TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, August 7, 2014

HUDUMA MPYA YA BWERERE YAZINDULIWA KUTOKA TTCL

 Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo TTCL,Bwa.Peter Ngota akionesha kipeperushi chenye taarifa mbalimbali kuhusiana na huduma yao mpya iliyojulikana kwa jina la Bwerere,Kwa waandishi wa habari,huduma hiyo imezinduliwa leo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar. 
 Baadhi ya Wandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa huduma mpya ya TTCL iliyojulikana kwa jina la Bwerere ,kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar. 
Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo TTCL, Bwa.Peter Ngota akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa mkutano wa uzinduzi wa huduma yao mpya iliyojulikana kwa jina la Bwerere,kwenye moja ya ukumbi wa mikutano ndani ya Ofisi za kampuni hiyo,zilizopo makao makuu mtaa wa Samora Jijini Dar.
=======  ======= =======
Bwa.Peter alisema kuwa siku ya leo ,TTCL inazindua rasmi promosheni inayolenga kuwapa wananchi huduma bora na za bei nafuu. Promotion hii inajulikana kwa jina la  BWERERE   yaani pata huduma nyingi zaidi kwa bei nafuu zaidi.

''Promosheni hii inatoa fursa kwa wateja wa majumbani na maofisini ambao wanatumia  huduma ya malipo ya kabla(pre-paid) kufurahia gharama ya viwango vya chini kabisa vya kupiga simu TTCL kwenda kwenda mitandao mingine yote ikiwa ni pamoja na TTCL yenyewe,

Vilevile Promosheni hii inatoa fursa maalumu kwa watumiaji wa vifurushi vya intaneti(DATA)  kwa njia ya Broadband mtandao wa Nyaya na Mkongo waTTCL kitaalamu Fixed lines kuweza kupata intaneti bila kikomo''.Alisema Bwa.Peter Ngota.

No comments:

Post a Comment