TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, March 7, 2016

WAZAZI WAOMBA SEREKALI KUCHUNGUZA KWANINI WATOTO WAO WANAFELI SANA WILAYANI KARATU.


Wazazi hao wametoa kilio hicho kufuatia ufauulu duni wa mara kwa mara kwa watoto wanaohitimu darasa la saba ambapo wanafunzi hao wamekuwa wanahitimu wakiwa hawajui kusoma wala kuandika na kushika nafasi za mwisho kitaifa katika mtihani wa darasa la saba jambo ambaalo wanaliona kama kuwapotezea muda watoto hao ambapo wazazi hao wakiwa wanawaitaji kuwachungisha mifugo. 

Aidha Kata hii ya Barai yenye shule 12 za msingi ambapo kati ya shule hizo shule sita zimefanya vibaya kitaifa na zimeshikilia nafasi za mwisho kabisa kitaifa ambapo alisema shule sita izo zipo katika nafasi za shule kumi zilizofanya vibaya kitaifa katika mtiani wa darasa la saba kwa mwaka jana. 
Mwandishi wa habari hii alitembelea shule tatu za Kata hiyo kujua sababu zinazosababisha kutafaulu kabisa kwa wanafunzi ambapo taarifa zinaonyesha kuwa kuwa shuke hizo zina walimu sita pekee ikiwa na maana kila shule yenye madarasa saba ina walimu wawili 
Wakizungumzia sababu za shule hizo kufanya vibaya mmoja wa mwalimu wa shule ya msingi Gidamilanda Paul Hando alisema kuwa ni pamoja na umbali mrefu ambao wanafunzi wanalazimika kutembea wakija mashuleni ambapo wanatembea zaidi ya kilimeta 24 kwenda shuleni ,pamoja na 
wanafunzi kutumia muda mwingi kuchunga mifugo badala ya kujisomea pindi wanapotoka mashuleni. 
Aidha alibainisha kuwa mbali na tatizo la umbali mrefu pia wanafunzi wamkuwa wakisumbuliwa na tatizo la njaa kwani shule hizo zimekuwa hasipikii wanafunzi mashuleni mchana kutokana na kutokuwa na bajeti hiyo.

Akizungumzia swala hilo mbunge wa jimbo la karatu Willy Qambalo alisema kuwa kwa upande wake anaona suluhisho la kutatua tatizo hilo ni pamoja na  kujenga mabweni ilikuweza kuwasadia wanafunzi kupata elimu ili kila mwanafunzi asome apoapo shuleni ili kuweza kujipatia muda wa kujisomea. 

"unajua kujengwa kwa haya mabweni pia itasiadia kuwapata wanafunzi kirahisi ambao muda wamekuwa wakiacha masomo na kwenda kuchunga mifugo jambo ambalo linapingwa vikali na wazazi wa vijiji hivyo na pia wanafunzi hao watapata muda mrefu wa kujisomea na swala wao kupata njaa litapungua kwani kutakuwa na chakula shuleni kwa ajili yao"alisema Qakambalo

Aidha Tafiti zinaonyesha walimu ,wenye utovu wa nidhamu watoro na walevi katika maeneo ya mijini ndio hupelekwa katika shule hizzo zilizoko maeneo ya porini kama adhabu kwao.Swali la kujiuliza je mwalimu huyu atakuwa na nia ya kuwafundisha wanafunzi?Kupelekwa kwa mwalimu huyu kama adhabu badala ya eyey kuridhia Kujua kusomaa na kandika kwa wanafunzi hawa itakuwa ni ndoto.

No comments:

Post a Comment