TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, August 7, 2014

kutana na maajabu ya Dunia- yasadikiwa ni kitu kutoka mbinguni.

Kwa mujibu wa chapisho la jumanne tarehe 5, katika mtandao wa The Express wa nchini Uingereza, picha hiyo ya ajabu inaonesha wingu kubwa lenye “shepu ya mkono” ukitokeza katika wingu huko Kent, nchini Uingereza jumatatu iliyopita.

Mpigapicha huyo mwenye umri wa miaka 38 na baba wa watoto wawili, alikuwa nyumbani kwake na mkewe Jodie (37), alipoona wingu likijikusanya kwa sura ya chujio.
Baba huyo hakuamini macho yake na kudai kuwa hajawahi kuona kitu kama hicho maishani mwake. “Ilionekana kweli kama Mkono wa Mungu. Ulionekana kama mkono mkubwa unachomoza kutoka mawinguni, ilikuwa ni ajabu” Alisema David.

“Nilitamani sana kwenda kupiga picha za kimbunga nchini Marekani ambapo kuna mambo mengi ya ajabu, lakini hili ni la ajabu zaidi, nafurahi sana kuweza kupata picha ya tukio zima katika video” aliongeza Christie.
Hii sio mara ya kwanza kwa tukio la ishara ya kidini kutokea mawinguni, wiki iliyopita mpigapicha mwingine jua huko Norfolk alifanikiwa kupata picha ya wingu lenye sura yenye ndevu kutokea mawinguni.

No comments:

Post a Comment