TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, December 31, 2015

WAKAZI WA WILAYA YA MBOGWE WAPATA UJASIRI WA KUTUMBUA MAJIPU BAADA YA MAFUNZO YA URAGHABISHI



Ndugu Halidi Abdu toka kijiji cha Shenda chenye wakazi wapatao 2,800 katika kata ya Masumbwi wilaya ya Mbogwe mkoani Geita;akihojiwa na mtangazaji wa redio free africa william bundala almaarufu Kijukuu cha Bibi k akielezea jinsi walivyoweza kuwaadaa viongozi wao waweze kuwasomea taarifa yao ya mapato na matumizi.


Waraghbishi toka vijiji vya Iponya, Nyakasumula, Bukandwe na Shenda wakiwa katika pichaya pamoja na mwenyekiti na mtendaji wa kijiji cha Shenda.

Na Krantz Mwantepele, Geita 
Ni miaka mitatu na miezi nane toka mraghbishi Fedson Yaida na wenzake toka vijiji vya jirani kukutana na Chukua Hatua. Ni rafiki waliyekutana naye mwaka 2011 katika mazungumzo maalumu ambayo walitakiwa kuyafikisha kwa wananchi wenzao wa vijiji vya Shenda, Iponya, Nyakasumula na Bukandwe katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita. Ni katika mazungumzo hayo ya siku tatu, ambayo Fedson toka kijiji cha Shenda alibadilishwa na kuwa mraghbishi wa aling’amua uwezo alio nao katika kusimamia rasilimali za kijiji chao, suala ni angezisimamiaje wakati yeye si kiongozi na ni jukumu la wanakijiji wote. Katika mazungumzo hayo rafiki yao,Chukua Hatua aliwaambia, “Ni jukumu lako Fedson na waraghbishi wengine mliopo hapa, ni jukumu lenu la msingi kuj i t aj i r i sha kwa taarifa na maarifa. Kwa kufanya hivyo mtakuwa na uwezo wa kujenga hoja mkizithibithisha na vielelezo. Hivyo ni jukumu lenu kujua ni wapi na toka kwa nani mtapata taarifa na vielelezo vya hoja yenu. Uzito wa hoja na maelezo kwa uthibitisho ni silaha muhimu kama mnataka kushawishi wenz e n u k u c h u k u a hatua.” Baada ya maelezo hayo walitakiwa kwenda kutembelea halmashauri ya wilaya yao, wakati huo ikiitwa Bukombe. Na baadhi ya maeneo hayo ni ofisi za Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri. Maelezo haya yalilenga katika haki ya kupata taarifa, kwa mujibu wa ibara ya 18 ya Katiba.


Ujasiri huo wenye msukumo wa ndani toka kwa mraghbishi mmoja kwenda kwa wenzake kwa njia ya kuwashirikisha aliyopatiwa na Chukua Hatua, ndio umekuwa chanzo kikubwa cha mafanikio ya pamoja ya wana Shenda katika kusimamia rasilimali zao. Safari ya mwandishi katika kijiji cha Shenda ilimtia moyo sana. Alikutana na waraghbishi toka vijiji vya Shenda, Ipoja, na Buluhe. Mkusanyiko huu ulikuwa na watu wa kada mbalimbali; walimu, wajumbe wa serikali ya kijiji, wazee, na wakulima. Aliwakuta wakiwa pamoja na Mwenyekiti na Mtendaji wa kijiji chao. Na wote kwa pamoja walikuwa wanazungumzia mustakabali wa maendeleo ya kijiji chao. Na kwa haraka aligundua wote wamekuwa waraghabishi, akajiuliza aliyekutana na Chukua Hatua alikuwa mmoja, lakini sasa wapo kwa makundi na wote wanajitambulisha kama waraghbishi. Hamu na shauku yao ya kutaka kusimamia rasilimali zao ndio imekuwa nguzo kubwa ya wao kuweza kufuatilia matumizi ya vyanzo vya mapato ya kijiji chao. Ni miaka miwili imepita toka wananchi hao wautoe uongozi wa kijiji madarakani kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha. Kwa pamoja waliongozana na mwenyekiti wao pamoja na mtendaji wa kijiji na mpaka ofisi ya kata na kuwakabidhi kwa polisi. Ubadhirifu huo ulithibitishwa na taarifa ya ukaguzi, iliyoonyesha upotevu wa kiasi cha shilingi milioni mbili laki tisa na elfu hamsini (2,950,000/-). Taarifa hiyo ilisomwa katika mkutano wa hadhara na viongozi kutakiwa kulipa pesa hizo ambazo walizirudisha.



K wa n z a wa meanza na ujenzi wa zahanati kwa k u k a m i l i s h a msingi wake. Na wananchi wamekubali kuchangia, kila kaya matofali 50 na wengine w a m e c h a n g i a mawe. Uhai umerudi tena na kila mtu ana shauku ya kufanikisha ujenzi huo. Lakinisi hivyo tu wanataka kukamilisha pia na ujenzi wa zahanati ya kijiji. Haya yote yakiwa ni matunda ya ushirikiano kati ya uongozi wa kijiji na waraghbishi na wanakijiji wote kwa ujumla. “Tumekaa muda mrefu sana bila zahanati hasa kwa ajili ya kina mama. Ni kilometa tano kutoka hapa mpaka zahanati ya jirani. Na kijiji chetu kama unavyokijua, hakina teksi, labda tumbebe kwa tela la ng’ombe au punda kama huna baiskeli. Tukajiuliza kwanini tusiiambie serikali yetu tujenge zahanati hapa karibu,”anafafanua Abdi Haridi. Lakini si hivyo tu Mwenyekiti ameshahamasisha kila mwananchi achangie mawe, achangie matofali. Kwa sasa wameonela kumalizia kabisa ofisi yao ya kijiji. Ya sasa ipo katika hali mbaya harufu ya kinyesi cha popo na jengo lenyewe lina nyufa ikinyesha mvua kubwa itakuwa ni shida inaweza hata kuanguka na hapa ndio makao makuu ya kijiji.










Gati zilizopo Shenda zinatokana na waraghbishi na wananchi kufuatilia suala hilo kwa karibu. Kwa sababu ni kitu walichokiomba wapatiwe na serikali. Baadhi ya vitongoji vya kijiji hicho vimetenganishwa na barabara. Hivyo wametaarifiwa kwamba gati haiwezi kuvuka barabara. Ili hali kwa baadhi ya viongozi wao gati imevuka barabara,” mraghbishi Abdi anauliza, “Lakini ukienda pale makao makuu ya kata pale unakuta gati imewekwa kwa kiongozi. Nikauliza swali pale mbona kule Shenda tumeambiwa gati haiwezi kukata barabara ndio maana wananchi wa upande wa pili wa kijiji hawapati maji. Imekuwaje kwa kiongozi imekata barabara na kuingia mpaka mgongoni mwa nyumba yake? Barabara ile ile niliyoambiwa gati haiwezi kukatiza ndio hiyo hiyo imetumiwa kukatiza gati.” Kaloras Majura, mraghbishi kutoka kijiji cha Bukandwe kutoka kata yenye jina hilo hilo la Bukandwe, pamoja na kwamba yeye ni mraghbishi lakini pia alikuwa ni mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi ya kijiji chao. 


Suala lingine ambalo limejitokeza ni kuhusu mganga wa zahanati ya kijiji cha Bukandwe, ambaye alikuwa akiwachangisha wananchi kiasi cha shilingi za kitanzania elfu kumi (10,000/-) za mfuko wa afya. Alichokuwa akifanya wakati anawaandikia alikuwa akiweka kumbukumbu tofauti za mwaka. “Kama mtu katoa hela mwaka huu yeye anamuandikia katoa mwaka 2012 na wengine mwaka 2013. Baada ya muda akawa amehamishwa sasa watu wanapokwenda pale zahanati wanaambiwa kwamba wewe muda umeshakwisha ulitoa mwaka juzi hivyo uanze upya,” anasimulia Majura Kutokana na nafasi yake ya uraghbishi Majura ameweza kukaa na kamati ya kijiji ya afya. Na ameishawishi kamati kuwasiliana na watu waliolipa kuandaa vielelezo vyao na kufanya mawasiliano na mganga mkuu wa wilaya, ili waweze kujua wanachukua hatua gani kuhusu huyo mganga. Lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha kwamba wananchi wanarudishiwa fedha zao walizochanga.

Si kitu kirahisi sana pia kufanya uraghbishi kwa sababu mara kadhaa waraghbishi wamekuwa wakitishiwa tishiwa ili wasiulize ulize maswali na kuhamasisha wananchi , lakini bado mambo yameendelea. “Sisi waraghbishi tunapata muda mgumu sana tunakutana na watu tofauti na viongozi tofauti. Tunatishiwa amani, ila na sisi tutapambana kama tulivyokwisha kupambana mpaka dakika ya mwisho ili haki yetu ipatikane. Tukianza kuyatafuta mashirika ili tushirikiane nayo katika kuweka mambo sawa, kama hivi. Tayari tunaonekana siye wabaya kwa wale viongozi wa juu. Kwamba sisi tunawapondea wale. Basi sisi tunaomba waje wale wakubwa zaidi, waje watuulizie nini kinaendelea ili tuwaambie ukweli,” anaeleza kwa kujiamini mraghbishi Abdi Haridi wa Shenda. Harakati hizi zinaungwa mkono na mwenyekiti wa kijiji cha Shenda, Masumbuko Kwileka, kama anavyosema kuhusu warghabishi, 

No comments:

Post a Comment