TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, August 4, 2014

Benki ya NBC yatoa mkopo wa mabilioni kwa Mohamed Enterprises

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (wa tatu kushoto) akisaini hati za makubaliano ya mkopo wa shs bilioni 100 na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Mohamed Enterprises Ltd (METL), Mohamed Dewji kwa ajili ya kampuni dada ya METL ya Star Oils inayoshughulika na biashara ya uagizaji na usambazaji mafuta. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni baadhi ya watendaji wakuu wa NBC, METL na Star Oils.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa METL, Mohamed Dewji wakionyesha mikataba muda mfupi baada ya kusaini  hati za makubaliano ya mkopo wa shs bilioni 100  kwa ajili ya kampuni dada ya METL ya Star Oils inayoshughulika na biashara ya uagizaji na usambazaji mafuta. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa METL, Mohamed Dewji (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya maofisa wa benki ya NBC katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bi Mizinga Melu akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya kuipatia kampuni ya Star  Oils mkopo wa takribani sh bilioni 100 ili kuAongeza ufanisi katika kampuni hiyo ya uagizaji na usambazaji wa mafuta nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (wa nne kushoto), Ofisa Mtendaji Mkuu wa METL, Mohamed Dewji (wa nne kulia), watendaji wakuu wa NBC, METL na Star Oils wakipozi kwa picha ya kumbukumbu mara baada ya utiaji saini makubaliano hayo.

No comments:

Post a Comment