Baadhi ya viongozi kutoka majiji sita ya Tanzania wakipata maelezo 
kuhusu mfumo wa ukusanyaji wa taka na uchujaji wa maji machafu katika 
jiji la LAHTI, kutoka kushoto ni mratibu wa mtandao wa majiji Tanzania, (
 Tanzania Cities Network) Philoteus Mbogoro, Meya wa jiji la Tanga Omary
 Guledi, Lissa Tervo wa taasisi ya Uongozi ya Tanzania, Johanna Palamoki
 ambae ni mtaalam wa mipangomiji katika jiji la LAHTI, Mkurugenzi wajiji
 la Lahti Kari Porra na Meya wa jiji la Mbeya Athanas Kapunga ( picha 
zote na Vedasto Msungu wa ITV)
 Mkurugenzi wa jiji la LAHTI, Kari Porra akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa 
nyumba hizo za mbao kwa mratibu wa ziara hiyo Godfrey Nyamrunda kutoka 
taasisi ya Uongozi ya Tanzania, nyuma yao ni Meya wa jiji la Dar Esa 
Salaam Dk Didas Masaburi
Badhi ya nyumba za ghorofa zilizojengwa kutumia mbao katika jiji la
 LAHTI nchini Finland ambazo zilitembelewa na madiwani wa majiji sita ya
 Tanzania waliokuwa katika ziara ya mafunzo nchini humo iliyoratibiwa na
 taasisi ya Uongozi ya Tanzania. Finland ni miongoni mwa nchi zenye maeneo makubwa ya misitu ya
 kupandwa dunaini, zaidi ya asilimia 80 ya eneo la nchi hiyo ni misitu 
na wenyewe wanasema nyumba zinazojengwa kwa kutumia mbao zina gharama 
nafuu kuliko kujenga kwa matofali au mawe.
 Viongozi kutoka majiji sita ya Tanzania wakiwa kando kando ya ziwa Maji 
ambako mkondo wa maji machafu kutoka majumbani huingia ziwani baada ya 
kuchujwa, viongozi hawa kutoka kushoto ni Stanslaus Mabula ambaye ni 
Meya wa jiji la Mwanza, Athanas Kapunga ambae ni meya wa jiji la Mbeya, 
Mussa Zungiza,mkurugenzi mtendaji wa jiji la Mbeya na Philoteus Mbogoro 
ambae ni mratibu wa mtandao wa majiji Tanzania TACIN
Badhi ya nyumba za ghorofa zilizojengwa kutumia mbao katika jiji la
 LAHTI nchini Finland ambazo zilitembelewa na madiwani wa majiji sita ya
 Tanzania waliokuwa katika ziara ya mafunzo nchini humo iliyoratibiwa na
 taasisi ya Uongozi ya Tanzania. Finland ni miongoni mwa nchi zenye maeneo makubwa ya misitu ya
 kupandwa dunaini, zaidi ya asilimia 80 ya eneo la nchi hiyo ni misitu 
na wenyewe wanasema nyumba zinazojengwa kwa kutumia mbao zina gharama 
nafuu kuliko kujenga kwa matofali au mawe.
No comments:
Post a Comment