TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, January 26, 2015

MBUNIFU WA MAVAZI WA KIMATAIFA, SHERIA NGOWI AMVALISHA RAIS MPYA WA ZAMBIA

Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum  (Presidential suit) iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi akikagua gwaride rasmi kabla ya kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia. Guy Scott, of Scottish 

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, SAID MECK SADIK AZINDUA TAWI JIPYA LA UCHUMI SUPERMARKET MBEZI KAWE

001
Mkurugenzi Mkuu wa Uchumi SuperMarket (Afrika mashariki), Jonathan Ciano (kulia) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik katika ufunguzi wa Tawi jipya la Uchumi lililoko Mbezi Kawe karibu na ukumbi wa Rainbow jijini Dar es Salaam.
002
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Said Meck Sadick akizungumza na wasambazaji na Wafanyakazi wa Uchumi Supermarket wakati wa Uzinduzi wa Tawi Jipya la Duka hilo.

Tigo Music yazinduliwa rasmi Tanzania.

unnamed1
Mwanamuziki Profesa J akiimba katika uzinduzi huo.

MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA NHIF YATOA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI WASIO KATIKA SEKTA RASMI

 001
Meneja Kiongozi wa Bima ya Afya CHIF Kanda ya Ilala, Christopher Mapunda akifunga semina ya siku tatu ya viongozi wa SACCOS za wajasiriamali zilipo Mansipaa ya Ilala iliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWEBLOG
002
Afisa Matekelezo Bima ya afya NHIF kanda ya Ilala, Hipoliti Lello akifafanua jambo kuhusina na kiwango cha uchangiaji kwa wajasiriamali ni shilingi za kitanzania 76,800 ambacho kinamwezesha mjasiriamali kuweza kupata matibabu kwenye zahanati, kituo cha afya, hospital za wilaya, mikoa na za rufaa nchini.
 Raymond akichangia mada yake wakati wa semina hiyo

WASANII MKOANI IRINGA WAMEMTUNGIA WIMBO MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA IRINGA MJINI FRANK KIBIKI

20150123_123538MSANII wa muziki wa kizazi, kipya mjini Iringa, ONE LEE akitoa zawadi kwa mwandishi wa Habari Frank Kibiki kwa niaba ya wasanii wenzake.
================================================
MSANII wa muziki wa kizazi, kipya mjini Iringa, ONE LEE akitoa zawadi  kwa mwandishi wa Habari Frank Kibiki kwa niaba ya wasanii wenzake, ambaye hivi karibuni alitangaza nia ya kugombea  ubunge katika jimbo la Iringa mjini.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa,  wasanii hao walisema wameamua kutengeneza wimbo huo kutokana na mchango mkubwa wa mwanahabari huyo, katika fani yao.
Msanii huyo Richard Kayombo  ‘One Lee’ ambaye alikabidhi wimbo kwa niaba ya wasanii wenzake alisema wimbo huo, unamtambulisha Kibiki, kama kiongozi wa kuigwa kutokana na tabia yake ya ucheshi na kujichanganya na watu.akizungumza wakati wa kukabidhi WIMBO huo msanii  ‘One Lee’ alisema kuwa FRANK KIBIKI amekuwa akiwapa elimu vijana juu ya kujitambua na kuwasaidia jinsi gani ya kujiajili wao wenyewe na kuonyesha njia ya kutokea kimaisha na dio imekuwa sababu ya wasanii wa mkoani hapa kutunga wimbo huo. 
“Wimbo unaitwa ‘Kuwa mfano wa kuigwa’, tumempa kaka yetu kama zawadi, ili wengine waige mfano wake.

SEMINA YA USAMBAZAJI WA MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAAZI YA MWAKA 2012 KWA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI YA FANYIKA ZANZIBAR.

Dr. Shein azindua sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa CCM

RAIS KIKWETE AWASI|LI RIYADH KUHANI KIFO CHA MFALME WA SAUDI ARABIA, KUFANYA ZIARA YA KIKAZI UJERUMANI NA UFARANSA

unnamed1jkRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wan Kijeshi mjini Riyadh,
Saudi Arabia,  asubuhi ya Jumapili, Januari 25, kuhani kifo cha
Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita. Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah,Rais Kikwete ataendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.
PICHA NA IKULU unnamedjkRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili mjini Riyadh, Saudi Arabia,asubuhi ya leo, Jumapili, Januari 25, 2015, kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita.
Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah, Rais Kikwete ataendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.

ROBO FAINALI KOMBE LA TAIFA WANAWAKE KUANZA KESHO

miguuHatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Taifa kwa Wanawake inachezwa kesho (Januari 26 mwaka huu) na Januari 27 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam kwa mechi mbili kila siku.
Mechi ya kwanza ya robo fainali ya michuano hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Televisheni itaanza saa 9 alasiri kwa kuzikutanisha Mwanza na Kigoma. Robo fainali ya pili ambayo ni kati ya Tanga na Pwani itaanza saa 11 kamili jioni.
Ilala na Iringa watacheza robo fainali ya tatu Januari 27 mwaka huu kuanzia saa 9 kamili alasiri, na kufuatiwa na robo fainali ya mwisho saa 11 kamili jioni itakayozikutanisha Temeke na Mbeya.
Nusu fainali za michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Proin zitachezwa Januari 29 mwaka huu wakati Fainali itachezwa Februari Mosi mwaka huu kuanzia saa 10.15 jioni ambapo itatanguliwa na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu (play off).
Timu zote zilizoingia hatua hiyo ya nane bora ya michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini zimefikia hosteli ya Msimbazi.
Wakati huo huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litakuwa na mkutano na waandishi wa habari. Mkutano huo utafanyika kesho (Januari 26 mwaka huu) saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.

RAIS DR. SHEIN AWASILI PEMBA TAYARI KWA UZINDUZI WA SHEREHE ZA MIAKA 38 YA CCM

1Rais wa Zanzibara na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Mh. Dr. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Pemba kwa ajili ya uzinduzi wa sherehe za miaka 38 ya CCM utakaofanyika leo kwenye uwanja wa Gombani mijni Chakechake Pemba ambapo Rais Dr. Shein  atakuwa mgeni rasmi, Sherehe za Kilele cha miaka 38 ya CCM kitaifa zinatarajiwa kufanyika Songea mkoani Ruvuma Februari 1 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Dr. Jakaya Kikwete. 2Rais wa Zanzibara na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Mh. Dr. Ali Mohamed Shein akisalimiana wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Chakechake Pemba. 

Airtel yazindua huduma ya kufanya malipo kwa kutumia kadi

11
Mfanyabiashara na mmiliki wa duka la dawa katika eneo la Mrombo Arusha Bi elizabeth mshana akiongea na Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde juu ya huduma ya kufanya malipo kwa kutumia kadi ya Airtel Money Near Field Communication (NFC) based solution ya  Airtel Money. kadi hii maalum inamuwezesha mteja kufanya malipo kwa haraka kwa kugusisha kwenye kifaa maalum tu mara moja, kisha kuweka nambari ya siri na kufanya malipo mahali popote. kwa sasa huduma hii imeanza kufanya kazi mkoani Arusha. Huduma hii ya Near Field Communication (NFC) yaani kulipa kwa kugusisha kadi na kifaa tu kupitia huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni ya simu za mkoni ya airtel
1111
Mama elizabeth mshana mmiliki wa duka la dawa akimuuzia mteja dawa kwa kupitia kadi huduma iliyozinduliwa na Airtel mkoani Arusha inayowawezesha wateja wake kufanya malipo kwa haraka zaidi kwa kutumia kadi hiyo maalumu ya airtel Money yenye teknolojia ya Near Field Communication (NFC) based ikiwa imeunganishwa na  Airtel Money.akishuhudia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde. Huduma hii ya Near Field Communication (NFC) kupitia huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni yasimu za mkoni ya airtel.

NYALANDU KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO ZA UTALII NCHINI


Lazaro-Nyalandu1

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu,
……………………………………………………… NA MWANDISHI WETU WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu,ameendelea na jitihada za kutafuta ufumbuzi wa kudumu kuhusiana na changamoto zinazowakumba wadau wa biashara ya utalii nchini. Katika kuhakikisha hilo linafanyika kwa mafanikio na kwa haraka, Nyalandu ametangaza kuanza kwa vikao vitakavyowakutanisha wataalamu wa Wizara zinazohusika na maliasili na utalii za Tanzania na Kenya kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali iili yapatiwe ufumbuzi kwa maslahi ya pande zote. Hatua hiyo imetokana na hivi karibuni Serikali ya Kenya kuyazuia magari ya utalii kutoka Tanzania kuingiza watalii kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, hivyo kusababisha usumbufu mkubwa. Hata hivyo, Nyalandu aliingilia kati kwa kuzungumza na Waziri wa Utalii wa Kenya, Phillys Kandie na kufikiwa kwa makubaliano ya kuruhusiwa na hapo wazo wa wizara hizo kukutana likaibuliwa. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Nyalandu alisema vikao ya wataalamu hao vitaanza rasmi Februari 3, mwaka huu, jijini Arusha ambapo vitahusisha pia wataalamu kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Alisema vikao hivyo vitajadili masuala mbalimbali ili kuhakikisha changamoto zote zinawaikabili sekta ya utalii kwa nchi hizo mbili zinapatiwa ufumbuzi. Aliongeza kuwa hatua hiyo pia inalenga kuimarisha ushirikiano pamoja na kuongeza ulinzi kwenye mbuga za wanyama na mapori ya akiba dhidi ya mtandao wa ujangili. Hata hivyo, aliweka wazi kuwa hoja kuhusiana na mpaka wa Borongoja haitajadiliwa kwenye vikao hivyo kwa kuwa si sehemu ya ajenda. “Nchi zetu hizi zinategemeana sana katika biashara ya utalii hivyo, kuna makubaliano tuliyafikia muda mrefu huko nyuma lakini yanaonekana kuanza kuwa na changamoto hivyo ni lazima tujadili ili tuweze kusonga mbele. Hatutaki watalii wanaokuja kupumzika wasumbuke kwani itakuwa ni hasara kwa wafanyabiashara wetu na kutahatarisha uchumi wa taifa…daima lazima tusonge mbele,” alisema Nyalandu. Aliongeza kuwa baada ya mkutano wa wataalamu utafuatiwa na wa makatibu wakuu wa wizara hizo utakaofanyika Februari 4 mwaka huu kisha utahitimishwa na wa mawaziri utakaofanyika Februari 5. Nyalandu alisema ana imani mikutano hiyo itatoka na mwanga mpya na maboresho kwa sekta ya utalii na kusisitiza maslahi ya pande zote yatazingatiwa. Alisema kuwa nia ya Tanzania ni kuendeleza Jumuia ya Afrika Mashariki na mahusiano yake mazuri na si kugombana na kuharibu uhusiano huo. Alisema daima Tanzania itakuwa makini kuhakikisha mahusiano yanakaa sawa katika majadiliano hayo na kwamba kusije kutokea jambo likaleta madhara kwa watu wengine. Nyalandu aliongeza Tanzania itafanya biashara za utalii na watu wengine kuhakikisha wanaendelea kulinda rasilimali za taifa sambamba na wafanyabiashara wakubwa wa kitalii na wadogo.

MSIMU WA PILI WA DARASA LA KISWAHILI WAANZA RASMI DMV

Wazazi, mwalimu na viongozi wa jumuiya waliohudhuria siku ya kwanza ya darasa la Kiswahili DMV wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kuanza kwa Awamu ya pili ya Darasa la Kiswahili kwa watoto waishio Washington DC  Januari 24, 2015. pia Rais wa Jumuiya Bw Iddi Sandaly alipata fursa ya kuzungumza na Wazazi na watoto hao kuhusu darasa hilo.
 
Wanafunzi wakimsikiliza Mwalimu Asha Nyang’anyi. Kushoto kwake ni Katibu wa Jumuiya ya waTanzania DMV

Rais Kikwete aapisha mawaziri wapya ikulu

 IKU1Moja wa Sura mpya katika baraza jipya la Mawaziri Naibu Waziri wa Elimu Anne Kilanngo Malecela akila kiapo Mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete ikulu jijini Dar es Salaam ,(PICHA NA FREDDY MARO)
IKURais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mawaziri na manaibu waziri aliowaapisha ikulu jijini Dar es Salaam jioni hii.Wanne kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA ASHIRIKI KUPANDA ZAO LA MWANI BAHARINI

1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa jimbo la  Muyuni Mh. Mahadhi Juma Mahadhi wakati alipowasili katika tawi la Pete ambapo amezungumza na wajumbe wa halmashauri ya wilaya ya Kusini akisisitiza zaidi masuala ya kushughulikia matatizo ya wananchi na kuwa waadilifu ili wananchi wawaamini katika majukumu yao jambo ambalo litakifanya Chama cha Mapinduzi kuaminika zaidi na wananchi kwani chama hicho ni kikubwa na kina historia kubwa kwa upande wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,ambapo pia Katibu mkuu huyo  anahamasisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya  mwaka 2010 ,  Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Kinana anaongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Katikati ni Mwakilishi wa jimbo la Muyuni Mh. Jaku Hashim. 2Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana Samia Suluhu Mbunge wa jimbo la Makunduchi mara baada ya kuwasili katika tawi la Pete Makunduchi, katikati ni Mwakilishi wa jimbo la Makunduchi Haroun Ali Suleiman. 3Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mh. Wanu Hafidh Ameir Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Mwakilishi nafasi za vijana

JINSI JAMBAZI ALIVYOPIGWA RISASI ZANZIBAR JUZI MTAA WA DARAJANI

unnamedJAMBAZI SUGU MAARUFU KHAMIS MABUNDUKI  LIKIWA KATIKA GARI LA POLISI MTAA WA DARAJANI MJINI ZANZIBAR BAADA YA KUPATA KICHAPO KIKALI  ALIPOFANYA UJAMBAZI  KUTAKA KUIBA AKIWA NA WENZAKE WAWILI HATIMAYE MMOJA WAO KUKIMBIA.

Wajumbe wa Baraza la Michezo la Taifa watakiwa kujenga utamaduni wa kutekeleza wajibu wao kwa kujitolea zaidi.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) mara baada ya kuzindua Balaza la 13 la Michezo mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.Waliokaa kutoka kushoto ni Katibu wa Baraza la Michezo Zanzibar, Naibu Kaibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel, Mwenyekiti wa BMT Bw. Dioniz Malinzi na mjumbe wa BMT Mhe. Zainab Vulu (MB).
Picha zote na Frank Shija, WHVUM.
unnamed2Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (MB) akitoa nasaha kwa wajumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wakati akizindua Balaza la 13 la Michezo leo jijini Dar es Salaam.Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel na wa mwisho kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo. Wajumbe waliohudhuria hafla hizo ni pamoja na ,Mkurugenzi wa PSPF Adam Mayingu, Zacharia Hans Pope, Jamal Rwambow, Mkurugenzi wa Operesheni wa NSSF Crescentius Magori ,wajumbe wengine ni Alex Mgongolwa, Jennifer Mmasi Shang’a, Mhe. Zainabu Vulu (MB), Mohamed Bawaziri na Mwl. Zaynab Mbiro.

RAIS KIKWETE ATANGAZA MABADILIKO MADOGO YA BARAZA LA MAWAZIRI JIONI HII

WAZIRI LEO0
Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akizungumza na vyombo vya habari jioni hii wakati akitangaza mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri,Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Mwishoni mwa juma ametangaza mabadiliko madogo katika Baraza lake la Mawaziri,ambalo Aliliapisha siku hiyo  Ikulu,Jijini Dar es Salaam.
Akitangaza uteuzi huo muda mchache kabla ya Mawaziri hao kuapishwa, Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue alisema uteuzi huo ulihusu pia kujaza nafasi mbili zilizoachwa wazi na Profesa Anna Tibaijuka Na Profesa Sospeter Muhongo.
Profesa Tibaijuka, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alieachishwa kazi kutokana na kuhusika kwake katika sakata la akaunyti ya Tegeta Escrow.
Kwa upande wa Profesa Muhongo aliachia ngazi mwenyewe mapema siku ya ijumaa ,  kwa kile alichotaja kuipisha Serikali iendelee kuwatumikia Wananchi badala ya kuendelea na malumbano ya Escrow.
Katika mabadiliko hayo,sura mpya za manaibu mawaziri zimeingia na baadhi ya mawaziri wamehamishwa wizara.
Akitangaza Mabadiliko hayo,Balozi Sefue aliwataja mawaziri hao kama ifuatavyo.
MAWAZIRI
1. Mh. George Simbachawene – Waziri wa Nishati na Madini
2. Mh. Mary Nagu – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mahusiano na Uratibu)
3.Mh. Christopher Chiza – Waziri Uwezeshaji na Uwekezaji
4. Mh. Harrison Mwakyembe – Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
5.Mh. William Lukuvi – Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi
6.Mh. Steven Wasira – Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika
7.Mh. Samwel Sitta -Waziri wa Uchukuzi
8.Mh. Jenista Muhagama – Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge
MANAIBU WAZIRI
1. Stephen Masele – Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu Rais – Muungano
2. Mh. Angela Kairuki –  Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi
3. Mh. Ummy Mwalimu – Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
4. Mh. Anna Kilango – Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
5 . Mh. Charles Mwijage – Naibu Waziri wa Nishati na Madini

PROFESA SOSPETER MUHONGO WAKATI WA KUBWAGA MANYANGA

DSCF1880
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na waandishi wa katika mkutano uliofanyika mchana huu kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za Wizara hiyo,zilizopo kwenye Mtaa wa Samora,Jijini Dar es salaam.
Waziri Muhongo ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo,kufuatia shinikizo la muda mrefu la kumtaka afanye hivyo au awajibishwe, kufuatia mapendekezo ya Bunge lililopita, lililoagiza serikali kuchukua hatua dhidi yake na wengine kadhaa kufuatia kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow. Kwa hisani ya http://issamichuzi.blogspot.com/ DSCF1860Waziri Muhongo akikazia kujiuzulu kwake huko amesema kuwa yeye sio mla rushwa bali ni mchapa kazi tu na akilizungumzia swala la akaunti ya Tegeta Escrow ambalo ndilo lililopelekea kujiuzulu kwake huko,Waziri Muhongo amesema kuwa sakata hilo lilitawaliwa na mambo makuu manne ambayo aliyataja kuwa ni Mvutano wa kibiashara, Mvutano wa kisiasa, Mvutano wa uongozi na madaraka pamoja na Ubinafsi.
Hivyo kasema ameamua kujiuzulu ili kuiachia Serikali na Bunge kusitisha malumbano ya sakata la Escrow, akidai inaonekana yeye ndiyo tatizo.Picha/habari na Othman Michuzi. DSCF1873Sehemu ya Waandishi wa kutoka vyombo mbali mbali vya habari wakifatilia kwa makini taarifa ya Waziri Muhongo.

Taarifa kwa Vyombo vya Habari kutoka Jeshi la Wananchi (JWTZ)

index
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa taarifa kwa wananchi na Vyombo vya Habari kuhusu mgogoro wa eneo la TONDORONI lililopo katika Wilaya ya Kisarawe kama ilivyokaririwa na baadhi ya Vyombo vya Habari hapa nchini.
 
Taarifa zilizotolewa na kukaririwa na baadhi ya Vyombo vya Habari kwamba Wanajeshi wametumia nguvu kuwatoa wananchi eneo la TONDORONI na baadhi yao kudai kupotelewa na mali zao siyo za kweli na ni za kuwapotosha wananchi kwa sababu wananchi hao walitaarifiwa kuondoka kupitia uongozi wa Wilaya na uongozi wa Vijiji vya MLOGANZILA na KILUVYA B. Aidha, walipewa muda wa kutoa vitu vyao na wao kuondoka.
 
 JWTZ linapenda kuwahakikishia wananchi kuwa hatua ya kuwaondoa wananchi wavamizi kutoka katika eneo la kambi ya Jeshi kwa uangalifu, umakini na kulikuwa na usimamizi wa hali ya juu na hakuna mali ya mwananchi iliyoporwa kama ilivyodaiwa. Ifahamike kwamba; Jeshi linaona ni bora lilaumiwe kwa kuwaondoa wananchi waliovamia  maeneo hatarishi  ya jeshi ambayo hutumika katika mafunzo yanayohusisha risasi za moto,  zana hatari za kijeshi  na mabomu ambayo wakati mwingine hulipuka baada ya muda fulani kupita badala ya kuwaacha wakae katika maeneo hayo  kutokana na sababu za kisiasa au ushabiki mwingineo na hivyo kuwa katika hatari ya kuweza kuumia vibaya au kupoteza maisha yao na mali zao.
Pia ni vema tukajua historia ya tatizo hili.
Mnamo mwaka 1978 eneo linalojumuisha vijiji vya MLOGANZILA na KILUVYA B na kilichokuwa kijiji cha TONDORONI lilichukuliwa na Serikali kwa ajili ya matumizi ya JWTZ.  Baada ya maamuzi hayo Kikosi cha JWTZ kilihamia TONDORONI mwaka 1981na kukalia eneo la hekta 4197.  Serikali ililipima eneo la TONDORONI kisheria mwaka 1984 na eneo lote liliwekewa mawe ya mipaka.
 
Baada ya hapo, Serikali ilifanya tathimini ya malipo  kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ilikuwa mwaka 1987/88 na wakati huo kulikuwa na wananchi wapatao 1,508.  Awamu ya pili ilifanyika 1992/93 ambayo ilijumuisha tathmini ya nyumba na majengo ambapo wananchi wengine 955 walifanyiwa tathimini.
 
Kufuatia tathimini iliyofanyika malipo yalikuwa kama ifuatavyo:
 Mwaka 1996 malipo yalifanyika kwa barua kumbukumbu         Na. FE 98/371/01/73 ya tarehe 11 Juni 2003.
 Malipo mengine yalifanyika mwaka 2002 na 2006. Baada ya Malipo hayo, mengine tena yalifanyika mwaka 2012 kutokana na kesi ya madai Na. 144/1996.  Kwa hiyo madai ya msingi ya wananchi yalishalipwa na sheria ya uchukuaji ardhi imetekelezwa kikamilifu.
 
Hata hivyo, mwaka 2005 baadhi ya wananchi wachache walifungua kesi Na. 78/2005 ambayo baadae ilifutwa na mahakama.  Tarehe 10 Dec 2013 M/kiti wa kamati ya Ulinzi ya Wilaya Kisarawe alikwenda eneo la TONDORONI kuwasomea wananchi maamuzi ya mahakama akiandamana na mwanasheria wa Wilaya ya Kisarawe.
 
Pamoja na taarifa hizo kupitia uongozi wa Wilaya na uongozi wa Vijiji vya MLOGANZILA na KILUVYA B. wananchi wachache  wameendelea na kazi zinazochangia kuharibu mazingira hasa ukataji wa miti, uchomaji wa mkaa na kuwasha moto mara kwa mara hali inayotishia usalama wa kambi na wa wananchi wenyewe ikizingatiwa kwamba hili ni eneo la mafunzo ambapo risasi za moto hutumika sambamba na zana zingine  hatari za kijeshi katika eneo hilo.
Wananchi waliowengi wanajua ukweli kuwa eneo la TONDORONI linamilikiwa kihalali na JWTZ, lakini wapo wananchi wachache wamekuwa wakiingia kinyemela katika eneo hilo na kufanya ujenzi mpya usiku licha ya jitihada mbalimbali zinazofanyika kuwaelimisha na kuwashauri kuwa waache tabia hiyo ya kulivamia eneo hilo la Jeshi, jambo ambalo hugunduliwa na kuzuiliwa uendelezaji wa ujenzi huo.
 
Jeshi linawataka wananchi wachache wanaovamia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya matumizi ya kijeshi; kutambua kuwa kufanya hivyo ni kosa la kisheria lakini pia kwa mara nyingine tena kuendelea kuwakumbusha wananchi kuhusu madhara yanayoweza kuwapata wananchi wanaovamia maeneo ya Jeshi na kujenga katika maeneo hayo.
Jeshi litaendelea kushirikiana na wananchi wema na kuheshimu mipaka iliyopo baina ya makambi yake na maeneo ya wananchi lakini pia  litaendelea kuwaondoa wale wachache wanaojenga katika maeneo yake kinyume cha utaratibu. 
 
 Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga