| 
 
MWAMBATA WA ZAMANI WA JESHI UBALOZI WATANZANIA NCHINI  MAREKANI NA CANADA BRIGADIEAR GENERAL EMMANUEL  MAGANGA ASTAAFU RASMI
 
Mwambata
 jeshi wa zamani nchini Marekani na Canada Brigadier General Emmanuel 
Edward Maganga siku  ya ijumaa trh 04 March alikuwa miongoni mwa 
majenerali 16 walioagwa rasmi baada ya kustaafu utumishi jeshini. 
Jenerali Maganga amestaafu akiwa na wadhifa wa Mkaguzi Mkuu wa Jeshi. 
Amelitumikia jeshi kwa takriban miaka 37 na mwezi mmoja. Katika utumishi
 wake zaidi ya kuwa Mwambata jeshi USA na Canada pia aliwahi kuwa 
Mwambata Jeshi nchini Africa ya Kusini akiwa pia analiwakilisha jeshi 
katika  nchi za Angola, Botswana,Lesotho na Namibia. Watanzania walioko 
Marekani watakumbuka upendo wake kwao akiwa  na mke wake Untie Love  na 
ushiriki wao usiobagua katika matukio ya raha na shida. Timu ya 
VIJIMAMBO inamuombea maisha mapya ya furaha na kumkaribisha URAIANI. 
Hongera SANA Kamanda, mwanataaluma ya uandishi wa habari,  
mwanadiplomasia, mwanamikakati, Mkaguzi uliyebobea na mwanamichezo 
madhubuti. 
![]() ![]() ![]()  | 
| 
 
Mbunge
 wa Viti Maalum CCM mkoa wa Arusha Mhe. Catherine Magige, leo amekabidhi
 ofisi ya UWT mkoa wa Arusha ambayo amefanyia ukarabati na kuweka vitu 
vya thamani iliyogharimu shilingi milioni 6 na nusu.   
Mbunge
 wa Viti Maalum CCM mkoa wa Arusha Mhe. Catherine Magige akicheza ngoma 
na viongozi wa UWT mkoa wa Arusha mara baada ya kukabidhi ofisi ya UWT 
aliyokarabati kwa gaharama ya shilingi milioni 6.5 ,ambapo ofisi 
imepakwa rangi ,kuwekwa tiles , viti, meza , amakabati pamoja na TV. 
Mbunge
 wa Viti Maalum CCM mkoa wa Arusha Mhe. Catherine Magige akiwa kwenye 
picha ya pamoja na viongozi na wajumbe wa UWT mkoani Arusha. 
 | 
| 
 
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AWAHUTUBIA WANAWAKE KWENYE MAADHIMISHI YA KIMATAIFA YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
 
Makamu
 wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan 
katikati akiwa katika picha ya pamoja Viongozi wa Kampuni ya TRUMARK 
iliyoandaa sherehe ya maadhimisho ya siku ya Ki,ataifa ya Wanawake 
Duniani alipowasili katika ukumbi wa Kingsolomon Kinondoni jijini Dar es
 salaam jana jioni  March 05,2016 kwa ajili ya kuhudhuria Maadhimisho 
hayo. 
 | 
| 
 
Bi. Mindi Kasiga naye akitolea ufafanuzi ratiba nzima ya ziara ya Rais huyo wa Vietnam. 
Sehemu nyingine ya waandishi wa Habari wakinukuu baadhi ya pointi wakati mkutano ukiendelea. Picha na Reginald Philip 
Rais
 wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang atakuwa 
Rais wa kwanza kufanya ziara ya kitaifa nchini Tanzania katika Serikali 
ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Rais 
Sang atawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere 
siku ya Jumanne tarehe 08 Machi 2016 saa mbili usiku na kupokelewa na 
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na 
Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ambapo mapokezi rasmi yatafanywa 
siku ya pili na mwenyeji wake, Rais Dkt. Magufuli katika Viwanja vya 
Ikulu. 
Akiongea
 na Waandishi wa Habari Ofisini kwake leo, Waziri Mahiga alieleza kuwa 
Rais Sang atafutana na mke wake, Mama Mai Thi, Mawaziri watano na 
Wafanyabiashara 51 katika ziara hiyo. Dkt. Mahiga alieleza kuwa Serikali
 inaupa uzito wa pekee ugeni huo kwa sababu ni ziara ya kwanza ya 
kitaifa katika Awamu ya Tano kufanywa na Mkuu wa Nchi. “Wakuu wa Nchi 
kadhaa walishakuja hapa nchini lakini kwa ziara za kikazi, sio za 
kiserikali, hivyo Vietnam imetupa heshima kubwa sana”.  Waziri Mahiga 
alisema. 
Rais
 Sang ni mara ya kwanza kufanya ziara katika Bara la Afrika na Tanzania 
ambapo pia atazuru nchi ya Msumbiji baada ya kuondoka hapa nchini tarehe
 11 Machi 2016. 
Dkt.
 Mahiga aliwambia Waandishi wa Habari kuwa Tanzania ina mambo mengi ya 
kujifunza kutoka Vietnam namna ilivyopiga hatua kubwa ya maendeleo 
katika kipindi kifupi, licha ya kuendesha vita kubwa ya mapambano ya 
kupigania uhuru dhidi ya Ufaransa na baadaye dhidi ya Marekani. Alisema 
nchi hiyo imepiga hatua katika sekta za viwanda, kilimo, mawasiliano na 
uvuvi.  Kwa upande wa kilimo, nchi hiyo ni ya kwanza kwa kuuza kahawa 
aina ya robusta na korosho duniani ingawa mbegu za mazao hayo 
zimechukuliwa Tanzania.  
Aidha, Vietnam ni maarufu duniani kwa kuuza samaki aina ya sato ambao walichukuliwa kutoka Ziwa Victoria. 
Waziri
 wa Mambo ya Nje alieleza kuwa ili Tanzania nayo ifike ilipo Vietnam ni 
lazima ifuate mambo matatu ambayo Vietnam inayazingatia. Mambo hayo ni 
kufanya kazi kwa bidii katika mazingira ya aina zote, utekelezaji wa 
maamuzi wanayofanya na kuwekeza katika mafunzo ya ufundi, miundombinu 
kama ya umeme, barabara, reli, bandari na mabemki kwa ajili ya mitaji na
 huduma nyingine za kifedha. 
Katika
 ziara hiyo, Rais wa Vietnam pamoja na mambo mengine atafanya mazungumzo
 rasmi na mwenyeji wake; Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein;
 Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Spika wa Bunge la 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai; Kuongea na 
wafanyabiashara na kutembelea eneo la uwekezaji la EPZA, Ubungo Jijini 
Dar es Salaam. 
 | 
| 
 
Mkuu
 wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Rajabu Rutengwe aliyekaa baada ya kuikabidhi 
Shule ya Msindi Mindu madawati  yaliyochangwa na wanafunzi wa somo la 
Menejimenti katika Chuo Kikuu Mzumbe mwishoni mwa wiki.  Wengine ni 
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Josephat Itika (wa pili 
kulia), Mkuu wa Skuli ya Utawala na Menejimenti,  Dkt. Stella Kinemo 
(kulia); Mratibu wa Mradi wa Madawati, Bw. Aloyce Gervas (kushoto), 
muwakilishi wa wanafunzi wa Menejimenti, Bw. Vivans Roseline (wa pili 
kushoto) na wanafunzi wa shule hiyo ya msingi. 
 | 
TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Monday, March 7, 2016
MFANYABIASHARA WA UTALII ARUSHA ATOA MISAADA YA KIJAMII HOSPITALI MKOA WA ARUSHA LEO. MTAZAME RAIS MAGUFULI AKIMTANGAZA KATIBU MKUU MPYA IKULU JIJINI DAR Kichupa cha leo #LETIGO by Nameless and Nyashinski WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA AENDELEA NA ZIARA MKOANI SIMIYU MWAMBATA WA ZAMANI WA JESHI UBALOZI WATANZANIA NCHINI MAREKANI NA CANADA BRIGADIEAR GENERAL EMMANUEL MAGANGA ASTAAFU RASMI CATHERINE MAGIGE AKARABATI OFISI YA UWT MKOANI ARUSHA RAIS MAGUFULI AMTEUA BALOZI JOHN WILLIAM KIJAZI KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AWAHUTUBIA WANAWAKE KWENYE MAADHIMISHI YA KIMATAIFA YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI DKT. SHEIN AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KWENYE MAZISHI YA MZEE HAMID AMEIR MUASISI WA MAPINDUZI RAIS WA VIETNAM KUFANYA ZIARA YA KWANZA YA KITAIFA NCHINI VIJIMAMBO INAKUTAKIA JUMAPILI NJEMA NA UPENDO NKONE- HALELUYA USIFIWE HAPPY BIRTHDAY UDSM YAKANUSHA TAARIFA ZA KUWANYANYASA WATUMISHI WAKE CHUO KIKUU CHA MZUMBE CHAPONGEZWA KWA KUIMARISHA ELIMU NCHINI DAR USIKU, UNAWEZA KUDHANI UKAHABA UMEHALALISHW IKULU YAVUNJA UKIMYA SAKATA LA UMEYA DAR CHADEMA YACHAMBUA SIKU 120 ZA MAGUFULI VIDEO: LULU NA RICHIE WASHINDA TUZO ZA AMVCA 2016 MAONESHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KATIKA VIWANJA VYA MNARA WA KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI KISONGE ZANZIBAR MAGAZETI YA MARCH 06, 2016 SHEREHE YA RED CARPET DAY SEATTLE WA. Bocco avuruga chereko Yanga Chadema Monduli yamkubali Magufuli Mama afariki dunia pamoja na watoto wake wachanga kwa kukosa damu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


















No comments:
Post a Comment