Kamati
ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) ilikutana Mei 26 mwaka huu ili kutoa mwongozo wa
nini kifanyike ndani ya Yanga baada ya wajumbe wake kudhaa kujiuzulu.
Kamati ya Uchaguzi ya Yanga ilikuwa imeomba mwongozo huo TFF.
Baada
ya kupata taarifa rasmi kutoka Yanga, Kamati imebaini kuwa Kamati ya
Utendaji ya Yanga imekosa akidi baada ya wajumbe wake wengi kujiuzulu
hivyo kutokuwa na uwezo wa kufanya uamuzi kwa mujibu wa Ibara ya 32(1)
ya Katiba ya klabu hiyo.
Hivyo,
Kamati imetoa mwongozo kwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF ambayo ndiyo
msimamizi wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kuwa ili Kamati ya Utendaji ya
Yanga iwe na nguvu za kikatiba kufanya shughuli zake ikiwemo uamuzi wa
masuala mbalimbali ndani ya klabu hiyo ni lazima iwe na akidi.
Kwa
mujibu wa Ibara ya 29(3) ya Katiba ya Yanga nafasi zilizo wazi katika
Kamati ya Utendaji zinatakiwa kujazwa katika Mkutano Mkuu wa Kawaida
ujao.
Pia
Kamati imebaini uteuzi wa kujaza nafasi zilizo wazi za wajumbe
uliofanywa na Kamati ya Utendaji ya Yanga, Mei 21 mwaka huu ni batili
kwa vile Kamati ya Utendaji iliyofanya uteuzi huo haikuwa na akidi.
Ili
kupata akidi na kufanya uamuzi Kamati ya Utendaji ya Yanga yenye
wajumbe 13 inatakiwa kuwa na asilimia 50 ya wajumbe wote, hivyo ili
wafanye uamuzi halali hawatakiwi kupungua saba.
Kwa
wajumbe ambao hawajajiuzulu; Sarah Ramadhan, Mohamed Bhinda, Tito Osoro
na Salim Rupia kwa sasa hawawezi kufanya shughuli zozote za Yanga hadi
nafasi zilizo wazi katika Kamati ya Utendaji zitakapojazwa.
Kama
inavyoelekeza Katiba ya Yanga, shughuli za kila siku za klabu hiyo
zitaendelea kufanywa na Sekretarieti ya Yanga ambayo kiongozi wake ni
Katibu Mkuu.
Alex Mgongolwa
Mwenyekiti
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji
No comments:
Post a Comment