TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Friday, March 11, 2016

ZEC yawanoa mawakala wa uchaguzi

Na Ali Issa, MAELEZO-ZANZIBAR 

WILAYA YA KASKAZINI A

MAWAKALA 1,500 kutoka vyama mbalimbali vya siasa kutoka majimbo manne ya Mkoa wa Kaskazini Unguja, wamepatiwa mafunzo ya usimamizi wa uchaguzi wa marudio wa Zanzibar, unaotarajiwa kufanyika Machi 20, mwaka huu.

Mafunzo hayo yametolewa leo katika skuli ya msingi Mahonda, yakishirikisha mawakala kutoka majimbo ya Donge, Mahonda, Bumbwini na Kiwengwa.Akifungua mafunzo hayo, Msimamizi Mkuu wa uchaguzi Wilaya ya Kaskazini ‘B’ Makame Khamis Pandu, amesema lengo la Tume ya Uchaguzi Zanzibar kutoa mafunzo hayo, ni kuwawezesha kutekeleza majukumu yao katika kufanikisha uchaguzi huo.

Aidha alifahamisha kuwa, uwakilishi mzuri wa vyama vyao ndio utakaosaidia kuendesha uchaguzi usiokuwa na mivutano na hivyo kuendeleza amani na utulivu nchini.“Mafunzo haya ni muhimu kwenu kwani nyinyi ndio mnaotegemewa na vyama vyenu katika kuviwakilisha na kuhakikisha zoezi la kusebu kura linafanyika kwa uwazi pasi na matatizo yoyote,” alieleza Pandu.

Msimamizi huyo alisema wakala wa vyama vya siasa hapa Zanzibar wapo kwa mujibu wa sheria ya Tume ya Uchaguzi na ushiriki wao ni muhimu katika kufanikisha zoezi hilo na kuondoa kasoro zinazoweza kujitokeza.

Mafunzo hayo ya siku moja ni miongoni mwa hatua za tume kuwapa elimu wadau wote wa uchaguzi wakiwemo makarani wataobahatika kuteuliwa kwa ajili ya shughuli hiyo muhimu ya kutafuta Rais na viongozi wa majimbo.

Kwa hivyo, aliwataka mawakala hao kuyapokea vyema mafunzo hayo na kasha wakayafanyie kazi kwa manufaa ya taifa.Washiriki wa mafunzo hayo walihakikisha kwamba watayafanyia kazi maelekezo yote na kuwajibika kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi.

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR-

No comments:

Post a Comment