Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam .
Pia ameitaja Iringa na Kilimanjaro kuwa ni mikoa ambayo imeweza kuthibiti ugonjwa huo hatari.Mwalimu akitoa takwimu za ugonjwa huo, amesema hivi sasa kuna wagonjwa wapya 76, hivyo idadi ya wagonjwa wapya imefikia 493 na kifo kimoja.“Hadi sasa mkoa wa Morogoro vijijini unaongoza kwa wagonjwa 56, ukifuatiwa na Arusha (28), Rorya (22), Bunda (21) na Kigoma vijijini 17.” Mhe. Mwalimu amesema”Aidha Mhe.Mwalimu ametoa agizo kwa wakuu wa mikoa na wilaya kuwa ni marufuku kuuza matunda yaliyokatwa barabarani,kuuza vyakula katika mazingira yasiyo safi na salama,huku akitaka kuandaliwa kwa taarifa za kila wiki kuhusu ugonjwa huo.Akitoa rai kwa wakuu wa wilaya na mikoa, kuwa walete taarifa sahihi za mlipuko wa ugonjwa huo kwa ajili ya kuudhibiti. Na kwa kuwasisitiza watanzania kunywa maji safi na salama na kunawa mikono kwa maji safi na salama.
No comments:
Post a Comment