Toleo la Leo.
BIA YA CASTLE
LITE SASA KUPATIKANA KATIKA KOPO
Dar es
Salaam, May 28. 2012:
Bia maarufu ya Castle Lite, inayozalishwa na kusambazwa
na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) leo imezindua rasmi muonekano wa kopo lililojazwa
kinywaji hicho ikiwa ni muendelezo wa kuwarahisishia walaji upatikanaji wa Bia
hiyo iliyotokea kupendwa na watumiaji wa vileo na kuifanya iwe bia inayokua kwa
kasi hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo,
Meneja wa Bia ya Castle Lite Bi. Pamela Kikuli alisema; Leo tunazindua ujazo
mpya wa bia ya Castle lite, bia yenu muipendayo kwa sasa inapatikana katika
kopo lenye ujazo wa mililita 330. Uamuzi huu unatokana na mahitaji makubwa toka
kwa watumiaji na wapenzi wa bia hii ambayo imekuwa ikipatikana katika chupa
yenye ujazo wa mililita 375. Wateja wetu walihitaji kuipata bia yao popote pale
walipo au kuwa nayo popote waendapo, hivyo kupatikana kwa bia hii katika chupa
peke yake kulipunguza uhuru wa kuwa na bia yao popote waendapo kwani walihitaji
kurudisha chupa kila waitumiapo.
Uzinduzi wa Castle lite ya kopo utasaidia zaidi kuongeza
upatikanaji wa kinywaji hiki katika maduka ya reja reja (super markets) n.k
kote nchini na kuwapa nafasi wapenzi wa castle lite kununua bia yao waipendayo
na kwenda nayo nyumbani. Bei ya reja reja kwa kopo ni shilingi 1700/- na bei ya
reja reja kwa chupa itaendelea kubaki ile ile 1700/-.
Kwa upande wake Meneja mawasiliano na mahusiano ya jamii
wa Tbl Edith Mushi aliwashukuru wapenzi na watumiaji wa bia ya Castle Lite kwa
kuweza kuipa mafanikio makubwa katika soko la bia hapa nchini,
“ninawahakikishia kuwa mnafanya uamuzi ulio sahihi kwa kuchagua kutumia Castle
Lite” nasi tutaendelea kuwapatia bia iliyo bora siku zote. Alisema Edith.
-MWISHO-
Meneja wa kinywaji cha Castle Lite Pamela Kikuli akizungumza
na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa castle lite ya Kopo, kulia ni meneja
habari na mawasiliano ya Umma wa Tbl Edith Mushi.
No comments:
Post a Comment