Mkuu wa kitengo cha kuzuia na kudhibiti madawa ya kulevya Mkoa wa Arusha
 Mrakibu wa Polisi Hamis Warioba akiwaonyesha waandishi wa habari 
shehena ya mifuko 50 ya bangi iliyokuwa kwenye gari baada ya kukamatwa 
tarehe 23/05/2012 wilayani Longido (PICHA NA GLADNESS MUSHI -ARUSHA)
Mkuu wa kitengo cha kuzuia na kudhibiti madawa ya kulevya Mkoa wa Arusha
 Mrakibu wa Polisi Hamis Warioba akihoji jambo kwa watuhumiwa hao.
MNAMO TAREHE 23/05/2012 MUDA WA SAA 9:00 ALASIRI 
HUKO SINYA VILIMA SABA MPAKANI MWA KENYA NA TANZANIA KATIKA WILAYA YA 
LONGIDO, ASKARI WA JESHI LA POLISI MKOANI HAPA KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI 
WA WANYAMA PORI WALIFANIKIWA KUKAMATA WATU WANNE WAKIWA NA MIFUKO 50 
YA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BANGI KWENYE GARI AINA YA CANTER DCM LENYE 
NAMBA ZA USAJILI T.922 AFJ MALI YA ZEPHANIA S/O KAMBEI MKAZI WA NGARAMTONI.
MADAWA HAYO YALIKUWA YANASAFIRISHWA KUTOKA KATIKA 
VIJIJI VILIVYOPO KANDO YA KANDO YA MLIMA MERU KUELEKEA NAIROBI NCHINI 
KENYA KUPITIA NJIA ISIYO RASMI (MAARUFU KAMA NJIA YA PANYA) ILIYOPO 
HUKO SINYA VILIMA SABA, NA BAADA YA KUONA HIVYO RAIA WEMA WALITOA TAARIFA 
KWA ASKARI HAO NA HATIMAYE KUFANIKIWA KUWAKAMATA.
WATUHUMIWA WALIOKAMATWA KATIKA TUKIO HILO NI BABUU S/O LAIZER (34) MKULIMA, 
MKAZI WA OLDONYOSAMBU,LOMNYAKI S/O LEKIBENGI 
(30) MKULIMA , MKAZI WA OLDONYOSAMBU, JOHN S/O JOSHUA AMBAYE 
NI UTINGO NA NI MKAZI WA OLDONYOSAMBU NA EDWARD S/O MOLLEL (27) 
DEREVA NA NI MKAZI  WA OLDONYOSAMBU.
BADO JESHI LA POLISI MKOANI HAPA LINAENDELEA KUWAHOJI 
WATUHUMIWA HAO ILI KUBAINI WAHUSIKA WENGINE NA PINDI UPELELEZI UTAKAPOKAMILIKA  
WATAFIKISHWA MAHAKAMANI.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI 
MKOA WA ARUSHA,
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA 
POLISI
(SACP) THOBIAS ANDENGENYE
TAREHE 25/05/2012.
No comments:
Post a Comment