Nchi mbalimbali duniani zimekuwa na sera mahususi kwa ajili ya kukaribisha wawekezaji mbalimbali kuja kuwekeza kwenye nchi zao ili kuweza kupata kipato kupitia kodi mbalimbali na faida nyingine kama ajira kwa wenyeji, uboreshwaji wa miundo mbinu n.k. Moja ya nchi hizoni pamoja naTanzania.
Tanzania ilibadilisha sera zake za kiuchumi mwanzoni mwa miaka ya 1990, kwa kutoa fursa kwa sekta binafsi kuweza kumiliki uchumi. Sera hii ilivutia wawekezaji wengi toka nje na ndani kuwekeza katika sekta mbalimbali, moja ya maeneo ambayo wakezaji wamejikita ni sekta ya madini. Shinyanga ni moja kati ya mikoa yenye utajiri mkubwa wa madini nchini na hivyo kuvutia wawekezaji wakubwa katika sekta hiyo. Mfano mzuri ni kampuni ya Barrick inayomiliki mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama mkoani humo.
No comments:
Post a Comment