TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Monday, May 28, 2012

MAONYESHO YA WANAFUNZI UDOM YAFANA JANA KATIKA UKUMBI WA CHIMWAGA ULIOPO CHUO KIKUU CHA DODOMA(UDOM)

 Muandaaji wa Maonyesho haya Ester Zangi ambaye pia ni Mwanafunzi wa Mwaka wa 3 anayesomea shahada ya kwanza ya sayansi ya siasa na utawala wa umma(Wa Kwanza Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma ambao Wameonyesha vipaji vyao Vya Kuchora Michoro inayoonekana hapo katika maonyesho yaliyofanyika jana Chuo Kikuu Cha Dodoma katika Ukumbi wa Chimwaga
PICHA NA JOSEPHAT LUKAZA WA http://josephatlukaza.blogspot.com
 Mwanafunzi wa Mwaka wa 3 anayesoma shahada ya kwanza ya filamu na sanaa anayejulikana kwa jina la wacko jacko akiwa amesimama pembeni mwa moja ya michoro aliyochora kwa Mikono yake na hapo alikua katika maonyesho yaliyofanyika chuo kikuu cha Dodoma jana
Mmiliki wa Mtandao wa Lukaza Blog Mh Josephat Lukaza (Wa kwanza Kulia) akiwa katika Picha ya Pamoja na Wadau wa Lukaza Blog mara baada ya Kumalizika kwa Maonyesho hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) katikati ni Mh Mzagamba Thobias Kutoka Uswis na Wa Kwanza Kulia ni Atu Mwanafunzi wa Mwaka wa 3 UDOM.
Wanafunzi wa UDOM wanaosoma shahada ya kwanza ya Filamu na Sanaa, Kiswahili wakionyesha uwezo wao wa kucheza boringo katika maonyesho yaliyofanyika jana Katika Ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu Cah Dodoma (UDOM)
Mmoja wa wanakamati wa maandilizi ya maonyesho haya ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa 3 Bi Atu anayesoma shahada ya kwanza ya Mazingira ya Chuo Kikuu Cha Dodoma alipokua akitoa neno wakati wa maonyesho hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Chimwaga uliopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) jana
Mmiliki na Mwendeshaji wa Mtandao wa Lukaza Blog Mh Josephat Lukaza alipokua akitoa maelekezo jinsi ya Lukaza Blog inavyofanya kazi na vilevile Mtandao wa Lukaza Blog unavyopatikana na ulivyoweza kupokelewa Vizuri ndani ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) na vyuo vikuu tanzania wakati wa Maonyesho yaliyofanyika Chuoni hapo jana
Mmoja wa Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sanaa na Filamu Babra Kalugira akiwa kwenye Kirekodi Video (VIDEO CAMERA) akichukua video ya matukio yaliyokuwa yakiendelea katika Maonyesho hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuoni Hapo

No comments:

Post a Comment