TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, February 11, 2015

Umeme kichocheo cha ukuaji wa uchumi nchini - Simbachawene Greyson Mwase na Rhoda James, Dar es salaam


Waziri wa  Nishati na Madini, George  Simbachawene amesema kuwa nishati ya  umeme ni  kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa nchi hivyo  serikali ipo  tayari kushirikiana na wadau mbalimbali  ili kuhakikisha kuwa nishati ya umeme inakuwa ni  ya uhakika.

Simbachawene aliyasema hayo kwenye ufunguzi wa mkutano  uliokutanisha wadau wa nishati kutoka sekta binafsi, asasi za kiraia na wataalamu kutoka  Wizara ya Nishati na Madini,  katika  hoteli ya Protea  jijini  Dar es salaam. Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kubadilishana ujuzi na uzoefu katika  usimamizi wa miradi ya umeme.

Alisema kuwa, Serikali  imekuwa ikiandaa mikakati mbalimbali  ya  kuhakikisha wananchi wote wanapata nishati ya umeme  ya uhakika na kwa gharama nafuu na kusisitiza kuwa ili kufikia lengo  hilo, Serikali imebuni  vyanzo mbalimbali kama vile umeme wa jua, upepo, tungamotaka,  jotoardhi na  gesi asilia kulingana na Sera ya Nishati ya Mwaka  2003.

“ Umeme wa Gridi ya  Taifa pekee hautoshi kabisa katika kuhakikisha wananchi wote wanaunganishwa na huduma ya umeme  ndio maana  Serikali imebuni  vyanzo  vingine ili   kuhakikisha kuwa yale maeneo ambayo  hayajafikiwa na  umeme wa gridi ya   taifa, wanapata umeme na kupunguza  umasikini kupitia nishati hiyo, “alisema Simbachawene.

Wakati huohuo, Meneja Uhifadhi kutoka Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala ya  utunzaji wa mazingira na maisha ya wanyamapori (WWF; World  Wide Fund for  Nature) Nchini  Dk. Amani  Ngusaru akizungumzia hali ya umeme duniani alisema kuwa  takribani watu bilioni 1.6 hawana  nishati ya uhakika ya umeme huku bilioni 2.4 wakiwa hawana nishati ya uhakika kwa ajili ya kupikia. Aliongeza kuwa kwa  upande wa Tanzania kwa kipindi cha miaka 10 Serikali imefanya  jitihada mbalimbali katika kuhakikisha inapunguza upungufu wa umeme nchini.

Akizungumzia  changamoto katika utekelezaji wa miradi ya  umeme nchini Dk. Ngusari alisema teknolojia, fedha za uendeshaji na ukosefu wa  ujuzi  zinazuia upatikanaji  wa umeme wa uhakika. Akielezea mchago wa WWF katika nishati ya umeme Dk. Ngusari alieleza kuwa, WWF imekuwa ikisaidiana na  Serikali katika kuongeza upatikanaji wa nishati mbadala na  kuongeza matumizi ya bayomass.

No comments:

Post a Comment