1.  Meneja
wa Kampuni ya TANCOAL  (wanne kulia) Tan
Brereton  na  Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo Emmanuel
Constantinides (wa tatu kulia) wakimwonesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini Eliakim Maswi  na ujumbe wake
namna shughuli za himbaji Makaa ya Mawe zinavyofanyika.
 Gari la kubeba kupakia Makaa ya Mawe likiendelea
na kazi hiyo katika Mgodi wa Ngaka unaomilikiwa na kampuni TANCOAL.
 Mashine
ya kusaga makaa yam awe katika viwango mbalimbali kulingana na mahitaji ya
wateja ikiendelea na kazi ya kusaga mawe katika Mgodi wa Mkaa ya Mawe wa Ngaka
unaomilikiwa kwa ubia na Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na kampuni ya Australia. 
  Gari
la kubeba makaa ya Mawe katika mgodi wa Ngaka likimwaga makaa sehemu maalum
kutoka mgodini kabla ya kusagwa katika viwango mbalimbali kulingana na mahitaji
y wateja.
=======  ========  ======
Madini
Migodini yapo Salama- Maswi
Ø Aeleza TMAA wapo
kuhakiki   mwenendo wa uzalishaji,uuzaji
Ø Mwekezaji  asisitiza Makaa ya Ngaka yana ubora wa juu
Na
Asteria Muhozya, Mbinga
Katibu
Mkuu  wa Wizara ya Nishati na Madini,
Eliakim Maswi amewataka watanzania kuondoa dhana kuwa madini  yanayochimbwa katika migodi mbalimbali nchini
yanaibwa  na wawekezaji wakubwa na
kusisitiza kuwa, Wizara  kupitia Wakala
wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), wapo katika migodi yote nchini
kuhakikisha kwamba madini hayo hayatoroshwi .
Maswi  ameyasema hayo alipotembelea Mgodi wa kuchimba
Makaa ya Mawe  wa kampuni ya  Tancoal eneo la Ngaka wilayani Mbinga inayomilikiwa
kwa ubia kati ya Kampuni ya Australia na Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na
kuongeza kuwa, TMAA wapo katika kila mgodi 
kujua kiasi cha madini kinachochimbwa, kinachouzwa na kwa  ajili ya kuhakiki vyeti vya mauzo ya madini
hayo kuhakikisha kuwa vinakwenda sambamba na kiasi cha mrahaba kinachotolewa na
wawekezaji.
Kwa
upande wake Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Paul Masanja alisisitiza hoja
ya Katibu Mkuu Maswi na kuongeza kuwa, Wizara kupitia maafisa wa TMAA wamekuwa
wakifanya ukaguzi kuhakikisha kwamba serikali inapata mrahaba stahili kupitia
madini yanayouzwa na kutoa mfano kwa madini ya Makaa ya Mawe ya Ngaka kwamba
serikali inapata asilimia 100 ya mrahaba.
“Nawapongeza
sana TanCoal ni wasikivu, maafisa wa TMAA huwa wanafanya ukaguzi kila baada ya
miezi mitatu kujua kiasi kinachozalishwa na kinachouzwa hivyo, tunakwenda nao
vizuri,” alisisitiza Masanja.
Naye  Mkurugenzi wa Tancoal  Tan Brereton ameeleza kuwa,  mgodi wa wa Ngaka ni mradi mkubwa kwa
Tanzania na kuongeza kuwa, uwepo wa mgodi wa makaa ya mawe wa Tancoal ni
mafanikio na maendeleo makubwa kwa Tanzania kutokana na  kuwezesha ajira kwa wataalamu mbalimbali
nchini ikiwemo serikali kupata kodi na mirahaba kupitia mgodi huo jambo ambalo
litawezesha kuboresha huduma za kijamii.
Aidha,
amezitaja faida  za nyingine za mgodi huo
kuwa, uwepo wa Mgodi huo utawezesha Tanzania kuzalisha kiasi kikubwa cha
nishati ya umeme kutokana na uwepo wa kiasi kikubwa cha makaa hayo katika mgodi
wa Ngaka  na kueleza kuwa, makaa ya mawe
kutoka katika mgodi huo yana ubora wa kiwango cha juu tofauti na madini yanayochimbwa
nchini Afrika Kusini.
“Makaa
ya Ngaka yana ubora wa hali ya juu sana tofauti na makaa ya nayochimbwa Afrika
Kusini kwasasabu madini haya hayahitaji kusafishwa kabla ya matumizi tofauti na
mengine ambayo husafishwa kabla ya kutumiwa ,alisisitiza Tan.
Aidha
ameongeza kuwa,  kampuni hiyo ina uwezo
wa kuzalisha kiasi cha tani  480,000  za makaa ya mawe kwa mwaka na kuongeza kuwa,
tayari kampuni hiyo imesaidia huduma mbalimbali za kijamii katika maeneo ya
afya,shule ,maji na kuwaendeleza vijana na kutumia zaidi ya shilingi milioni
mia sita na kuongeza kuwa, kampuni hiyo imekwisha toa kiasi za bilioni 2 kama
kodi na mrahaba  kwa serikali.
Kwa
mujibu wa Tan, ameeleza kuwa, makaa yanayozalishwa na kampuni hiyo yanatumika
katika viwanda vya  saruji vya Mbeya
Tanga Lake,  kampuni ya METL na viwanda
vya karatasi viwanda vya nguo.
No comments:
Post a Comment