Mkurugenzi wa Huduma za mifungo Tanzania katika wizara ya Kilimo, mifugo na Uvuvi, Dkt. Abdu Hayghaimo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kusikitishwa kwao kama wizara kutokana na wanyama kuadhibiwa bila hatia yoyote kwenye migogoro kati ya wakulima na wafugaji hapa nchini. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa wizara ya kilimo, mifugo na Uvuvi, Judith Mliwa.
Hayghaimo amesema kuwa wananchi wenye tabia ya kuwadhuru wanyama waiache mara moja kwa kuwa wanyama hao wanaongozwa na binadamu kwenye maeneo yasiyowahusu wanayama. Amesema kuwa kwa mujibu wa sheria ya ustawi wa wanyama wanahaki ya chakula, maji, mahali pazuri pakupumzika, kulindwa dhidi ya maumivu yeyote, magonjwa na mateso ikiwa pamoja na kuwasaabishia kifo.Pia wizara imewatahadharisha wananchi wote wanaochukua sheria mkononi na kusababisha madhara makubwa yasiyokubalika kutokana na migogoro ya migogoro ya wakulima na wafugaji kuwa huwanyima wanyama haki zao ni uvunjifu wa amani.Jamii imeshauriwa kuwa itafute suruhu ya migogoro hiyo kupitia kamati zitakazo matumizi endelevuya ardhi kwa mujibu wa walaka unaoandaliwa na wizara.
No comments:
Post a Comment