TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, August 5, 2014

YANGA YATEMEWA CHECHE CHA (Cecafa)

Kocha Mkuu, Marcio Maximo.
By KHATIMU NAHEKA 
  • Awali Yanga ilipanga kupeleka kikosi cha mastaa wao, lakini baadaye Kocha Mkuu, Marcio Maximo, akabadili mawazo na kusema vijana waende na yeye atakwenda Pemba na kikosi cha kwanza kukisuka zaidi.
BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) limepokea majina 20 ya Yanga na kuyaangalia mara mbili na kisha kuyaweka pembeni na kuwaambia viongozi wa Jangwani pamoja na Shirikisho la Soka la Tanzania(TFF): “Msitutanie hili siyo bonanza”
Awali Yanga ilipanga kupeleka kikosi cha mastaa wao, lakini baadaye Kocha Mkuu, Marcio Maximo, akabadili mawazo na kusema vijana waende na yeye atakwenda Pemba na kikosi cha kwanza kukisuka zaidi.
Katika orodha ya wachezaji 20 wamo wa kikosi cha pili ambao ni Ally Mustapha ‘Barthez’, Nizar Khalfan, Rajab Zahir, Hussein Javu, Said Bahanuzi, Omega Seme, Oscar Joshua. Kutoka kikosi cha vijana wamewachukua Said Ally, Kulwa Baumba, Patrick Ngoyani, Joseph Sadick, Amos Abel, Mwinyi Ndimbo, Henry Michael, Shaban Idd, Hamis Issa, Juma Kayanda, Frank Shineiba na Frank Gerald.
Mwanaspoti linajua kwamba Cecafa pamoja na waratibu wa michuano hiyo ambayo ni Shirikisho la Soka la Rwanda(Ferwafa), ilizungumza na kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima (hayupo kwenye orodha) na akawahakikishia kwamba kikosi kilichotumwa ni wachezaji wa benchi na vijana wakali wote wamewekwa kando akiwamo yeye.
Cecafa ikarudisha majina hayo kwa Yanga na TFF na kisha kuwapa mpaka usiku wa kuamkia leo Jumanne  wabadilishe, lakini Yanga wakakomaa na hadi tunakwenda mitamboni kulikuwa na mzozo mkubwa huku Yanga ikisisitiza kwamba uamuzi wake ni sahihi kwani wachezaji hao ni wa Yanga kikanuni.
Hivyo Cecafa ikaamua  kupiga simu Azam na kuwaambia wakae tayari kuchukua nafasi ya Yanga kama klabu hiyo itasimamia msimamo wake.
Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholaus Musonye, alisema wamekigomea kikosi cha Yanga kwa vile ni dhaifu  kisichoendana na hadhi ya mashindano.
Musonye alisema waliitaka Yanga kubadilisha haraka kikosi chao ikiwa ni pamoja kuwaingiza wachezaji wao wenye majina makubwa wakiwemo kipa Juma Kaseja, Mbuyu Twite na wachezaji wao wawili wapya Genilson Santos ‘Jaja’ na Andrey Coutinho pamoja na kocha wao Maximo na kama hilo lingeshindikana mpaka usiku watawapiga chini na kuipa Azam nafasi.
Yanga inapaswa kushiriki kwa vile ndio ilikuwa bingwa wa Bara msimu uliotangulia kabla ya uliopita.
“Unajua hii kwa Yanga inakuwa kama tabia yao kuwa na visingizio vingi,  kwanza walikuwa na kiburi cha kuchelewa kuthibitisha kushiriki, lakini sasa wametuma watoto, leo ikikubaliwa kwa Yanga kesho itafanywa na timu nyingine hatutaki kuruhusu hilo,” alisema Musonye.
“Ukiacha hao wachezaji wanaosema wapo katika timu ya taifa ambao hawazidi wanane, kuna wachezaji wengi wapo hapo Dar es Salaam wakifanya mazoezi mfano ni Kaseja (Juma) hao Wabrazili kijana wao Twite (Mbuyu), lakini angalia hata kocha Maximo naye haji, hiyo ni dharau,” alisisitiza Musonye ingawa Katibu Mkuu wa Yanga, Benno Njovu alikuwa akidai kwamba hawana taarifa na walikuwa wanasubiri tiketi tu.
Msemaji wa Ferwafa, Bonny Mugabe alisema: “Yanga wameonyesha dharau kubwa kwa Cecafa, haya mashindano Rais Paul Kagame amewekeza hela nyingi sana hatuwezi kukubali kuletewa timu ya majaribio. Walichofanya Yanga ni dharau na hakivumiliki.

No comments:

Post a Comment