TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, February 12, 2015

WAZIRI CHIKAWE AWAPA SOMO MAKATIBU KATA CCM NACHINGWEA, MKOANI LINDI

chik1Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) akizungumza na Makatibu Kata wa CCM, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi leo. Katika mazungumzo hayo yaliyojumuisha Makatibu Kata zaidi ya 30, Waziri Chikawe aliwataka viongozi hao kuhakikisha wanazunguka katika kata zao kuhakikisha wanawahamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwa ajili ya maandalizi ya kuipigia kura Katiba inayopendekezwa pamoja na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwaka huu nchini. Katikati Meza Kuu ni Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Mussa Liliyo akifuatiwa na Mwenyekiti wa Makatibu Kata hao, Ally Napepa.
chik3Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, mkoani Lindi, Mathias Chikawe (wanne kushoto-mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Kata wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimboni humo baada ya kuwapa somo makatibu hao la kuhakikisha wanawahamasisha wananchi kujitokeze kwa wingi kujiandikisha kwa ajili ya kuipiga kura Katiba inayopendekezwa pamoja na Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwaka huu nchini. Picha zote na Felix Mwagara.

No comments:

Post a Comment