TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, February 13, 2015

Tamasha la Pasaka kamili kusaidia jamii



WAANDAAJI wa Tamasha la Pasaka wamesema wataendelea kusaidia jamii katika kila tamasha lao litakapofanyika.
 
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam  leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya miaka 15 ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama ilieleza kuwa kwa miaka yote hiyo wamekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii.
"Tumedhamiria kwa dhati kusaidia jamii kwa namna mbalimbali, hii haitakuwa mara ya kwanza kwetu kufanya hivyo, tulisaidia matamasha yaliyopita, tutaendelea na juhudi hizo kila tutakapopata nafasi, “ alisema Msama katika taarifa hiyo.
 
Alisema katika miaka yao 15 wamesaidia sehemu mbalimbali ikiwemo waathirika wa mabomu yaliyotokea kwenye kambi ya jeshi Gongo la Mboto, Dar es Salaam.

Pia alisema Tamasha la Pasaka wamewahi kusaidia fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji ya biashara wanawake wajane. “Tangu mwanzo tulishajionesha kwamba tuna dhamira ya dhati na ndio maana tunafurahia sana kila mwaka kwamba nasi tunashirikiana na jamii na hata mwaka huu tutafanya hivyo,” alisema Msama.
 
Pia alisema kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali wamekuwa wakitoa semina za kusaidia wajane, yatima na vijana wasio na ajira ikiwa ni pamoja na kuwapa mbinu za kufanya biashara na kuachana na dawa za kulevya.

"Mimi naamini mtoaji wa vyote ni Mwenyezi Mungu, hivyo ni busara upatapo kidogo ugawane na wasiojiweza ili kuongeza thawabu yako.

Kuhusiana na tamasha la mwaka huu, alitamba kuwa wamewaandalia mashabiki wa muziki wa Injili mambo mazuri  yatakayowaburudisha na kuridhika.

No comments:

Post a Comment