Baadhi ya kinamama wa wilayani Rufiji Mkoani Pwani waliohuduria mkutano wa mradi wa Kuwaunganisha Wanawake wenye lengo la kujifunza ujasiriamali na kutunza mazingira wakifuatilia kwa makini, Kampuni ya Tigo ndio mdhamini wa mradi huo.
Mkurugenzi Mtafiti Kinga Jamii toka REPOA, Dkt. Flora Myamba akiongea na waandishi wa habari na kinamama wa wilayani Rufiji waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali na utunzaji wa mazingira programu ijulikanayo “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake”. Wengine toka kushoto John Kikomo Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa mazingira(JET) na Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas
Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas akimkabidhi simu Bi.Habiba Mtigino kutoka kijiji cha Umwe wilayani Rufiji. Jumla ya simu 200 zilitolewa na Kampuni ya Tigo kwa Wanawake wasiokuwa na uwezo wa kununua simu wilayani humo kupitia mpango unaojulikana kama, “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake”
Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa mazingira(JET), John Kikomo akionyesha kimoja kati ya vyeti watakavyopewa kinamama walioshinda shindano la kutunza mazingira wilayani Rufiji. Mpango huo ulidhaminiwa na Tigo na asasi tatu zisizo za serikali za REPOA, KIDOGO KIDOGO na Care International.
Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas akimkabidhi simu Bi.Mozza Salum kutoka kijiji cha Umwe wilayani Rufiji. Jumla ya simu 200 zilitolewa na Kampuni ya Tigo kwa Wanawake wasiokuwa na uwezo wa kununua simu wilayani humo kupitia mpango unaojulikana kama, “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake”
Baadhi ya kinamama wa wilayani Rufiji Mkoani Pwani waliohuduria mkutano wa mradi wa Kuwaunganisha Wanawake wenye lengo la kujifunza ujasiriamali na kutunza mazingira wakifuatilia kwa makini, Kampuni ya Tigo ndio mdhamini wa mradi huo.
No comments:
Post a Comment