TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, March 9, 2016

AY akutana na TCRA kujadili kufungiwa kwa "Zigo remix" WAFANYAKAZI 597 WA NIDA WASIMAMISHWA KAZI International Women¹s Day Celebrations Champion a Planet 50-50 by 2030 HAPPY BIRTHDAY SERIKALI YAWAPONGEZA WASANII RICH RICH NA LULU KWA USHINDI WA AMVCA2016 RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MWAKILISHI WA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUHUDUMIA WAKIMBIZI UNHCR ANAYEMALIZA MUDA WAKE BI. JOYCE MENDS-COLE IKULU JIJINI DAR LEO WAZIRI MKUU MAJALIWA AMPA POLE RAIS MSTAAFU. KATIBU MKUU KIONGOZI MPYA AKARIBISHWA RASMI, ATEMBEZWA MAENEO MBALIMBALI IKULU LEO Madaktari 3, wauguzi 6 watumbuliwa Mwanza IBADA YA PAMOJA YA PASAKA DMV Benki ya NMB yatoa milioni 25 kwa Timu ya Taifa Mpira wa Magongo Taasisi ya Gihon Needy Comfort Organization (GINCO), yaendesha semina kwa Wanawake Wajasiriamali Yanga, Azam zaipaisha Simba Mabalozi wa Tanzania wakwama ughaibuni. RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AMUAPISHA MHE. BALOZI ENG. JOHN WILLIAM KIJAZI KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI Kichupa cha leo Nay Wa Mitego - Shika Adabu Yako [Official Music Video] BABA WA KAMBO- WIMBO ULIOMPA WAKATI MGUMU KAMANDA RAS MAKUNJA MTANGAZAJI WA SIKU NYINGI EMMANUEL JENKINS MUGANDA KUWEPO KWENYE KIPINDI CHA JUKWAA LANGU KINACHORUSHWA LIVE KILA SIKU YA JUMATATU USIKOSE AUDIO: JANUARY NA MWAMVITA MAKAMBA WAMJIBU MUITALIANO ALIYEWAPA TUHUMA NZITO WANATABORA WAISHIO DAR WAPATA MWENYEKITI NAIBU WAZIRI MASAUNI AFANYA MAZUNGUMZO NA KAIMU BALOZI WA MAREKANI NCHINI Shilole ndani ya BSS studioz Spika wa Bunge la EALA aziasa nchi wanachama kutumia Kiswahili katika kufanya kazi ndani ya Jumuiya. WASIFU WA KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI MHANDISI JOHN WILLIAM KIJAZI HUU HAPA

 AY akutana na TCRA kujadili kufungiwa kwa "Zigo remix"


PRESS RELEASE
For Immediate Release
07 March 2016

Media Inquiries

Oisika Chakrabarti, +1 646 781-4522, oisika.chakrabarti[at]unwomen.org
Sharon Grobeisen, +1 646 781-4753, sharon.grobeisen[at]unwomen.org
Zina Alam, +1 646 781-4783, zina.alam[at]unwomen.org

Español | Français
International Women’s Day Celebrations Champion a Planet 50-50 by 2030
Acclaimed soprano Renée Fleming to perform; momentum for Stepping It Up for Gender Equality rises

(New York, 7 March) International Women’s Day celebrations on 8 March will mobilize people around the world to call for a Planet 50-50 by 2030. UN Women is organizing a series of diverse, high-profile events in over 40 countries, where ordinary citizens, activists, musicians, athletes, students, security personnel, scholars and stock exchange officials will be among those who commit to “Stepping It Up for Gender Equality.”

At the United Nations Headquarters in New York, prominent speakers from governments, the United Nations, businesses and civil society, including youth groups, will convene to debate how to advance women’s empowerment and overcome barriers to change. UN Women Executive Director Phumzile Mlambo-Ngcuka and Pamela Falk of CBS News will moderate the session. Celebrated soprano Renée Fleming, one of the most acclaimed singers of our times, will perform at the high-powered event, along with young artist Tennille Amor and Broadway singers.

Key to the discussion will be the essential role of gender equality in attaining the recently agreed Sustainable Development Goals, a blueprint for global development endorsed by all UN Member States. The event will further highlight the importance of equal representation of women at all levels of the UN system, and the integration of gender issues in all aspects of the UN’s work.

“Women and girls are critical to finding sustainable solutions to the challenges of poverty, inequality and the recovery of the communities hardest-hit by conflicts, disasters and displacements. They are at the frontline of the outbreaks of threatening new epidemics, such as Zika virus disease or the impact of climate change,” said UN Women Executive Director Phumzile Mlambo-Ngcuka in her message for the Day. “The participation of women at all levels—and the strengthening of the women’s movement—has never been so critical, working together with boys and men, to empower nations, build stronger economies and healthier societies. It is the key to making Agenda 2030 transformational and inclusive,” she added.

Early in the day, film stars and UN and New York City officials will kick-off the inaugural HeForShe Arts Week, a new initiative by UN Women to leverage the arts for gender equality. UN Women Goodwill Ambassador Emma Watson, SDG Advocate and UNESCO Goodwill Ambassador Forest Whitaker, First Lady of New York City Chirlane McCray, UN Women Executive Director Phumzile Mlambo-Ngcuka, The Public Theater’s Artistic Director Oskar Eustis and others will take part in the launch. The HeforShe Arts Week will run from 8-15 March 2016, during which time over 30 partners throughout the city of New York—ballets, operas, Broadway shows, music concerts, theatres, cinemas, galleries and museums—will highlight gender equality and women’s rights, and donate a percentage of proceeds to UN Women.

UN Women Regional Ambassador and actor-director-singer from India Farhan Akhtar will release his powerful song “We all are on the Goodside” on 8 March. The song, produced by his organization Men Against Rape and Discrimination (MARD), advocates for women’s empowerment and celebrates an equal world for all.

Around the world to mark International Women’s Day, 35 stock exchanges will ring their opening or closing bells to raise awareness. In Santiago, 800 private sector and government leaders will gather to show support. The Dhaka exchange will highlight the low share of women in board positions among listed companies and announce a survey to inform steps to boost participation. A half-day session at the Nairobi exchange will profile best practices by companies to empower women, while speakers in Amman will stress how gender diversity improves corporate performance.

Based on a partnership agreement signed on the occasion of the day, in Nigeria, UN Women will join MasterCard, the National Identity Management Commission and civil society organizations to kick off a new programme that aims to ensure at least 500,000 women obtain national identity cards that enable access to financial services, including electronic payments—a foundation for economic empowerment.

The Sorgente Group of America, a real estate company that specializes in historic and sustainable buildings, will highlight the message of “Planet 50-50: Step It Up for Gender Equality” on its iconic Flatiron building, to mark International Women’s Day on8 March.

In association with UN Women, Snapchat, the popular mobile story-telling app, will feature remarkable women from all walks of life in a format called ‘Live Story’, which will be shared with Snapchatters on 8 March. Users who watch the story in their app will have the chance to contribute their own Snaps, telling their stories and honouring the remarkable women in their lives.

Commemorating International Women’s Day in New York and New Delhi, the United Nations Postal Administration and India Post will jointly issue stamps, designed by Mirko Illic, which illustrate gender equality by showing half a face—either male or female. The message: men and women have to work together to make gender equality a reality. The initiative is part of UN Women’s HeForShe global solidarity movement to engage men and boys as agents of change for women’s rights and gender equality.

In every region of the world, people will organize marches, competitions, performances and other events. Thousands will run, walk, march or cycle to demonstrate their commitment to a gender-equal world, such as through cycle rallies in India and the Maldives. Women’s and men’s hockey teams will square off in a match in Tanzania.

The arts will feature prominently, with Haiti hosting a concert and photo exhibit, the State of Palestine a series of performances, and Albania a photo competition. Film festivals will take place in Barbados, Cambodia, the former Yugoslav Republic of Macedonia, Georgia, Jordan and Moldova. In Jordan, HeForShe volunteers will unveil an art collage.

A public gathering in Mali will give awards to women pioneers and emerging leaders. Pakistan will launch an award ceremony for women’s rights activists, the first in an annual series. In Brazil, women will run to “Step It Up” for the HeForShe campaign, and a special ceremony will recognize companies with best practices in terms of gender equality and women’s empowerment.

Viet Nam plans a university event on gender stereotypes, and Thailand a series of feminist dialogues. In Bosnia and Herzegovina, a competition for journalists will be initiated, encouraging them to focus attention on gender equality issues.

In the lead-up to International Women’s Day, on 7 March, a new series of orange dresses, scarves and ties will be launched at the National Portrait Gallery in London. The vibrant colour signifies hope and positive momentum in the global movement to end violence against women; proceeds from sales will benefit the UN Trust Fund to End Violence against Women (UN Trust Fund). Fashion designers Daniella Helayel and Ozwald Boateng created the items through a partnership with LDNY. Models and celebrities such as Lily Donaldson, Olivia Grant, Jodie Kidd and Caroline Weinberg will attend the launch, followed by a pop-up store at Goldman Sachs in London.

Also on 8 March, during an event on the role of ethical fashion in preventing violence against women and girls, at the London boutique Celestine Eleven, VOZ (meaning ‘voice’) will unveil a Manta (blanket) to benefit the UN Trust Fund. The Manta was designed and produced by rural women artisans in Chile, providing employment and training.
Imeandaliwa na Andrew Chale,Modewjiblog/Mo tv Online
Katibu wa Bodi ya filamu ya ukaguzi na Michezo ya kuigiza, Bi. Joyce Fisso akiwatambulisha wasanii kwa Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye (kulia) wakati wa mkutano huo mapema leo 7 Machi
Msanii wa filamu ya Shoe Shine na Samaki Mchangani, Amri Shivji akitoa shukrani zake kwa Serikali. Shivji naye filamu yake ya Samaki Mchangani iliweza kushiriki katika tuzo hizo za AMVCA 2016, kama filamu ya Kiswahili.Msanii Single Mtambalike 'Rich Rich' akizungumza machache juu ya ushindi wake ambapo pia ameipongeza Serikali kwa ushirikiano waliowapa hadi kufikia hapo.
Msanii wa filamu ambaye naye filamu yake ilishiriki katika tuzo hizo za AMVCA 2016 akitoa shukrani zake kwa Serikali 
Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Mh. Nape Nnauye (katikati) akizungumza juu ya kuwapongeza wasanii Rich Rich na Lulu Michael kwa ushindi wao katika tuzo za AMVCA 2016 zilizofanyika nchini Nigeria mwishoni mwa wiki. Wengine ni viongozi wa Wizara hiyo.. Mapema leo 7 Machi.2016
Mkutano huo ukiendelea...
Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akimkabidhi cheti maalum cha pongezi, Msanii wa filamu Amir ShivjiWaziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akitoa vyeti kwa wasanii waliofanya vizuri.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akimkabidhi cheti cha pongezi Joseph Lukaza Mwakilishi wa Proin akipokea cheti kwa niaba ya msanii Elizabeth Michael 'Lulu' ambaye bado hajarudi kutoka Nchini Nigeria.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akimkabidhi cheti Msanii Rich Rich kama pongezi kwa Serikali. Kulia anayeshuhudia ni Katibu wa Bodi ya filamu ya ukaguzi na Michezo ya kuigiza, Bi. Joyce Fisso wakati wa mkutano huo mapema leo 7 Machi.2016
Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akipokea tuzo hiyo kutoka kwa msanii Rich Rich.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akiwa amebeba tuzo hiyo kama ishara ya kuwawakilisha watanzania wote.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye na Msanii Rich Rich (katikati ) wakiwa katika picha ya pamoja wasanii wengine na viongozi wa Wizara hiyo.
Katibu wa Bodi ya filamu ya ukaguzi na Michezo ya kuigiza, Bi. Joyce Fisso akipiga picha ya ukumbusho na Msanii Rich Rich wakati wa mkutano huo mapema leo 7 Machi.2016. Mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).

Serikali kupitia Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, wamewapongeza wasanii wa Tanzania kwa kuipeperusha vyema Bendera ya Tanzania nje ya mipaka kwa kufanya vizuri na kuibuka na ushindi ikiwemo tuzo katika filamu bora za Kiswahili zinazotoka Tanzania.

Akitoa pongezi hizo mapema leo 7 Machi.2016, Waziri wa Habari, Mh. Nape Nnauye aliyetembelewa ofisini kwake na wasanii mbalimbali wa filamu nchini waliowasindikiza washindi wa tuzo hizo za African Magic Viewers’ Choice Awards (AMVCA2016) zilizotolewa mwishoni mwa wiki nchini Nigeria,

Akiwemo mshaindi wa tuzo ya filamu Bora ya Lugha ya Asili (Best Local Language -Swahili) kupitia filamu ya ‘Kitendawali’, Msanii Single Mtambalike ‘Rich Rich’ pamoja na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba ambapo Waziri aliwapongeza kwa mshikamano wao huo waliouonyesha na hata kurudi kutoa pongezi.

Waziri Nape amebainisha kuwa, awali Rich Rich kabla ya kwenda Nigeria, alipata Baraka kutoka kwake hivyo hata kurejea kutoa shukrani ni jambo jema huku akieleza kuwa, Serikali itahakikisha inawalea wasanii katika umoja pamoja na kuweka mazingira mazuri ya ufanisi katika shughuli zao ikiwemo kuandaliwa Sera, kanuni na misingi ya sharia katika kuifanya tasnia ya filamu kuwa ya kimataifa zaidi na yenye kuleta fursa za ajira kwa wasanii ndani na nje.

“Kwa nafasi yangu ya Uwaziri. Nitahakikisha nawapigania wasanii kufikia malengo tuliyoyakusudia. Hii ni paamoja na kuwa na Sera madhubuti na kuzuia mianya ya wafujaji wa kazi za Wasanii wa Tanzania. Serikali ya awamu ya tano kupitia kwa Rais wetu Mh. Dk. John Pombe Magufuli ameanza na ili la stika za TRA

na munashuhudia wenyewe Mamlaka ya Mapato inavyopambana na watu wanaorudisha maendeleo ya wasanii nyuma kwa kufunga maduka yao huu ni mwanzo tutapambana mpaka mwisho katika hili” alieleza Mh.Nape na kupaata pongezi kutoka kwa wasanii wenyewe ambao waliweza kushangilia kwa kauli hiyo ya matumaini huku wakipiga makofi.

Aidha, katika tukio hilo, Serikali imeweza kuwatunukia wasanii hao walioshinda tuzo hizo za AMVCA 2016 vyeti maalum vya shukrani hii ni pamoja na wasanii wote ambao filamu zao pia zilienda kushindanishwa huko pamoja na waandaaji waliowezesha filamu hizo kwa mchango wao mkubwa.

Katika tuzo hizo mbali na Rich Rich, kushinad tuzo hiyo, Msanii mwingine aliyeshinda ni pamoja na Msanii Elizabeth Michael (Lulu) akishinda tuzo ya Filamu Bora ya Afrika Mashariki (Best Movie -Eastern Africa) kupitia filamu yake ya ‘Mapenzi’.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo

MADAKTARI watatu, wauguzi sita na watumishi wengine wawili katika Hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure pamoja na ya Wilaya ya Nyamagana, Butimba, wamesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwamo kusababisha vifo vya watoto pacha na mjamzito.

Uamuzi huo umechukuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, kutokana na vifo vya watoto wanne waliozaliwa pacha kutoka kwa wanawake wawili tofauti. Pia katika kadhia hiyo, mama mmoja ambaye watoto wake walifariki, naye alifariki. Akinamama hao wametajwa kuwa ni Suzana John ambaye alijifungulia watoto mapacha kwenye beseni katika Hospitali ya Butimba.

Watoto hao walifariki dunia kwa kukosa huduma muhimu za afya. Mwingine ni Pendo Masanja ambaye alijifungua mapacha waliokufa na yeye kupoteza maisha kutokana na upungufu wa damu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Sekou Toure; saa moja na robo baada ya watoto wake kufariki.

Mkuu wa Mkoa alisema uamuzi wa kuwasimamisha kazi watumishi hao wa afya umefanyika baada ya kugundua kuwa kulikuwepo uzembe mkubwa wa kitaaluma pamoja na lugha chafu ambazo zilitumiwa wakati wa kuwahudumia wajawazito hao wawili. Akizungumza na madaktari na wauguzi katika Hospitali ya Sekou Toure, Mulongo alisema matukio hayo yote yameleta taswira mbaya kwa Mkoa wa Mwanza kutokana na ukweli kuwa shughuli zinazofanywa na taasisi hizo zina lengo la kuokoa maisha ya watu.

Alimuagiza Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Ndalo Kulwijira kuwasimamisha kazi madaktari na wauguzi wote waliohusika katika kusababisha vifo hivyo kwenye hospitali hizo mbili tofauti. “Hospitali ya Sekou Toure ndiyo inabeba taswira ya huduma za afya kwa mkoa wetu. Kwa heshima ya hospitali hii, madaktari waliohusika kusababisha vifo katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana (Butimba) na hapa Sekou Toure tumewasimamisha kazi kupisha uchunguzi.

Hatuwezi kuwa na chombo ambacho watumishi wake hawawajibiki katika kuwahudumia watu,” alisema. Waliosimamishwa Butimba Waliosimamishwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana iliyoko Butimba kwa kuhusishwa na mjamzito aliyejifungulia katika beseni ni Dk Nathan Mbagaya, wauguzi Furaha Kingunge na Edina Mwasiga.

Mwingine ni dereva wa gari la wagonjwa, Gharib Hamad aliyedaiwa kutumia muda mwingi kufanya malumbano badala ya kumwahisha, Pendo Masanja katika Hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure ambako alikuwa amepewa barua ya rufaa kwenda. Waliosimamishwa Sekou Toure Aliwataja waliosimamishwa kwa upande wa Hospitali ya Sekou Toure kuwa ni Muuguzi Kiongozi wa zamu siku ya tukio, Happiness Sospeter, muuguzi Angel Chacha, aliyempokea Pendo.

Wengine ni muuguzi Anna Malole na Lucy Kisura ambao walitumwa kwa nyakati tofauti kufuatilia dawa maabara ili Pendo atundikiwe dripu ya damu. Madaktari waliosimamishwa ni Dk Still Mbaga aliyekuwa mganga wa zamu, Dk Jamal Namkarara na mtaalamu wa maabara (kutoa damu) katika Hospitali ya Sekou Toure, Godfrey Silvester ambaye amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi na kuisaidia Serikali kupeleleza tukio hilo.

“Hawa wote wanasimama kazi kuanzia leo (jana) kupisha uchunguzi, lazima kama Serikali tulinde credibility (hadhi) ya hospitali yetu ya mkoa, lengo letu hasa likiwa ni kutenda haki kwa matukio yote mawili,” alisema Mkuu huyo wa Mkoa. “Hawa tunawasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi, kwa kuwa malumbano yao yalisababisha kuchelewa kumpeleka Pendo Masanja katika hospitali ya mkoa, wakijua kuwa aliandikiwa barua ya rufaa.

Watasimamishwa kazi mpaka itakapothibitika baadaye”, alisema Mulongo. Alisisitiza: “Tunataka kuona haki ya marehemu Pendo Masanja na wataalamu waliomsaidia kuokoa maisha yake inapatikana. Tutaangalia ni daktari au muuguzi gani alitenda haki na tukiliacha jambo hili jinsi lilivyo litaleta manung’uniko makubwa, hivyo kama serikali tumechukua hatua.”

Aliwataka watumishi, wauguzi na madaktari wa Hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure kuwa makini katika utendaji kazi wao kwa kutumia viapo vyao kuhudumia wagonjwa. Tume yaundwa Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa ameunda tume kuchunguza matukio hayo. Tume hiyo inaongozwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake kutoka Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Dk Richard Rumanyika na imetakiwa kukamilisha uchunguzi wake kwa siku tano.

Wajumbe wengine wa tume hiyo ni Mwanasheria, Victor Kalumuna kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali; Muuguzi Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Agnes Hassan; Inspekta Haji kutoka ofisi ya RCO Mwanza na Evarist Kunyaranyara. Mashuhuda wazungumza Dada wa marehemu, Debora Hamisi alidai kifo cha ndugu yake kilitokana na uzembe wa wauguzi na madaktari.

Alidai alipofikishwa hospitalini, alichelewa kupatiwa huduma. Mume wa marehemu, Masanja Lucas aliomba serikali imsaidie gharama za maziko. Alisema katika tukio la kifo hicho hawezi kumlaumu Mungu kwani hakuridhika na huduma jinsi walivyopokelewa tangu Hospitali ya Butimba hadi ya Mkoa ya Sekou Toure.

HABARI LEO

Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas (wa pili kulia) akimkabidhi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (wa pili kushoto) moja ya mabegi iliyotoa kwa ajili ya wachezaji wa Timu ya Taifa Mpira wa Magongo chini ya miaka 21. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa mpira wa Magongo, Abraham Sykes akishuhudia tukio hilo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (wa pili kushoto) akiliangalia moja ya mabegi yaliotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya wachezaji wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Magongo chini ya miaka 21. Timu hiyo inayoelekea nchini Namibia kushiriki mashindano ya kufuzu Kombe la Afrika mpira wa magongo chini ya udhamini wa NMB.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akikabidhi bendera kwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Magongo chini ya miaka 21, Elieza Jeremiah (wa pili kushoto). Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa mpira wa Magongo, Abraham Sykes akishuhudia tukio hilo. Timu ya Taifa ya Mpira wa Magongo chini ya miaka 21 inaondoka nchini Machi 3, 2016 kuelekea nchini Namibia kushiriki mashindano ya kufuzu Kombe la Afrika mpira wa magongo chini ya udhamini wa NMB.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati) akifafanua jambo kwa wanahabari katika hafla ya Timu ya Taifa ya Mpira wa Magongo chini ya miaka 21 kukabidhiwa bendera na udhamini wa Benki ya NMB. Benki ya NMB imetoa Shilingi Milioni 25 pamoja na mabegi kwa kila mchezaji anayekwenda kushiriki mashindano ya kufuzu Kombe la Afrika mpira wa magongo.
Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas (kulia) akizungumza kabla ya kukabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Milioni 25 ikiwa ni fedha ya udhamini wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Magongo chini ya miaka 21 inayoelekea Namibia kushiriki mashindano ya kufuzu Kombe la Afrika mpira wa magongo. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akizungumza kabla ya kupokea mfano wa hundi ya Shilingi Milioni 25 iliyotolewa na NMB ikiwa ni fedha ya udhamini wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Magongo chini ya miaka 21 inayoshiriki mashindano ya kufuzu Kombe la Afrika mpira wa magongo yatakayofanyika nchini Namibia. Kulia ni Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas.
Kulia meza kuu ikiongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (wa pili kulia), Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas (wa kwanza kulia) na Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa mpira wa Magongo, Abraham Sykes wakizungumza na waandishi wa habari leo Dar es salaam katika hafla ya Timu ya Taifa ya Mpira wa Magongo chini ya miaka 21 kukabidhiwa bendera na udhamini wa NMB.
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa mpira wa Magongo, Abraham Sykes, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas wakijibu maswali ya wanahabari katika hafla ya timu hiyo kukabidhiwa bendera na udhamini wa NMB.







Mshambuliaji wa Simba,Hamis Kiiza (katikati),
Dar es Salaam. Waswahili wanasema vita ya panzi furaha ya kunguru, ndicho kilichotokea baada ya sare ya Yanga na Azam kuinufaisha Simba kukalia usukani wa Ligi Kuu Bara kwa kuichapa Mbeya City kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mshambuliaji Danny Lyanga aliyeingia akitokea benchi kuchukua nafasi ya Brian Majwega aliifungia Simba bao la kuongoza dakika ya 72, baada ya kuunganisha mpira uliotemwa na kipa wa Mbeya City, Hannington Kalyesebula aliyepangua shuti la Awadh Juma.


Simba ilijihakikishia pointi tatu muhimu dakika ya 90, baada ya beki wa Mbeya City, Hassan Mwasapili kujifunga mwenyewe wakati akijaribu kuokoa krosi iliyopigwa na Ibrahimu Ajib na kumpita kipa Kalyesebula. Kwa ushindi huo, Simba imefikisha pointi 48 na kukalia usukani ikifutiwa na Yanga na Azam zenye pointi 47, baada ya kutoka sare 2-2 juzi.

Akizungumzia nafasi ya timu yake katika mbio za ubingwa, Kocha wa Simba, Jackson Mayanja alisema kwa sasa kikosi chake kimekamilika na amejipanga kwa mechi zote zilizobaki.

“Lengo ni kumaliza katika nafasi ya juu zaidi, ushindi huu umetuongezea nguvu kufikia mafanikio hayo, hatukujiandaa kwa ajili ya Mbeya City pekee ila timu zote,” alisema Mayanja.

Katika mchezo huo, kinara wa ufungaji wa Simba, Hamis Kiiza alishindwa kuonyesha makali yake akipoteza nafasi kadhaa za kufunga kama ilivyokuwa kwa kiungo wa Mbeya City, Haruna Moshi ‘Boban’.

Hata hivyo, Mbeya City watajilaumu wenye kwa kushindwa kutumia nafasi nyingi katika kipindi cha kwanza kushinda mchezo huo.

Mwanzoni mwa kipindi cha pili, Kocha wa Simba raia wa Uganda, Mayanja alilazimika kufanya mabadiliko kwa kuwatoa Majwega, Kiiza na Emery Nimubona kuwaigiza Lyanga, Awadhi Juma na Ramadhan Kessy; wakati mpinzani wake raia wa Malawi, Kinnah Phiri akiwatoa Boban na Ditram Nchimbi na kuwaingiza Themi Felix na Ramadhani Chombo ‘Redondo’.

Mabadiliko hayo yalikuwa na faida kwa Simba na kurudi mchezo kwa kugongeana pasi za haraka na kupitisha mashambulizi yao kutokea pembeni kwa Kessy na Mohamed Hussen na kufanikiwa kuifungua ngome ya Mbeya City na kupata mabao yao mawili.

Kocha wa Mbeya City, Phiri alisema wachezaji wake walicheza vizuri makosa madogo katika safu ya ulinzi yamewagharimu.

“Simba ina wachezaji wengi wenye uzoefu, wametumia vizuri nafasi chache walizopata kutufunga,” alisema Phiri.

Simba: Vicent Angban, Emery Nimubona, Mohamed Hussen, Novaty Lufunga, Juuko Murshid, Justine Majabvi, Mwinyi Kazimoto, Jonas Mkude, Hamis Kiiza, Ibrahimu Ajibu na Brian Majwega.

Mbeya City: Hannington Kalyesebula, Hassan Mwasapili, Abubakar Shaban, Tumba Sued, Haruna Shamte, Kenny Ally, Raphael Alpha, Haruna Moshi, Geofred Mlawa, Joseph Mahundi na Ditram Nchimbi.
Uamuzi wa Rais Dk. John Magufuli wa kuwarejesha nyumbani mabalozi waliomaliza muda wa utumishi wao umekwamishwa na ukata, imeelezwa.
Januari 25, mwaka huu, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alitangaza agizo la rais kwa Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga, kuwarejesha nyumbani mara moja mabalozi wawili ambao mikataba yao imekwisha.

Mabalozi hao ni Dk. Batilda Buriani aliyeko Tokyo Japan na Dk. James Msekela, aliyeko Rome, Italia.

Akizungumza na waandishi wa habari, Balozi Sefue alisema siku hiyo mabalozi hao walitakiwa kukabidhi kazi kwa maafisa wakuu au waandamizi ambao wako chini yao.

Hata hivyo, jana Waziri Mahiga alipoulizwa juu ya agizo hilo, alisema kukosekana kwa fedha kumekuwa kikwazo katika kulitekeleza agizo hilo lakini kwa sasa wako katika hatua za mwisho kuhakikisha fedha za kugharamia usafiri, posho na mizigo yao zinapatikana.

Februari 15, mwaka huu, Rais Magufuli aliwateua aliyekuwa Waziri wa Sheria na Katiba katika serikali ya awamu ya nne, Dk. Asha-Rose Migiro, Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau kuwa mabalozi.

Tarifa ya Ikulu juu ya uteuzi wao iliyotolewa na Balozi Sefue ilieleza kuwa vituo vya mabalozi hao wapya vitajulikana baada ya taratibu husika za kidiplomasia kukamilika.

Lakini Dk. Mahiga alitolea ufafanuzi kuwa mabalozi watatu walioteuliwa na rais wanasubiri kupangiwa vituo vya kazi na kwamba kuwapeleka na kuwarudisha watumishi ni gharama kubwa ambayo inahitaji maandalizi.

“Kuwarudisha mabalozi na watumishi hawa ni gharama kwani wanahitaji marupurupu yao na kusafirisha mizigo na wakati mwingine haikuwa kwenye kasma yetu, lakini watarudi kwa kuwa tumeshapata fedha za kuwagharimia,” alisisitiza.

Hadi sasa vituo sita vya ubalozi viko wazi ambavyo ni London nchini Uingereza, Tokyo (Japan), Rome (Italia) na Brussels (Ubelgiji) kutokana na aliyekuwa Balozi Dk. Deodorous Kamala kuchaguliwa kuwa mbunge.

Wengine ni Kuala Lumpar, Malaysia kutokana na Balozi Dk. Aziz Mlima kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa na Brasilia, Brazil baada ya Balozi Francis Malambugi kustaafu.

Balozi mwingine aliyerejeshwa nyumbani ni Balozi wa Tanzania aliyeko London, Uingereza, Peter Kallaghe, anayerejea wizarani kupangiwa kazi nyingine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi pamoja na Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara mbalimbali mara baada ya kuisha tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU.









Mara kadha alitafutwa kwa bakora ! Mdomo wake ndio chanzo

Hakuna kazi isiyokuwa na ugumu,watunzi na waimbaji wa muziki nao wanakumbana na ugumu katika kazi zao,mmoja wao katika ya wanamuziki

wanaopata misuko suko kazini ni mwanamuziki nguli Ebrahim Makunja alimaarufu Kamanda Ras Makunja mkuu wa kikosi cha Ngoma Africa band aka FFU wenye maskani kule Ujerumani.

Mwanamuziki mtanzania Kamanda Ras Makunja mtunzi,mshairi mwimbaji aliyepindia akili kazi yake,ametunga na kuimba nyimbo nyingi zenye utamu na uchungu,lakini katika nyimbo zote wimbo wa "Baba wa Kambo" ni wimbo uliompa wakati mgumu sana,mara tatu kutafutwa na bakora na wazee walioguswa na wimbo huo,akiwamo mtu mzima Malumba Kassongo alishawahi mara mbili kuvamia kambi ya bendi hiyo kwa bakora na kudai


kuwa kamanda Ras Makunja lazima atiwe adabu kwani mdomo wake

si mzuri,mzee huyo amedai mtunzi wa nyimbo hiyo "Baba wa Kambo" amekuwa akiyachunguza maisha ya mzee huyo. pamoja na makubaliano mbele ya wapatanishi kuwa nyimbo hiyo isiende hewani lakini bendi hiyo imekiuka makubaliano na kurusha hewani tena song hilo "Baba wa Kambo"

jiburudishe na song hilo chini.
https://soundcloud.com/issamichuzi/kamanda-ras-makunja-baba-wakambo1
Kipindi JUKWAA LANGU Jumatatu hii

Kitu kikubwa kilichochukua Headline za magazeti na mitandao mbali mbali ya kijamii leo ni kuhusu Balozi Ombeni Sefue kuondolewa Ukatibu Mkuu kiongozi kwa mtizamo wako unafikiri nini inaweza kuwa sababu kubwa

Zanzibar USIKOSE

Jumatatu kuanzia saa 11 kamili jioni (5:00pm) EST kwa saa za Marekani ya Mashariki.
 Piga simu 240 454 0093 utuambie ni nini maoni yako kwa Tanzania uipendayo 



No comments:

Post a Comment