TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, August 25, 2014

MASHAUZI CLASSC KUPELEKA WIMBO WA ASIYEKUJUA AKUTHAMINI NAWINA RESORT MBAGALA KUU,



Na: Violeth John (DACICO TANZANIA).

Bendi ya muziki wa Mwambao (Taarabu) Mashauzi classic,  siku ya jumamosi ya tarehe 30/8/2014 wiki hii, itashuka kwenye Ukumbi wa Kisasa wa Nawina Resort Mbagala kuu ambako wanatarajia kwa Mara ya kwanza kuwapa raha Mashabiki kwa kibao kipya cha Asiyekujua Akuthamini.
Akizungumza mapema hii leo Meneja wa Mashauzi Classic Bw. Ismail Rashid (Suma Ragar) amesemakuwa maandalizi yote yamekamilika kwa ajili ya onyesho hilo siku ya jumamosi katika Ukumbi wa Nawina Resort uliopo mbagala kuu.
“tunatazamia kuwapa raha Mashabiki wetu wa mbagala kuu, kutokana na vibao vinavyozikoga nyoyo mashabiki wetu, katika Ukumbi wa Nawina Resort kila tunapopeleka burudani mashabiki ujitokeza kwa wingi kiasi cha kuleta msisimko wa hali ya juu, lakini hata hivyo awamu hii tumeamua kuwapa kitu kipya kibao ambacho kinasema asiyekujua hakuthamini ulioimbwa na nyota nguli wa Muziki wa Taarabu aisha Mashauzi” amesema Suma Ragar
Naye  mkurugenzi wa Nawina Resort,  Mama Mary Komba, amesema kuwa kwa Upande wa maandalizi kuhusiana na burudani hiyo, kila kitu kimekamilika hivyo Wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake wajitokeze kwa ajili ya kufika kupata burudani hiyo ambayo inapatikana kwa musimu kutokana na Aisha kuwa na Ratiba ndefu ya burudani katika mikoa mbali mbali ya Tanzania.
“kama unavyofahamu tena kwa sasa baada ya Mfalme wa Muziki wa Taarabu, Mzee Yusuph Kuachana na aina ya huu muziki, kwa sasa hakuna shaka kwamba Mashauzi ndiyo bendi pekee inayoendelea kutingisha katika Ulimwengu wa Miziki ya Mwambao yaani Taarabu, kwa hiyo ninachukua fulsa hii kuwakaribisha sana mashabiki wote wa Mashauzi Clasic siku ya jumamosi katika ukumbi wetu wa Nawina Resort, ili wafike kusikia Vibao Vipya ukiwemo huu wa asiyekujua hakuthamini, pamoja na nyimbo nyingine nyingi, lakini pia nichukue fulsa hii kuwaeleza mashabikim kuwa, Usalama wa Magari pamoja na Vifaa vyao umeandaliwa wa kutosha hivyo hakuna shaka kuhusiana na suala zima la ulinzi” amesema Mama Mery Komba.
Vibao vingine vinavyotarajia kuitikisa mbagala Kuu siku hiyo ni pamoja na kibao cha ropokeni yanayowahusu kilichoimbwa na Saida Ramadhani, Haya ni Mapenzi tu kibao kilichoimbwa na Zubeida Malicky, Bonge la Bwana kibao kilichoimbwa na Hashim Saidi.
Kiingilio katika Onyesho hilo kimepangwa cha kuridhisha kutokana na hali ya maisha ya wakazi wa eneo la Mbagala na Vitongoji vyake ambapo kiingilio kimepangwa mlangoni shilingi 7000. Burudani hiyo inatarajia kuanza mapema saa 2:00 usiku na kuendelea.
Mwisho.


No comments:

Post a Comment