Moses Mashalla,
Mahakama
 kuu nchini kitengo cha biashara kanda ya Arusha imemuamuru 
mfanyabiashara ambaye pia ni mmiliki wa hoteli ya Snowcrest ya jijini 
Arusha,Wilfred Tarimo pamoja na familia yake kumlipa jumla ya $ 1.7 sawa
 na zaidi ya sh,3 bilioni mkurugenzi wa kampuni ya Grand Alliance 
Ltd,James Ndika kama malipo ya awamu ya kwanza ya kununua hisa ndani ya 
hoteli hiyo.Mbali
 na agizo hilo mahakama hiyo pia imeagiza washtakiwa wanne kati ya 
watano katika kesi hiyo  walipe  kiasi cha riba cha asilimia 4 ya fedha 
hizo  tangu kufunguliwa kwa kesi hiyo na kiasi kingine cha asilimia 7 
tangu kufungwa kwa shauri hilo hadi siku ya malipo.
Hukumu
 ya kesi hiyo ilisomwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Jaji Robert 
Makaramba mbele ya mahakama hiyo mara baada ya kueleza kuridhika na 
ushahidi uliowailishwa na upande wa mlalamikaji kupitia kwa wakili wake 
Melkizedek Lutema.
Katika
 kesi hiyo iliyopewa usajili wa nambari 9 ya mwaka 2012 Ndika alieleza 
kutapeliwa jumla ya $ 1.7 milioni  sawa na sh,3 bilioni baada ya 
kupatiwa hati mbili za eneo la hoteli hiyo lakini baadaye ilikuja 
kubainika kwamba eneo la hoteli hiyo lina hati tatu.
Katika
 hati ya madai mlalamikaji anadai kuwa hati moja kati ya tatu ilikuwa na
 mkopo wenye riba wa kiasi cha sh,1.5 bilioni kupitia benki mojawapo 
hapa nchini na baada ya kugundulika hilo ilikwamisha biashara ya 
mauziano ya hoteli hiyo.
Kwa
 mujibu wa nakala ya hukumu iliyosainiwa na Jaji Makaramba washtakiwa 
watano katika kesi hiyo mshtakiwa wa kwanza ,Wilfred Tarimo,Derick 
Tarimo,Doreen Tarimo ambaye ni mke wa mshtakiwa wa kwanza Irene Tarimo 
pamoja na kampuni ya Snowcrest And Wildlife Safaris Ltd  wameamriwa 
kumlipa Ndika fedha hizo pamoja na kiasi cha riba hadi tarehe ya kukazia
 hukumu.
Mbali
 na agizo hilo washtakiwa wote katika kesi hiyo pia waliamriwa kulipa 
gharama za uendeshaji wa kesi hiyo  tangu ilipoanza kuunguruma huku 
wakipewa nafasi ya kukata rufaa ndani ya siku 30  tangu hukumu hiyo 
ilipotolewa.
Akihojiwa
 jijini Arusha wakili wa upande wa mlalamikaji,Lutema alisema kuwa wao 
wameridhika na hukumu hiyo na kwa sasa wanajiandaa kuwasilisha gharama 
za uendeshaji wa kesi hiyo tangu ilipoanza kuunguruma mnamo Januari 5 
mwaka 2012.

No comments:
Post a Comment