TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, December 29, 2015

UBADHIRIFU WA FEDHA NA RASILIMALI WAPUNGUA VIJIJINI KWA VIONGOZI KUHOFIA KUCHUKULIWA HATUA NA WAKAZI WA MAENEO HAYO.














 Pamoja na Shenda kuonekana kwamba kwao maji yameshaanza kutoka katika mabomba, bado kuna changamoto nyingi za kuwezesha kukamilika kwa mradi huo wa maji. Na waraghbishi wapo mstari wa mbele kufuatilia nini kinachoendelea kwenye mradi huo. Ni mradi ambao waliomba wapatiwe na utekelezaji wake umeshaanza ingawa baadhi ya maeneo bado hawapati maji.   “Mradi huu wa maji ni sawa na hakuna. Sisi wananchi wa Shenda tumechangia nguvu zetu. Tumechangia asilimia yetu tuliyoambiwa na serikali. Serikali ikachangia asilimia yake, ina maana kilikuwa ni kisima tu cha vitongoji vine vya kijiji chetu. Tuna tenki lile pale limeshakamilishwa.  Mashine ipo kule kwenye chanzo cha maji. Italike kule, lakini kijiji kizima kuna gati nane tu. Kuna vitongoji vingine havina gati. Kitongoji kizima kinapewa gati moja ebu niambie kitakidhi wangapi?” anauliza Abdi Haridi mraghbishi wa Shenda.

Gati zilizopo Shenda zinatokana na waraghbishi na wananchi kufuatilia suala hilo kwa karibu. Kwa sababu ni kitu walichokiomba wapatiwe na serikali. Baadhi ya vitongoji vya kijiji hicho vimetenganishwa na barabara. Hivyo wametaarifiwa kwamba gati haiwezi kuvuka barabara. Ili hali kwa baadhi ya viongozi wao gati imevuka barabara,” mraghbishi Abdi anauliza,  “Lakini ukienda pale makao makuu ya kata pale unakuta gati imewekwa kwa kiongozi. Nikauliza swali pale mbona kule Shenda tumeambiwa gati haiwezi kukata barabara ndio maana wananchi wa upande wa pili wa kijiji hawapati maji. Imekuwaje kwa kiongozi imekata barabara na kuingia mpaka mgongoni mwa nyumba yake? Barabara ile ile niliyoambiwa gati haiwezi kukatiza ndio hiyo hiyo imetumiwa kukatiza gati.” Kaloras Majura, mraghbishi kutoka kijiji cha Bukandwe kutoka kata yenye jina hilo hilo la Bukandwe, pamoja na kwamba yeye ni mraghbishi lakini pia alikuwa ni mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi ya kijiji chao.  







No comments:

Post a Comment