Mechi
ya kirafiki ya kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Malawi (The
Flames) iliyochezwa Mei 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
imeingiza sh. 40,980,000.
Mapato
hayo yametokana na washabiki 10,767 waliokata tiketi kushuhudia pambano
hilo kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 51,000 na sh. 20,000.
Washabiki 9,365 walikata tiketi za sh. 3,000.
Asilimia
18 ya mapato hayo ambayo ni sh. 6,251,186 ilikwenda kwenye Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa tiketi
(sh. 4,999,800), waamuzi (sh. 1,105,000), usafi na ulinzi (sh.
2,350,000), maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh. 400,000),
Wachina- Beijing Construction (sh. 2,000,000) na umeme (sh. 300,000).
Kwa
upande wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh. 4,714,803,
asilimia 10 ya uwanja sh. 2,357,401, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Afrika (CAF) sh. 1,178,701, asilimia 20 ya Mfuko wa Maendeleo
ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 4,714,803 na asilimia 45 ya TFF (sh.
10,608,306).
No comments:
Post a Comment