TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, February 14, 2015

Lyimo atangaza kupeperusha bendera ya TLP katika kuwania Urais wa Tanzaia

max 
Mwanachama wa chama cha siasa cha TLP Bwn Macmillan Lyimo (kushoto) akirejesha fomu ya kuomba kugombea uraisi kwa tiketi ya chama hicho kwa katibu mkuu wa chama hicho Meja Jesse Makundi huku katibu msaidizi wa TLP Bwn Hamad Tao akishuhudia.Picha ilipigwa mwaka 2010 kwa hisani ya http://changamotoyetu.blogspot.com                           
………………………………………………………………………….
Na Happy Shirima-MAELEZO-
Dar es salaam Mwanachama wa chama cha Tanzania Labour Party [TLP] Macmillan Lyimo ametangaza nia ya kugombea nafasi ya uraisi kupitia chama hicho. Lyimo ametangaza azma hiyo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu nia yake ya kuamua kugombea urais kupitia Chama hicho na sababu zilizo mfanya agombee Amesema kuwa sababu zilizomfanya agombee nafasi hiyo kupitia chama hicho ni kuendeleza juhudi za Mwenyekiti wa chama hicho Mhe. Augustino Mrema za kutunza historia nzuri alioiweka kwenye chama hicho wakati wa uchaguzi wa mwaka 1995. ”Mhe.Mrema ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa chama na Mbunge wa Jimbo la Vunjo itakuwa ni aibu na fedheha kwa mtu yeyote kutotambua mchango wa kiongozi huyo wakati akiwa kiongozi serikalini na hatimaye wakati akiwa upinzani toka 1995 ”alisema Lyimo. Aidha amesema kuwa sera kuu ya chama hicho ni amani , kuandaa kizazi kipya na taifa jipya Tanzani litakalo jengwa na misingi mkuu ukiwa ni Mungu kupewa nafasi ya kwanza lengo kuu ikiwa ni kuifanya Tanzania kuwa taifa kubwa la dunia katika kipindi kifupi. Ametoa wito kwa viongozi wa kada zote na wananchi wote kushiriki kwa amani na upendo katika matukio makuu muhimu kwa Taifa hilo ambayo ni kupigia kura Katiba inayopendekezwa ,uchaguzi mkuu na kujenga umoja ili kuepuka ufa uliojitokeza katika masuala ya dini kwa ajili ya mustakabali mzuri wa Tanzania .

No comments:

Post a Comment