TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Monday, December 28, 2015
ARUSHA TOURISM MARATHON LUCIAN NA FABIAN JOSEPH WATAMBA
Baadhi ya wanariadha walifanikiwa kupata zawadi katika shindano Arusha tourism Marathon wakiwa katika picha ya pamoja .
Afisa utalii wa tanapa fredy shirima akiwa anamkabidhi zawadi Mwanariadha Reginal Lucian baada ya kushinda kilometa 42,baada ya kukimbia kwa muda wa 1:00:05.
Na Woinde Shizza,Arusha
Mwanariadha Reginal Lucian alifanikiwa kushinda kwa upande wa
wanaume,katika shindano la Arusha Tourism Marathon baada ya kutumia
muda wa 1:00:05,akifatiliwa na mwanariadha wa kimataifa, Fabian Joseph
1:00:14, nafasi ya tatu,Gabriel Gerald muda wa 1.00.37.
katika mashindano hayo ya kilomita 42, yaliyoandaliwa na taasisi la
Alfredo Shahanga na Mwanariadha kutoka Kenya, Evance Kiblanget
alishika nafasi ya nne baada ya kutumia muda wa 1:07 huku nafasi ya
tano ikishinda Wilbart Peter na nafasi ya sita akishinda mwanariadha
wa kimataifa Dockson Marwa.
Kwa upande wa wasichana Angelina Tsere alishinda kwa kutumia musa wa
1:11:17, akifuatiwa na mwanariadha wa kimataifa Mary Naali muda wa
1:11:23, nafasi ya tatu ulikwenda kwa Mkenya Ladis Shemayo aliyetumia
muda wa 1:11:37 .
Katika mashindano hayo, ambayo mgeni rasmi alikuwa ni ,Afisa Michezo
wa Mkoa wa Arusha,Mwamvita Okeng'o mshindi wa kwanza hadi wa 10
walipewa zawadi.
Viongozi wengine waliotoa zawadi ni pamoja na Katibu Mkuu wa kamati ya
Olimpic Tanzania(TOC), Filbert Bayi, Rais wa zamani wa chama cha
riadha nchini(TAAA) Franis John na Afisa Utalii wa TANAPA Fred
Shirika.
Katika mashindano hayo, washindi wa kwanza walipoewa zawadi ta
shilingi 500,000, washindi wa pili, 250,000,washindi wa tatu, 200,000,
wanne 150,000 na wa tano 100,000 ambapo wa 6 hadi 10 pia walipewa
zawadi.
Wakizungumza wakati wa kutoa zawadi, Bayi na Okeng'o walipongeza
wanariadha waliojitokeza kwa kuonesha upinzani mkubwa na kutoa wito
mashindano haya yafanyike kila mwaka ili kusaidia kukuza utalii wa
ndani.
Mkurugenzi wa Alfredo Shahanga kwa upande wake, alisema lengo la
mashindano hayo lilikuwa ni kuhamasisha utalii wa ndani, kuhamasisha
amani mkoa wa Arusha na kutaka sasa riadha itumike kutangaza utalii.
Mashindano hayo ambayo ni sehemu ya mashindano ya Arusha Tourism
Festival ni mara ya kwanza kufanyika nchini, yalidhamiwa na shirika la
hifadhi za Taifa(TANAPA), kampuni ya vinywaji ya SBC(T) Ltd,radio
Sunrise,BiG Expedetion,Mega Trade Investment,Tanzania Breweris na
Criative Solution.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment