Mwathirika
 wa ugonjwa wa Kisukari, Ramadhan Mongi akizungumza na waandishi wa 
habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na kufuata sheria za ulaji ili
 kuepukana na ugonjwa wa kisukari ambao ni ugonjwa usaosababishwa na 
ulaji mbaya wa chakula pamoja na kutokufanya mazoezi.
Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ugonjwa wa Kisukari(Tanzania 
Diabets Association), Profesa Andrea Swai katikati, kulia ni Mwathirika 
wa ugonjwa wa Kisukari, Ramadhan Mongi na Mratibu wa Mpango wa kitaifa 
wa kisukari Tanzania, John Gadna wakiwa katika mkutano na waandishi wa 
habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na ugonjwa wa Kisukari.
CHAMA cha wagonjwa wa Kisukari Tanzania kushirikiana na wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto 
kuandaa kambi ya upimaji wa ugonjwa wa kisukari bila malipo 
Machi 13 katika viwanja vya shule ya msingi Kibugumu Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ugonjwa wa 
Kisukari(Tanzania Diabets Association), Profesa Andrea Swai jijini Dar 
es Salaam leo amesema kuwa ugonjwa wa kisukari ni ugonjwa ambao 
hauambukizwi ambao husababishwa na ulaji mbaya.
 Swai amesema kuwa madaktari na 
matabibu watakuwepo kwaajili ya kupima afya ya kinywa, kupima uzito 
naushauri wa lishe siku hiyo na 
watakaogundulika matatizo maalumu watapewa rufaa.
Swai amesema kuwa ugonjwa wa kisukari husababishwa na ulaji mbovu (kula 
vyakula vilivyokobolewa), kutokufanya mazoezi na kutokula matunda.
Amesema kila watu 100 wakikusanyika kwa kupima ugonjwa wa kisukari hapo 
utawapata watu 9 wenye kisukari na 2 wanakuwa wanajua na wengine 7 
hawajui kama wanaugonjwa huo.
Aidha ametoa wito kwa jamii kufuata kanuni bora za ulaji wa chakula ili kuepukana na ugonjwa huo usio wa kuambukizwa.


No comments:
Post a Comment