Na Mwandishi Wetu.
IDADI ya abiria wa Shirika la ndege la Air Tanzania (ATCL)
imezidi kuongezeka kila kukicha kutokana na wananchi kuonyesha uzalendo na
imani kwa kampuni hiyo , Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Paul Chizi amesema.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari
jana Chizi alisema kutokana na imani hiyo, kampuni yake imejizatiti kuleta
mabadiriko makubwa katika sekta ya usafiri wa anga kupitia mpango wa maendeleo wa miaka mitano wa shirika hilo.
Chizi alisema tangu uzinduzi wa safari za Dar es
Salaam-Kilimanjaro-Mwanza wiki moja iliyopita kwa kutumia ndege ya aina ya Boeing
737-500,kampuni yake imekuwa ikijaza abiria takribani 106 katika kila safari kwa
siku tatu mfulilizo ikiwemo na siku ya jana hali ambayo inaashiria kuwa
wananchi wameanza kuwa na imani na huduma zinazotolewa na shirika lake.
“Ndege yetu kwa
takribani siku tatu zilizopita imekuwa ikija katika safari zote za Dar es
Salaam-Kilimanjaro-Mwanza . Sikujua kuwa tutakuwa na uwezo wa kurejea na kupata
mapokezi ya namna hii kwa haraka kutokana na kuwa kuna watoa huduma wengine
katika njia hii .
“Baada ya wananchi
kuonyesha imani na uzalendo,tutaendelea na kuongeza nguvu zetu katika kutoa
huduma zetu kwa wakati na kwa bei nafuu. Nawaomba wananchi kuendelea na
uzalendo wanaouonyesha kwa faida ya kampuni yetu na nchi nzima kwa ujumla,”
alisema.
Chizi alisema kuwa mipango ya kampuni hiyo ya kupata ndege
nyingine ambayo itatumika katika safari za kimataifa katika miezi mitatu mpaka
sita ijayo inaenda vizuri na kuongeza kuwa kampuni itatoa taarifa kamili wakati
muafaka utakapofika.
“Kutokana ukweli kuwa tunatarajia kuanza safari za
kimataifa, ni dhahiri kuwa ndege ambayo tunategemea
kuleta lazima iwe kubwa,” aliongeza.
Alisema kuwa kampuni yake kwa sasa imejikita katika utekelezaji
wa mpango wake wa maendeleo wa miaka mitano utakaosaidia kuongeza ubora katika
kampuni hiyo na kuboresha utoaji huduma kwa ujumla.
“Tutajikita katika kuongeza ubora wa huduma tunazozitoa na
vilevile kuchukua nafasi ile tuliyoipoteza hapo nyuma. Tunamatarajio ya kupata
ndege nyingine ya Boeing na mazungumzo yameshaanza na tumefikia pazuri,”
alisema.
Kurudi kwa huduma za ndege ya ATCL kumeanzisha vita ya viwango vya bei za usafiri wa anga
bada ya ATCL kutoza bei ya shilingi 199,00 kwa safari zake kwenda na kurudi
(return ticket) na kusababisha watoa huduma wengine wakiwemo Precision Air nao kupunguza
gharama zao ile ilikukabiriana na ATCL.
No comments:
Post a Comment