnamed (36)Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamaed Shein (katikati) akiwa katika picha na ya pamoja na na madakatari Bingwa wa maradhi yanayohusiana na mfumo wa utoaji wa haja ndogo  kutoka Uingereza alipowaalika chakula cha mchana Ikulu Mjini Zanzibar leo,pia wakiwepo Viongozi wengine wa Serikali, madaktari hao wapo nchini baada ya kuhudhria mkutano maalum uliofanyika juzi katika Hoteli ya Breezes Hotel Bwejuu Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja,[Picha na Ikulu.]unnamed (35)Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamaed Shein (kushoto) akiagana na madakatari Bingwa wa maradhi yanayohusiana na mfumo wa utoaji wa haja ndogo kutoka Uingereza alipowaalika chakula cha mchana Ikulu Mjini Zanzibar leo, madaktari hao wapo nchini baada ya kuhudhria mkutano maalum uliofanyika juzi katika Hoteli ya Breezes Hotel Bwejuu Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja,[Picha na Ikulu.]

Harakati za kuhamasisha vijana zawafikia Vijana wa Mbozi.

 unnamed (29) Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Mbozi Bw. Elisey Ngowi akifungu semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivi karibuni katika Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya. Kushoto ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa na kulia ni Afisa Vijana kutoka Wizara hiyo Bi. Amina Sanga.
unnamed (30)Vijana wa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya wakisikiliza kwa makini mafunzo yaliyokua yakitolewa wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivi karibuni katika Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya.
unnamed (31)Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa kulia akifafanua jambo walipotembelea mradi wa kikundi cha vijana cha Miranaco wanaomiliki duka la madawa muhimu katika Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya. Kushoto ni Afisa Utamaduni Wilaya ya Mbozi Bw. Godfrey Msokwa, wapili kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele na wapili kulia ni Mwenyekiti wa kikundi cha Miranaco Bw. John Maige. (Picha zote na: Genofeva Matemu – Maelezo)
…………………………………………………………….
Na: Genofeva Matemu – Maelezo, Mbeya Tarehe 22/01/2015 Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi imeshauriwa kupeleka vijana wa wilaya hiyo katika Vituo vya Vijana kupata mafunzo mbalimbali ili kuweza kupata mbinu mbadala za kiujasiriamali. Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Bw. Laurean Masele wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana hivi karibuni katika Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya. Bw. Masele amesema kuwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inasimamia Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya kinachotoa mafunzo ya ujasiriamali katika fani za Kilimo na Ufugaji, Kituo cha Vijana cha Ilonga Morogoro kinachotoa mafunzo katika fani ya teknolojia ya habari na mawasiliano na Kituo cha Vijana cha Marangu Moshi kinachotoa mafunzo ya uthubutu/ujasiri kwa vijana. Aidha Bw. Masele amesema kuwa moto uliowashwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuhamasisha vijana mbinu za kiujasiriamali unalenga kuwajengea vijana ujasiri wa kuthubutu na kufikia malengo waliyojiwekea. Akizungumza wakati wa kufungua semina hiyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Bw. Elisey Ngowi amewataka vijana kuzingatia elimu inayotolewa na kuifanyia kazi kwani vijana bado wanauwezo mkubwa wa kufikiri hivyo kutumia akili nyingi na nguvu nyingi kufanya mambo mbalimbali kwa maendeleo ya Wilaya hiyo. Kwa upande wake kijana Yohana Chaula kutoka kikundi cha Bodoboda B. Mloo Wilaya ya Mbozi amesema kuwa kundi la vijana wasiokua na ajira kwa sasa linazidi kuongezeka hivyo kuiomba Wizara inayosimamia masuala ya Vijana kuongeza fungu katika Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili vijana wote nchini waweze kunufaika na Mfuko huo. Naye mwakakikundi wa kikundi cha Umoja wa Vijana Wilaya ya Mbozi Bw. Chemli Ndema ameushukuru ujumbe kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kufika Wilaya ya Mbozi na kutoa elimu ya ujuzi kwa vijana kwani elimu aliyoipata katika semina hiyo imemtoa katika giza nene na kukiri kuwa atakuwa chachu ya maendeleo na kiongozi bora katika jamii.

Kamati ya Masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya yajadili Muswada wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Dawa za Kulevya ya mwaka 2014

 unnamed (20)Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia mambo ya Bunge, Sera na Uratibu Mhe. William Lukuvi akifungua kikao cha Kamati ya Masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya kujadili Muswada wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Dawa za Kulevya ya mwaka 2014 kilichofanyika 22/01/2015 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
unnamed (21)Baadhi ya wadau toka Taasisi mbalimbali zisizo za Kiserikali wakichangia mada kupitia vifungu mbalimbali vya Muswada wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Dawa za Kulevya ya mwaka 2014 kwa lengo la kuuboresha muswada huo wakati wa kikao cha Kamati ya Masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya kilichofanyika 22/01/2015 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. unnamed (22) unnamed (23) unnamed (24) unnamed (25)Baadhi ya wajumbe toka Taasisi mbalimbali wakifuatilia kwa makini kikao cha Kamati ya masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya kilichofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kuhusu Muswada wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Dawa za Kulevya ya mwaka 2014.
unnamed (27)Baadhi ya wajumbe toka Taasisi mbalimbali wakifuatilia kwa makini kikao cha Kamati ya masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya kilichofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kuhusu Muswada wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Dawa za Kulevya ya mwaka 2014.
 (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO, DSM)
Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti_______________________
Na demasho.com
 Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma
imefanya tahimini ya elimu ya na matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi
mwaka 2014 katika ukumbi wa EMAU Peremiho.
Katika tathimini hiyo mkuu wawilaya ya Songea
Joseph Mkirikiti amewataka Madiwani ,Maafisa tarafa, Watendaji wa kata  na Watendaji wa Vijiji kuwapa elimu wazazi
juu ya umuhimu wa kuchangia chakula cha kutosheleza muhula wa masomo
ili kusaidia wanafunzi kufanya vizuri katika masomo
Kwani kufanya hivo kutasaidia wanafunzi kujifunza muda wote wawapo shuleni na kujenga ushirikiano baina yao wanapokuwa pamoja na hali hiyo iatainua kiwango cha ufaulu” alisema Mkirikiti.
Hata hivyo Mkirikiti amewataka Madiwani ,Maafisa tarafa,
Watendaji wa kata  na Watendaji kuacha
kusingizia wanasiasa kuwa wamezuia suala la kuchangia chakula
Tabia ya kuwasingizia wanasiasa kuwa wamezua kuchangia chakula mashuleni muache sio kila kitu kusingizia wanasiasa hivi ni kiongozi gani asiependa maendereo ?, maana saiz kila kitu wanasiasa wamezuia hasa kipindi hiki tunachoenda cha uchaguzi utasikia wanasiasa wamezuia ukiona mwanasiasa anazuia basi huyo ni SHIDAAA Alisema Mkirikiti.
Naye Kaimu Afisa elimu wilya Bw. Tanu Kameka ameomba baada ya Tathimini hiyo wakutane na waratibu wakata, wazazi , walimu pamoja na watendaje ili uongezwe muda wa ziada wa ufundishaji ili kuweza kuleta mwamko wa elimu katika halmashauri hiyo ya Songea vijijini na kuleta ufaulu mzuri.
 “ Miaka yote tumekuwa tukifanya hivo na ndiyo maana
tukawa tunaongoza katika matokeo , ila kwa mwaka jana hatukuweza kusimamia hili swala la muda wa ziada ndiyo maana tumeshuka ila kwa mwaka huu tunalirudisha swala la muda wa ziada hivyo tutafanya vizuri katika matokeo Alisema Bw.
Kameka.

MBEGU ZILIZOPANDWA KWENYE SHAMBA DARASA LA WAZIRI MKUU HAZIJAOTA

unnamed (17)Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Ibrahimu Msengi  akipata maelezo kutoka kwa Mshauri wa kilimo wa mkoa Mr. Nyoni  juu ya mbegu ya mahindi  aina ya Pioneer inayozalishwa na kampuni  By Treda ya mkoani Arusha  mbegu zilizopandwa kwenye  shamba la waziri mkuu na hazijaota.unnamed (18)Wakulima wakiwa shambani, shamba darasa la waziri mkuu walipokutana na mkuu wa mkoa kumweleza sakata la mbegu kushindwa kuota baada ya kupandwa hali ambayo walimweleza Mkuu wao wa Mkoa kuwa huenda wakakumbwa balaa la njaa kwani hata wakipanda muda huu mvua ziko hatarini kukatika kutokana na msimu wa mvua katika ukanda huu . (Picha zote na Kibada Kibada)

WAZIRI CHIKAWE AWAAPISHA WAJUMBE WA SEKRETARIETI YA TUME YA JESHI LA POLISI NA MAGEREZA DAR ES SALAAM LEO

unnamed (16)
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia-meza kuu) akiongoza kikao cha Tume ya Jeshi la Polisi na Magereza inayoshughulikia masuala ya kiutumishi na kiutendaji wa askari katika Majeshi hayo, katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto Meza Kuu ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
unnamed (14)Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimuapisha Afisa wa Jeshi la Magereza, Elmas Linus Mgimwa kuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Jeshi la Polisi na Magereza inayoshughulikia masuala ya Utumishi na Utendaji wa askari wa majeshi hayo, katika Ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwa Waziri Chikawe ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, na katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
unnamed (15)Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimpa hati ya kiapo Afisa Utumishi wa wizara hiyo, Ernest Maalugu kuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Jeshi la Polisi na Magereza inayoshughulikia masuala ya Utumishi na Utendaji wa askari wa majeshi hayo, katika Ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

YAH: KUVUNJIWA NYUMBA KWA GHAFLA NA MH. DIWANI WA KATA YA MIANZINI MBAGALA

unnamed (10) unnamed (11) unnamed (13)
Mimi mtajwa hapo juu ni mwandishi wa habari ninayefanya kazi katika gazeti la Sani kwa miaka minne sasa nikiwa kama Mwandishi wa habari Mwandamizi na mpiga picha.
Ninayo masikitiko makubwa kufuatia kitendo cha Mkurugenzi na mmiliki wa Gazeti la Sani ambaye pia ni Mh. Diwani Athuman Bawj Mbwana wa kata ya Mianzini, Mbagala Temeke kuchukua hatua za kuivunja nyumba niliyokuwa naishi kwa ghafla huku familia yangu ikiwa ndani hivyo kuniacha bila mahali pa kuishi na kuruhusu mali zangu kuibiwa vikiwemo vitendea kazi.
Tukio hili alifanya Januari 19 majira ya saa 9 alasili ambapo bila kuwa na kibali chochote, wala idhini ya Serikali ya Mtaa, mjumbe au usimamizi wa Polisi na pasipo kunipa Notice Mheshimiwa huyo alivamia nyumba hiyo na kuivunja huku familia yangu ikiwa ndani. Nyumba hiyo ipo eneo la Kokoto, mbele kidogo ya Mbagara Rangi Tatu karibu na Shule ya St. Marys .Alinikabidhi kwa hiyari nikiwa kama mshiriki wa kazi zake ili niweze kuishi pamoja na familia yangu. Kutoka tarehe niliyotaja hapo juu mpaka sasa mimi na familia yangu ya watu watano tumekuwa tukiishi nje hivyo kujikuta tukiishi kwa taabu sana . Uamuzi wa kuivunja nyumba hiyo ulitokana na mgogoro wa kikazi akinituhumu kwamba nimeacha kazi kwake kimyakimya jambo ambalo si kweli kwani hadi kufikia Januari 20 ,January 2015 bado nilitambulika na bodi ya Uhariri kama Mwandishi wa habari Mwandamizi. Huu ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, unyanyasaji pamoja na matumizi mabaya ya madaraka ambavyo amekuwa akitumia Mh. Diwani Mbwana. Pia ni ukatili mkubwa dhidi ya wafanyakazi pamoja na kielelezo cha jinsi waandishi wa habari hapa nchini tusivyo thaminiwa. Ninaiomba Serikali ,na wadau kunisaidia katika kipindi hiki kigumu kwani hivi sasa hali ni mbaya hasa upande wa familia yangu kwani nina watoto wadogo wakiwemo wa miaka 10,5 na 2 ambao kwa takriban siku tatu sasa naishi nao nje. nikiendelea kufuatilia taratibu za haki kuchukua mkondo wake. Aidha tunaishi kwa hofu kutokana na Diwani huyo kunipa tishio la mdomo kwamba ataniua tu. Mh. Diwani alitamka hayo tukiwa katika kikao cha usuluhishi katika ofisi za Serikali ya Mtaa Kimbangulile tar 17 jan 2015 ambapo na mimi niliripoti siku hiyo hiyo katika kituo cha Polisi Kizuiani, Temeke, na kweli alifika tar 18,jan 2015 na kujaribu kufanikisha jaribio la kuua kwa kuvunja nyumba wakati mimi na familia tukiwa ndani . Nalishukuru Jeshi la Polisi Temeke ambalo lilisimama imara kuinusuru familia yangu ambayo ilikuwa ndani wakati paa la nyumba hiyo likivunjwa huku vijana walioamrishwa na diwani huyo wakiwemo watoto wake wakipora mali zangu na kutoweka, vikiwemo vitendea kazi vyangu vya uandishi wa habari. (Jinsi ya kufika eneo la tukio ni Barabara ya Kilwa kituo Mbagala Kokoto katika kituo cha Mafuta cha Camell. ) Kwa maelezo zaidi 0654 58 67 88 CHRISTOPHER LISSA

Watanzania watakiwa kuitumia vyema fursa ya kimataifakatika maonyesho ya biashara

unnamed (1)Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akitoa nasaha zake kwa Washiriki wa Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman,kushoto kwake ni Naibu Balozi wake Bw.Juma Othman.
unnamed (3)Baadhi ya Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini humo Bw. Ali Ahmed Saleh alipokuwa akiwanasihi Washiriki hao.
unnamed (4)Baadhi ya Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini humo Bw. Ali Ahmed Saleh alipokuwa akiwanasihi Washiriki hao.
unnamed (5) Mkuu wa Msafara wa Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika mjini Mascut, nchini Oman Bi Khadija Batashy akitoa shukran zake kwa niaba ya wenzake baada ya kupewa nasaha na Balozi wa Tanzania nchini humo Bw. Ali Ahmed Saleh wa katikati, kulia kwake ni Naibu Balozi Bw.Juma Othman unnamed (7)Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akiwa katika picha ya Pamoja na Wakuu wa Msafara wa Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman kulia ni Masha Hussein na kushoto ni Khadija Batashy. Picha na Faki Mjaka.
unnamed (8)Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akiwa katika picha ya Pamoja na Watanzania wanaoshiriki Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman mara baada ya kuwapa nasaha zake. Picha zote na Faki Mjaka.
unnamed (9) Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh akisalimiana na Mwandishi wa Chanel Ten Said Makala Ofisini kwake alipowaita kwa lengo la kuwapa nasaha Washiriki wa Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman. Picha na Faki Mjaka. unnamed (82)2 Mkuu wa Utawala Ubalozi wa Tanzania nchini Oman Abdallah Kilima kushoto akimkaribisha  Balozi wa Tanzania nchini Oman Bw. Ali Ahmed Saleh kulia kutoa nasaha zake kwa Washiriki wa Maonesho ya mwezi mmoja ya Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, nchini Oman. Katikati ni Mkuu wa Msafara wa Watanzania hao Bi Khadija Batashy.
………………………………………………………………
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar, akiwa Mascut-Oman 22/01/2015
  Watanzania wanaoshiriki katika Maonesho Kimataifa ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea nchini Oman wametakiwa kuitumia vyema fursa ya kimataifa walioipata kwa kufuata vyema Miongozo waliyopewa ili ziara yao iweze kuleta Tija. Miongozo hiyo ni pamoja na Mashirikiano miongoni mwao,kujituma kwa bidii na kutumia lugha nzuri katika Maonesho hayo kwa kuzingatia kuwa Wananchi wengi wa Omani wanaelewa vyema Lugha ya Kiswahili. Wito huo umetolewa na Balozi wa Tanzania nchini Oman Mh. Ali Ahmed Saleh wakati alipokuwa akitoa nasaha zake kwa Washiriki wa Maonesho hayo Ofisini kwake Mascut nchini Oman. Amesema Tanzania ni nchi inayoongoza kuwa na Mahusino mema na Oman hivyo Washiriki hao wanapaswa wafanye kazi zao kwa bidii na kuzingatia kanuni na Maadili ya Oman. Balozi Saleh ameongeza kuwa kufuata kanuni na sheria za Oman kutawafanya Wajasiriamali hao wa Tanzania kufanyakazi zao kwa utulivu bila ya kupata usumbufu jambo ambalo litazidi kuimarisha mahusiano mema kati ya Tanzania na Oman. Amebainisha kuwa Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete aliyoifanya mwaka jana nchini humo imezidi kuyaweka pazuri mahusiano na kwamba Washiriki hao wanapaswa wayatunze na kuyalinda. “Ndugu zangu Tanzania ina nafasi ya kipekee nchi Oman,tunaheshimiwa sana kuliko nchi yoyote hasa baada ya ziara ya Rais Kikwete, naomba Mahusiano haya muyaendeleze kwa kufanya kazi zenu kwa bidii na kuchunga maneno yenu maana hawa Waoman wanakijua vyema Kiswahili Mkiwasema Wanafahamu” Alinasihi Balozi Saleh. Ameongeza kuwa Raia wa Oman wanautamaduni wa Kumsifu na Kumtukuza Mfalme wao Sultan Qabus kwa mengi mazuri aliyowafanyia hivyo Watanzania hao wanapaswa kulifahamu hilo na kulichukulia Tahadhari. Balozi Saleh amesema Mashirikiano miongoni mwao ni Jambo muhimu na kwamba wote wamekuja kwa Niaba ya Jamhuri ya Tanzania na Sio Bara au Visiwani. “Kitu kingine Mufahamu kuwa hapa Tunaiwakilisha Tanzania kwa hiyo Uzanzibari na Ubara usiwepo maana mukiupa nafasi utamusumbua,Tusimameni katika Jina moja tu la Utanzania ambalo ndio uwakilishi wetu kimataifa” Alisema Balozi. Aidha ametoa Wito kwa Wajasiriamali ambao hawakupata fursa ya kushiriki Maonesho hayo kutokata tama na kuamini kuwa ipo siku nao watapata nafasi ya kushiriki Maonesho ya kimataifa. Kwa upande wake Mkuu wa Msafara wa Watanzania Wanaoshiriki Maonesho hayo Bi Khadija Batashy alimshukuru Balozi Saleh na Wasaidizi wake kwa Mapokezi mazuri na Nasaha alizozitoa. Aidha Bi Khadija alimuahidi Balozi huyo kuzifanyia kazi nasaha hizo ikiwemo kujituma, kuzidisha mashirikiano na kutumia lugha nzuri ili kuwavutia wateja katika Maonesho hayo. Awali Mkuu wa Utawala katika Ofisi ya Ubalozi Bw. Abdallah Kilima wakati akimkaribisha Balozi aliishukuru nchi ya Mascut kwa kuzidi kuongeza njanja za kuimarisha mashirikiano ikiwa ni pamoja na Mwaliko wa Maonesho hayo. Kilima aliwataka Washiriki hao kuwa kitu kimoja na kusaidiana kwa hali na mali jambo ambalo litaipatia sifa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Maonesho hayo ya muda wa mwezi mmoja ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, huanza kila ifikapo saa 10 za jioni na kufungwa saa 04 usiku kwa majira ya nchi ya Omani ambapo Washiriki huonesha bidhaa za nchi zao na Watu kunua bidhaa hizo.

Wananchi wa maeneo ya miradi ya maji watakiwa kutozembea kujadili maendeleo ya miradi

unnamed (68)Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mwantumu Mahiza akiwakaribisha wajumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji waliotembelea mkoa huo kukagua baadhi ya miradi ya Maji iliyopo mkoani humo.
unnamed (70)Kiongozi wa ziara ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Amina Makilagi akieleza lengo la ziara ya kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji mkoani Mtwara kwa Mkuu wa mkoa huo Mwantumu Mahiza (kushoto).Kulia ni mjumbe wa kamati hiyo Asaa Hamadi.
unnamed (71)Mwenyekiti wa Halmashauri ya Lindi Mathei Makwinya, akieleza jambo wakati ziara ilipowasili kwenye kijiji cha Mnara kukagua mradi wa Rondo-Mnara.Kulia kwake ni Kiongozi wa wajumbe wa kamati ya Bunge, Amina Makilagi, Mkuu wa wilaya ya Lindi Nassor Himid na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Lindi Olliver Vavunge.
unnamed (72)Baadi ya viongozi wa kijiji na kamati ya maji ya kijiji cha Mnara na Chiponda wakimsikiliza Kiongozi wa ziara ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Amina Makilagi (hayupo pichani).
unnamed (74) Kiongozi wa ziara ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Amina Makilagi, akizungumza na viongozi wa mradi wa maji wa Rondo-Mnara na kata ya Mnara.
unnamed (75)Mhandisi wa Maji mkoa wa Lindi Valentine Ndyano (aliyevaa shati la kitenge) akifafanua jambo kwa wajumbe wa kamati ya Bunge kuhusu mtambo wa kusukuma maji.
unnamed (77)Mhandisi wa Maji mkoa wa Lindi Valentine Ndyano akifafanua jambo kwa wajumbe wa kamati ya Bunge kuhusu mtambo wa kusambaza maji kwenye vituo vya maji.
unnamed (78)Kiongozi wa wajube wa kamati akizingumza na wananchi wa kijiji cha Mnara baada ya kukagua mradi wa maji wa Rondo-Mnara. unnamed (80)Wajumbe wakikagua maendeleo ya mradi huo unaotarajiwa kukamilika Machi mwaka huu.
…………………………………………………………………….
Hussein Makame, MAELEZO, Lindi WANANCHI waliopo kwenye maeneo ya miradi ya maji mkoani Lindi na nchini kwa ujumla wametakiwa kuacha kuzembea kwenye vikao vya kujadili maendeleo ya miradi hiyo kwani kufanya hivyo kutachangia kufa kwa miradi hiyo. Hayo yamesemwa na Kiongozi wa ziara ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji mkoani Pwani, Lindi na Mtwara Amina Makilagi (Mb) wakati alipotembelea mradi wa maji wa Rondo-Mnara uliopo katika kijiji cha Mnara Kata za Mnara na Chiponda wilaya ya Lindi mkoani Lindi. Alisema miradi mingi ya maendeleo imekufa kutokana na wananchi kuzembea kwenye vikao vya kujadili uendeshaji wa miradi ya maji, hivyo kuwafanya viongozi wasio waaminifu kutumia vibaya fedha za miradi hiyo. “Mnachotakiwa msizembee kwenye vikao vya kujadili miradi ya maji kwani mkifanya hivyo miradi itakufa kutokana na viongozi kutumia vibaya fedha za miradi hiyo kujinufaisha wenyewe” alisema Makilagi. Alisema wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanasimamia utaratibu wa kuingiza fedha za miradi ya maendeleo ya maji kwenye akaunti kwani kufanya hivyo kutaepusha viongozi wabadhirifu kuihujumu miradi hiyo. Akisoma taarifa ya mradi huo mbele ya wajumbe wa kamati hiyo ya bunge, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Lindi Olliver Vavunge alisema mradi wa Rondo-Mnara ulisanifiwa kuhudumia wakazi 18,000 kwenye vijiji sita. Alisema mradi huo uliojengwa na serikali mwaka 1973 una uwezo wa kuzalisha mita za maji zenye ujazo wa 450 kwa siku lakini kutokana na changamoto ya uchakavu wa mitambo na gharama kubwa za uendheshaji, uzalishaji umepungua hadi mita za ujazo 328 kwa siku. “Vituo vitatu vya kusukua maji vilijengwa kutoka kwenye chanzo cha maji kilichopo katika kijiji cha Chikote.Ambapo kwenye kila kituo ilifungwa mitambo miwili ya kusukuma maji iliyotumia injini ya diseli.” Alisema Vavunge. Alisema mradi wa Rondo-Mnara ni miongoni mwa miradi minne ya maji safi na salama ambayo hadi sasa imekamilika na inatoa huduma kwa wananchi ikiwemo miradi ya Kiwawa, Likwaya na Namkongo. “Miradi hiyo inatoa huduma ya maji kwa wakazi 5,000 huku halmashauri ikiendelea kutekeleza miradi ya Maji ya Namangale, Hingawali, Littipu, Nyangamara na Nahukahuka” alisema. Kwa upande wa mradi wa Ng’apa unaojulikana kwa jina la 7 Towns Upgrading Program, unaofadhiliwa na serikali ya Ujerumani na Jumuiya ya Ulaya, una lengo la kuboresha huduma ya maji katika mji wa Lindi. Mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Machi mwaka huu na kufikisha huduma ya maji safi na salama kwa wakazi 194,143 wa manispaa ya Lindi na unajenga mtambo wa kusafisha majitaka yanayozalishwa katika mji wa Lindi. Awali akiwasilisha taarifa ya huduma ya maji mkoa wa Lindi kwa wajumbe wa kamati hiyo ya Bunge mkoani Lindi, Afisa Tawala wa Mkoa wa Lindi Abdallah Chikota alisema hadi Novemba mwaka 2014 wakazi wa mijini wanaopata maji safi ni asilimia 55.4 ya wakazi wote 162, 049. Alisema kwa upande wa wakazi wa vijijini wanaopata huduma ya maji safi na salama wanakadiiriwa kufikia 297,796 kati ya wakazi 702, 603 wa vijijini. Naye Mkuu wa mkoa wa Lindi Mwantumu Mahiza alisema pamoja na Serikali kutoa fedha kwa ajili ya kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa mkoa huo, lakini huduma hiyo haipatikani kama inavyotakiwa kutokana na tatizo la kukatika kwa umeme ambao kwa siku unaweza kukatika kati ya mara 22 hadi 25. Hata hivyo, alisema amewasilisha taarifa kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na wanatarajia kukutana na uongozi wa juu wa shirika hilo hivi karibuni ili kujadili changamoto hiyo ambayo inategemewa kwa kiasi kikubwa katika upatikanaji wa maji mkoani humo. Ziara ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji inaendelea kukagua miradi ya maji katika mkoa wa Mtwara ambapo inatarajia kukagua miradi ya Nanyamba-Namkuku na Tandahimba-Matogolo.

Thursday, January 22, 2015

MAREKANI NA UJERUMANI WAIPA TANZANIA VIFAA VYA KISASA KUKABILIANA NA UJANGILI MBUGA YA SELOUS

Meneja wa Mbuga ya wanyama ya Selous, Benson Kibonde akimpatia maelezo kuhusu masalia ya injini ya mvuke iliyoachwa na Wajerumani, kwa Waziri wa Maliasili na Utalii Lazao Nyalandu (kushoto), waziri huyo alipofika katika mbuga hiyo, kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kupokeavifaa vya kukabiliana na ujangili vilivyotolewa na serikali za Marekani na Ujerumani kwa ajili ya Mbuga ya Selous jana
Maelezo kuhusu masalia ya  injini hiyo ya moshi iliyoachwa na wajerumani Benson Kibonge
Waziri Nyalandu akitembela maeneo mbalimbali ya mbuga hiyo ya Selous kabla ya kukabidhiwa vifaa hivyo ya kukabiliana na ujangili katika mbuga ya wanyama ya Selous leo. anayemuongoza na Meneja wa mbuga hiyo
Waziri Nyalandu akisalimiana na Ofisa Mawasiliano na Umma wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania,  David Feloemann, alipowasili kwenye mbuga ya Selous jana
Mkurugenzi wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo, ambaye alialikwa kwenye hafla hiyo, akitazama mto Ruaha unaopita katika mbuga ya Selous

Waandishi wa habari wakiwa kwenye hafla hiyo
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza maneno ya Utangulizi kabla ya kukabidhiwa vifaa vya kukabiliana na ujangili kutoka na serikali za Marekani na Ujerumani katika hafla hiyo. Kulia ni Balozi wa Mrekani Mark Childress na waili kulia ni Balozi wa Ujerumani Egon Kochanke
Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress akizungumza kabla ya kutiliana saini na Nyalandu mkataba ya kukabidhiana vifaa hivyo. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani  Egon Kochanke
Balozi wa Marekani Mark Childress na Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Lazaro Nyalandu wakitiliana saini mkataba wa Marekani kuipa Tanzania msaada wa mafunzo yakiwemo ya kikomandoo kwa askari wa wanyamapori na vifaa vya kisasa vya kukabiliana na ujangili katika mbuga ya wanyamapori ya Selous jana.
Waziri Nyalandu akibadilishana hati na Balozi wa Marekani, Mark Childress baada ya kusaini mkataba huo. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani Egon Kochanke
Waziri Nyalandu akibalidilishana hati na Balozi wa Ujerumani Tanzania  Egon Kochanke, baada ya kutiliana saini mkataba wa ujerumani kuipa Tanzania msaada wa vifaa vya kisasa vya kukabiliana na majangili katika mbuga ya wanyama ya Selous jana
Waziri Nyalandu akimshukuru balozi huyo wa Ujerumani baada ya kubadilishana hati walizosaini. kulia ni Balozi wa Marekani Tanzania Mark Childress
Waziri Nyalandu akitoa maelezo baada ya kutiliana saini na mabalozi wa Marekani na Ujerumani
 Vifaa mbalimbali vya kisasa vilivyotolewa na serikali za Marekani na Ujerumani kwa ajili ya kukabiliana na majangili katika mbuga ya wanyamapori ya Selous
 Askari wa Wanyamapori Anita Albert akijaribu kionambali ambacho ni miongoni vya vifaa vilivyotolewa kwa Tanzania na Seriali za Marekani na Ujerumani kwa ajili ya kukabiliana na ujangili
Askari wa wanyamapori wakikagua mahema ambayo ni miongoni mwa vifaa vya kisasa vilivyotolewa na serikali za Marekani na Ujerumani kwa ajili ya kukabiliana na ujangili katika mbuga ya wanyamapori ya Selous. Picha zote na Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog