Wakulima
wote nchini wameaswa kutumia vizuri mikopo wanayopewa ili kuweza kutimiza
malengo yao binafsi na ya Serikali katika kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na
usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania.
Mama
Masenza alisema kuwa wakulima wakitumia mikopo waliyopewa kwa malengo husika
watafika mbali na kuweza kuchagiza mikakati ya Benki hiyo katika kusaidia
Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kilimo kibiashara ili
kukuza uchumi na kupunguza umaskini.
Mama
Masenza aliwaomba wakulima hao kuwa
Mfano Bora na wanaojitambua vilivyo, hasa nia ya kutoka katika kiwango fulani
cha maisha kwenda katika hatua nyingine za juu zaidi kimaisha kwa kuongeza
kipato na ubora wa kimaisha kwa ujumla kupitia huduma za TADB.
“Nawasihi
kutotumia pesa hizi kinyume na malengo yaliyokusudiwa, kwani kwa kufanya hivyo,
siyo tuu tunaiua Benki yetu bali pia tunajimaliza wenyewe kiuchumi. Wito wangu
kwenu ni kujipanga kwa dhati ili kuweza kutimiza malengo makuu ya mikopo hii
ambayo ni kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa
kusaidia upatikanaji wa fedha na sera nzuri zitakazosaidia maendeleo ya kilimo
nchini,” aliongeza.
Naye,
Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi amesema kwamba Benki yake
imedhamiria kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini ili
kuchagiza na kusaidia kuwezesha Sekta ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu
kwenda kilimo cha kibiashara ili kukuza uchumi na kupunguza umaskini nchini.
Bw.
Samkyi alisema TABD imejizatiti kuchangia kwa kiasi kikubwa katika mapinduzi ya
kilimo kwa kuongeza tija na upatikanaji wa mikopo ya riba nafuu maalum kwa sekta
ya kilimo, kama njia ya kuleta Mapinduzi yenye tija kwa wakulima nchini.
“Benki
imejipanga kutoa mikopo yenye riba nafuu katika muda mfupi, wa kati na mrefu
kwa Wakulima wadogo wadogo, wa kati na
wakubwa, hususan kuziba pengo la upatikanaji wa fedha za kwenye mnyororo wa
ongezeko la thamani katika tasnia za kilimo, mifugo, uvuvi na mazao ya misitu
(ufugaji nyuki),” alisema Bw. Samkyi.
Mkurugenzi
huyo alisema kwamba kwa kuanzia walengwa wakuu wa TADB ni wakulima wadogo
wadogo, hatahivyo, hata wale wakulima wa kati na wakubwa watahudumiwa.
“Sera
ya TADB ni kutathmini mnyororo mzima wa thamani ili kutambua mapengo na
mapungufu yanayohitaji utatuzi, na ambayo utatuzi wake utaongeza tija na uwezo
wa ushindani kwenye masoko, na hivyo kukuza uchumi wa walio wengi na kupunguza
umaskini,” aliongeza.
Akizungumzia
malengo ya TADB kwa upana, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo,
Bibi Rosebud Kurwijila alisema kuwa Benki inalenga kutelekeza kwa vitendo
Maelekezo ya Serikali ya kupunguza changamoto zinazomkabili mkulima.
Aliongeza
kuwa kwa sasa Benki inalenga kusambaa nchi nzima kwa kuanzisha Ofisi za Kikanda
ndani ya miaka mitano ijayo, kuwajengea uwezo na kuanzisha Programu Maalumu ya
Vijana wajihusishao na shughuli za Kilimo cha kibiashara na kushirikiana na
wadau wengine kuhuisha shughuli za umwagiliaji na miradi ya kisasa ya umwagiliaji.
Mkurugenzi wa Mikopo na
Biashara wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Robert Pascal
(Kulia) akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kisheria wa Benki, Bibi
Neema Christina John (aliyevaa miwani) wakati wa uhakiki wa fomu zilizojazwa na
moja kati ya vikundi vilivyofanikiwa kupata mkopo kutoka Benki hiyo.Mwanasheria mwandamizi wa TADB, Bibi Salome Masenga (Kulia) akimuelekeza mmoja wa wanakikundi waliopata mikopo kutoka Benki hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (Aliyesimama) akiwapungia wakulima waliojitokeza wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya mikopo kati ya TADB na wakulima wadogo wadogo wa mkoa wa Iringa, katika kijiji cha Igomaa, wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), wakiwapungia wakulima waliojitokeza wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya mikopo kati ya TADB na wakulima wadogo wadogo wa mkoa wa Iringa, katika kijiji cha Igomaa, wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (Kushoto) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bibi Amina Masenza (Kulia) wakifuatilia kwa makini matukio wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya mikopo kati ya TADB na wakulima wadogo wadogo wa mkoa wa Iringa, katika kijiji cha Igomaa, wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (Kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Bw. Kasunga (Kulia).
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Thomas Samkyi (aliyesimama) akizungumza wakati wa hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment