TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, December 29, 2015

WAZEE WAMWOMBA RAIS DKT. MAGUFURI AWAKUMBUKE

Wazee waishio kata ya Kimandolu wilaya ya Arusha mkoani Arusha wamemuomba Rais John Pombe Magufuli awakumbuke wazee kwa kuhakikisha kuwa wanapata huduma bora za afya ,lishe bora na kupata mafao ya uzeeni kutokana na mchango wao katika ujenzi wa taifa kupitia sekta binafsi na za serikali tangu nchi ipate uhuru.
Wazee hao ambao wanaishi katika hali ngumu za kimaisha na wengine kutokua na uhakika wa milo mitatu huku wakikabiliwa na jukumu la kulea familia zao pamoja na wajukuu licha ya uzee unaowakabili pamoja na kutokua na kipato cha uhakika na wengine kutokua na nguvu ya kufanya kazi.

Amon Mwita ni mzee anayeishi kata ya Kimandolu alisema kuwa licha ya mchango wao katika uchumi wa nchi na maendeleo ya taifa tangu kipindi cha uhuru wamekua ni watu wa kusahaulika jambo ambalo linawafanya waiishi maisha ya shida.

Mwita alisema kuwa kwa muda mrefu wamekua wakipigwa danadana juu ya kupatiwa matibabu bure hali ambayo imesababisha afya za wazee wengi kuzoroto kwani wengine hukosa fedha za matibabu na kujikuta wakipoteza maisha kwa kukosa matibabu.

Navoneiwa Maeda ni mzee ameitaka Serikali iwathamini wazee kwani ni kundi linaloishi katika mazingira magumu na bado halijapewa kipaumbele na serikali jambo ambalo linawaumiza hivyo ameiomba serikali na jamii ichukue jukumu la kuwalea wazee na kuwatunza.

Mwenyekiti wa Baraza la wazee mtaa wa kimandolu Emmanuel Mollel asema kuwa wazee wengi wamekua wakijificha majumbani ingali wagonjwa bila kupata matibabu na wengine kutopata mlo wa siku kutokana na hali ngumu za kiuchumi walizonazo hivyo ameiomba jamii ijitokeze kuwasaidia wazee.

No comments:

Post a Comment