TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, February 10, 2015

JENGO MOJA MTAA WA LIBYA/MOSKI-KARIAKOO JIJINI DAR UMEZUKA MOTO MKUBWA NA KULETA MACHAFUKO

 Moto uliozuka mapema leo na kuteketeza majengo matatu ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika makutano ya Mtaa wa Libya na Mosque jijini Dar es Salaam.
Moto Mkubwa umezuka mapema leo kwenye moja ya nyumba pichani iliopo mtaa wa Libya na Moski -Kariakoo jijini Dar,na kupelekea mali kadhaa kuteketea.Kikosi Kazi cha Globu ya Jamii kilkuwepo eneo la tukio na kukuletea kila kilichojiri ,lakini kwa taarifa kutoka kwa mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio walieleza kuwa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika rasmi,Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio kuhakikisha amani na utulivu unakuwepo huku kikosi cha zimamoto na magari nayo yaliendelea  kuwasili kupambana na moto huo..
Mmoja wa wapiga picha akitazama kwa mshangao moto mkubwa uliokuwa ukiendelea kuwaka kwa nguvu na kuteketeza baadhi ya mali zilizomo ndani ya jengo hilo lililopo mtaa wa Jamuhuri na Moski-Kariakoo jijini Dar.

Moto huo ulioanza majira ya saa tatu asubuhi kwa kuanza kufuka moshi na baadae kuwaka na kuteketeza eneo lote la juu ya majengo hayo.
Akizungumza leo na waandishi wa habari katika eneo la tukio Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina wa Jeshi la Polisi Suleiman Kova amesema vikosi vya uokoaji na Zima Moto vimefanya ushirikiano katika kuzima moto huo baadhi ya maeneo na kuokoa maduka katika majengo hayo.

 ‘’Vikosi vya zima moto vimefanya ushirikiano kwa kuleta magari sita ya kuzima na uzimaji na kufanikisha kuuzima moto ambao ulikuwa mkubwa’’amesema Kova.

Kova amesema kuwa vikosi vya ukoaji vya zima moto vimefanya kazi kwa ushirikiano ambavyo ni  Zima moto za Uwanja wa Ndege,Zima Moto ya Kampuni ya Ulinzi ya Altimate,Night Support ,pamoja  na Kikosi cha Zima moto ya Jiji.

Amesema kuwa  chanzo cha moto bado hakijafahamika mpaka sasa.Amesema uchunguzi wa kubaini chanzo cha moto huo bado unaendelea .Aidha Kamanda Kova amesema thamani ya vitu vilivyoungua katika majengo hayo bado wanaendelea na uchunguzi lakini hakuna maafa katika moto huo.

Naye Kamishna msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Kanda Maalum ya Dar es salaam,Jeswald Nkongo amewataka wananchi kutoa taarifa mapema pindi waonapo matukio ya moto na sio kudharau kwa kuamini kuwa moto ni mdogo na wanaweza kuudhibiti.
 Baadhi ya Polisi kutoka Jeshi la Polisi na Kikosi cha Zimamoto vikiwasili eneo la tukio mtaa Libya na Moski.
 Baadhi ya wasamaria wema wakiondoa gari iliokuwa jirani na jengo linaloteketea kwa moto
 Baadhi ya Polisi kutoka Jeshi la Polisi wakiwa katika eneo la tukio,huku wananchi nao wakishuhudia tukio hilo la kusikitisha.
Moja ya Gari  la zimamoto likiwa limewasili eneo la tukio hivi punde.

No comments:

Post a Comment