TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, February 12, 2015

“HATUTAFAIDIKA NA MIRADI YA MAJI TUNAYOITEKELEZA, KAMA HATUTATUNZA VYANZO VYA MAJI TULIVYONAVYO”-MAKALLA

mak2Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla mara akiwa amesimama pembeni ya mradi wa Kijiji cha Managhat, Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara,pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Omari Chambo na Mkurugenzi wa Mji wa Babati, Omari Mkombole mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye mradi huo.

mak3Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera wakikata rasmi utepe, kabla ya kuweka jiwe la msingi kwenye jengo jipya la Mamlaka ya Mji wa Babati.
mak4Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera, Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Omari Chambo (mwisho kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya BAWASA, Mashughuli Minja (anayefuatia) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Babati (BAWASA), Iddi Msuya ndani ya jengo jipya la Mamlaka ya Maji Babati.
mak5Naibu Waziri wa Maji akikagua pampu ya kusukumia maji kwenye chanzo cha maji cha Masika, Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara.
…………………………………………………………………….
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla amesema wananchi hawatafaidika na miradi ya maji inayotekelezwa na Serikali hivi sasa, kama hawatakuwa makini kuvitunza na kuvilinda vyanzo vya maji. Mhe. Makalla amezungumza hayo jana katika ziara yake wilaya ya Babati, mkoa wa Manyara wakati akikagua utekelezaji wa miradi na kuzindua miradi iliyokamilika katika mkoa huo. “Miradi hii inayotekelezwa na Serikali hivi sasa, haitakuwa na maana kama hatutaacha uharibifu wa vyanzo vya maji tulivyonavyo, ambao unatokana na shughuli za kibinadamu za kila siku ndani au kandokando ya vyanzo hivyo. Miundombinu tunayoiweka haitakuwa na maana na itabaki kuwa kama magofu kama hatutakuwa na vyanzo vya maji vya kudumu”, alisema Mhe. Makalla. “Imefika wakati wananchi waamue na kuchukua hatua thabiti ya kutunza na kulinda vyanzo vya maji, la sivyo juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali zitakuwa bure na kuingia gharama kubwa bila faida yoyote. Wananchi naomba mtupe ushirikiano katika hili, ili sisi tuweze kuhakikisha tatizo la maji katika nchi yetu linafikia kikomo”, aliongeza Mhe. Makalla. Naibu Waziri alisema kuwa miradi hii inagharimu mamilioni ya shilingi na Serikali imedhamiria kuwapa wananchi maji na si vinginevyo, lakini bila ushirikiano wao lengo letu halitafanikiwa. Hasa ukichukulia maeneo mengi ambapo miradi imetekelezwa kwa ufanisi, imechangiwa na ushirikiano mzuri unaopata Serikali kutoka kwa wananchi wake. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera alishukuru jitihada za Serikali za kutatua tatizo la maji nchini kote, na alitoa agizo kwa viongozi wa mkoa mpaka vijijini, kuhakikisha kuwa wanachukua sheria kali na kuhakikisha hatua kali zinachukuliwa dhidi ya uharibifu wa vyanzo vya maji. Huku akisisitiza sheria ya kutofanya shughuli zozote za kibinadamu umbali wa mita 60 kutoka chanzo cha maji izingatiwe na kuahidi kama Mkuu wa Mkoa atalifanyia kazi ipasavyo. Hii imetokana na maeneo mengi ya vyanzo vya maji vya miradi mingi kuonekana haitunzwi vizuri katika wilaya za Hanang na Babati, huku shughuli nyingi za kibinadamu hasa kilimo zikionekana kushamiri katika vyanzo hivyo na kuleta changamoto kubwa katika utekelezaji wa miradi ya maji mkoani Manyara.

No comments:

Post a Comment