Naibu
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. 
Hamisi Kigwangalla ametoa siku tatu kwa uongozi wa Hospitali y teule ya 
rufaa ya Mkoa wa Pwani-Tumbi kufunga chumba cha kuhifadhi maiti 
(Mochwari) baada ya kubaini matatizo mbalimbali baada ya kufanya ziara 
katika hospitali hiyo.
Katika
 ziara hiyo, Dk. Kigwangalla alibaini mambo mbalimbali kutoenda sawa 
ikiwemo suala la utendaji mbovu ambapo alitoa agizo la kumtaka 
Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha wanaosimamia Hospitali hiyo kutoa 
maelezo ndani ya masaa 24 kama anafaa kubaki ama la!.
Aidha,
 Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, hali aliyoikuta katika chumba cha 
kuhifadhia maiti ni mbaya hivyo ilikuondoa matatizo amelazimika kuifunga
 kwa muda huo wa siku tatu ilikufanyia marekebisho kwa baadhi ya mambo 
ndani ya chumba hicho cha mochwari hospitalini hapo.
Awali
 vyombo vya habari vilitoa taarifa mbalimbali juu ya Mochwari hiyo 
ikiwemo badhi ya maiti kuhifadhiwa nje na kuatarisha afya za wananchi.
Naibu
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. 
Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa na uongozi wa Hospitali hiyo akiwemo
 Mganga Mkuu wa Hospitali, Dk. Peter Datani (kulia) akitembelea katika 
hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Pwani-Tumbi wakati wa ziara hiyo mapema 
jana Machi 10.2016.
Naibu
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. 
Hamisi Kigwangalla akikagua Mochwari ya Hospitali ya Rufaa ya Tumbi.


No comments:
Post a Comment