TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, August 25, 2014

Benki ya Exim yaijengea maliwato Shule ya Msingi Kilakala

 Mkuu wa matawi (Cluster Head) wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Agnes Kaganda (wapili kushoto) na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kilakala, Bw. Abdul Kuratasa kwapamoja wakifungua jiwe la msingi kuonyesha makabidhiano rasmi ya maliwato iliyojengwa na benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia ni Kaka Mkuu wa Shule Seif Ahmed (wa kwanza kushoto), Dada Mkuu wa shule Naomi Shakila (wa kwanza kulia) na mlezi wa shule hiyo Dkt. Ellen Otaru (wa pili kulia). Na mpiga piga wetu.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kilakala, Bw. Abdul Kuratasa akikata utepe kuashiria ufunguzi wa maliwato iliyokabidhiwa na Benki ya Exim Tanzania katika hafla iliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. 
========  =======  ======
 
BENKI ya Exim Tanzania imekabidhi vyoo vya kisasa kwa Shule ya Msingi Kilakala iliyopo katika wilaya Temeke jijini Dar es Salaam ikiwa ni jitihada za benki hiyo kuboresha hali ya usafi na mazingira ya kujifunzia shuleni hapo. 

Ujenzi huo wa matundu kumi ya vyoo na mfumo safi wa maji ni moja kati ya miradi ya kimaendeleo iliyotekelezwa na kugharamiwa na Benki ya Exim Tanzania katika shule hiyo ya Kilakala iliyo chini ya benki tangu mwaka 2012 ikiwa kama benki mlezi.       

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano shuleni hapo jana Mkuu wa Matawi/Cluster Head wa Benki ya Exim, Agnes Kaganda, alisema benki yake imeamua kupiga jeki mradi huo ikitambua umuhimu wa usafi kwa afya ya wanafunzi na walimu na mchango wake katika maendeleo kitaaluma kwa shule hiyo.  
                 
“Shule ilikuwa na maliwato yenye matundu nane tu ikiwa na wanafunzi 2739. Kutokana na Benki ya Exim kuongeza matundu mengine kumi, tunaamini kuwa hali hii sasa italeta ahueni kwa wote, walimu na wanafunzi hapa shuleni,” alisema.

Alisema kuwa mbali na matundu hayo kumi, wavulana nao wana sehemu maalum ya maliwato ikiwa na maji yanayotembea ili kuiweka maliwato katika hali ya usafi muda wote.

“Tunaamini kuwa, kwa kuboresha hali ya usafi ya shule kutasaidia kuzuia wanafunzi haswa wasichana kutoruka vipindi vya masomo ili kutafuta vyoo visafi au wanafunzi kutoambukizwa magonjwa ya kuambukizwa. Hii itawasaidia wao kuelekeza zaidi jitihada zao katika masomo, na hivyo kuweza kufanya vizuri zaidi darasani,” alisema Kaganda.

Alibainisha kuwa sasa ni juu ya uongozi wa shule na jamii inayoizunguka shule kuhakikisha kuwa maliwato hiyo inatumika vizuri ili iweze kutumika na wanafunzi wengine wanaoweza jiunga na shule hiyo siku za usoni.

 “Ningependa kuuasa uongozi wa shule na wanafunzi kuhakikisha kuwa maliwato hii inatunzwa na inabaki kuwa safi. Lengo hili litatimia tu endapo tutaweza kuiweka maliwato yetu katika hali ya usafi,” aliongeza. 

Alibainisha kuwa Benki ya Exim imekuwa ikiibadilisha shule taratibu tangu ilipokuwa benki mlezi, ambapo sasa shule hiyo inajivunia kuwa na maktaba ya kipekee, wanafunzi wakisoma wamekaa kwenye madawati yaliyotolewa na benki, na sasa shule ina mfumo nzuri wa maji safi, vikitajwa kwa uchache. Miradi yote ikifadhiliwa na benki kama sehemu yashughuli mbali mbali za kijamii.

Naye, mwalimu mkuu wa shule hiyo, Bw. Abdul Kuratasa alipongeza jitihada za benki katika kufuatilia maendeleo ya shule tangu ilipoichukua kama benki mlezi na kusema kuwa sasa wanafunzi wa Shule ya Msingi Kilakala wanafurahia matumizi ya vifaa vya kisasa kama shule nyingine za binafsi. 

Alisema kuwa mchango huo wa maliwato ni moja kati ya hatua ambazo zinapaswa kuigwa na makampuni mengine ili kuboresha sekta ya elimu nchini.

“Naipongeza benki kwa jitihada zake kuhakikisha kuwa tunaboresha mazingira ya kujisomea ya shuleni hapa. Dhamira ya benki katika kusimamia maendeleo ya shule imekuwa thabiti tangu ilipoichukua shule yetu kuwa benki mlezi mnamo Agosti mwaka 2012.

“Tungependa kuishukuru Benki kwa kutujengea maliwato na tunahaidi kuwa tutaitunza vyema kwa ajili ya wanafunzi wengine katika siku za usoni,” alisema Bw. Kuratasa.

No comments:

Post a Comment