TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 11, 2015

Moto wateketeza bweni la wanafunzi Idodi Sekondari

Wananchi na  wanafunzi  wa shule ya  sekondari  Idodi Iringa   wakishiriki  kuzima  moto katika  bweni la   wanafunzi  wa  kike  shuleni  hapo amnbalo lilikuwa  likiwaka  moto  leo  asubuhi
MOTO mkubwa  ambao  chanzo chake  kinatajwa  kuwa  ni  hitirafu  ya  umeme  umeteketeza bweni  la  wasichana  katika  shule  ya  Sekondari  Idodi wilaya  ya  Iringa  mkoani Iringa .
 
Tukio hilo  limetokea  muda  wa saa 4  asubuhi  leo wakati 
wanafunzi  wakiwa  wakiwa madarasani  wakiendelea na masomo.
 Akizungumzia tukio hilo,kamanda wa jeshi la Zimamoto Mkoani Iringa, InspektaKennedy Komba alisema kuwa bweni hilo limeteketea lote na kuunguza mali zilizoko katika bweni hilo na chache kuokolewa na wananchi waliowahi kufika eneo la tukio kusaidia  kuzima moto  huo.
Alisema kuwa chanzo cha moto huo imesababishwa nahitalafu ya umeme na hakuna mwanafunzi yoyote aliyejeruhiwa na moto huo. Komba alisema kuwa baada ya jeshi la zimamoto kupata taarifa waliondoka mjini Iringa ambapo  ni  zaidi ya  kilometa 20 hadi  ilipo shule  hiyo  ili  kwenda  kuzima  moto  huo. Hata  hivyo  aliwapongeza wananchi kwa moyo wa ushujaa kujitolea kuzima moto huo na kuwataka kutoa taarifa mapema pindi majanga ya moto yanapojitokeza katika maeneo yanayowazungu.
  “Endapo tungepata taarifa mapema nina amini tungeweza kuokoa vitu vingi zaidi na kuwataka wananchi wasitegemee mtendaji au kiongozi apige simu katika kikosi cha kuzima moto kwani kila mtu ana haki ya kupiga simu 111 katika kitengo cha mawasiliano cha jeshi hilo kuweza kutoa taarifa ya majanga, tumetumia muda mdogo kufika eneo la tukio kutokana  ubora wa gari hivyo nawashukuru sana wananchi kwa taarifa na kuweza kuonyesha ushirikiano katika uzimaji wa moto huo usilete madhara zaidi “ alisema Akizungumzia hasara iliyosababishwa ni kiasi gani Komba alisema hadi sasa hawajapata tathmini kamili ya mali zilizoteketea ila baada ya kazi kukamilika itafahamika ni thamani ya vitu vilivyoungua na kuwekwa wazi kwa wanachi.
 
Mbunge  wa   jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi ambako maafa  hayo yametokea  mbali ya  kuwapa  pore  walimu na  wananchi  wa  Idodi  kwa tukio  hilo  bado  aliwapongeza  wananchi  kwa  umoja  wao kwa  kufika mapema  kuthibiti  moto  huo pamoja na kikosi  cha  Zimamoto kutoka mjiniIringa.
 
Tukio  hilo kubwa  kulikumba  jimbo la Isimani  linaloongozwa na  mbunge  wake  Wiliam Lukuvi ambae ni  waziri  wa  nyumba na ardhi 
 
Akizungumza  kwa niaba ya mbunge  Lukuvi katibu  wa  mbunge  huyo  Thom Malenga alisema  kuwa  wananchi  wamefanyajitihada  kubwa katika  kuthibiti  moto  huo na  kuwa mbali ya mali za  wanafunzi  hakuna madhara  kwa  binadamu.
 
Kuhusu  thamani ya mali  zilizoteketea  kwa  moto  huo  alisema  kwa  sasa  bado mapema  kujua  ila uongozi  wa  shule  hiyo pamoja  na  wazazi na  wananchi wa Idodi  wapo katika  kikao ili  kujua madhara  zaidi  na hasara  iliyojitokeza.
 
 Agosti 25/ 2009  jumla  ya  wanafunzi 13  walipoteza maisha baada ya  bweni hilo kuteketea kwa  moto na  baadhi  yao  kujeruhiwa kwa ajali  kama   hiyo ya  moto ambayo kwa  kipindi hicho moto  huo ulisababishwa na mshumaa.

No comments:

Post a Comment