TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Sunday, May 27, 2012

Msama Promotions yadaka mtambo wa CD feki

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama amesema kuwa wamefanikiwa kukamata mashine za kudurufu kazi za wasanii wa nyimbo ambazo tathmini yake katika utendaji kazi ni mkubwa ukilinganishwa na mashine nyingine alizowahi kuzikamata.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, Msama alisema utaratibu wa kuwasaka wezi wa kazi za wasanii wa nyimbo za injili unaendelea katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na mashine hizo zilikamatwa mwanzoni mwa wiki iliyopita.

Alisema mbali ya kukamata mashine hizo, pia walifanikiwa kumkamata mhusika anayefanya kazi hiyo, Anord Chrispian ambaye anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma hizo.

Msama alisema wamefanikiwa kukamata mitambo hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na kusisitiza kuwa msako wa kuwabaini watu wanaojihusisha na kazi hiyo ya wizi unaendelea kwa ari na kasi aliyoanza nayo.

Akizungumzia tukio hilo Ofisa Upelelezi wa Jeshi la Polisi ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa sababu za kiintelijensia, alisema mtambo huo wa kudurufu kazi za wasanii ulikamatwa katika nyumba ya mtu anayefahamika kwa jina maarufu 'Msukuma' katika eneo la Kimara Bonyokwa.

Alisema mtuhumiwa alikamatwa akifanya kazi hiyo mchana na baada ya upekuzi wa zaidi ya saa mbili ndani ya nyumba hiyo walikuta mikasi na sindano za kufanya kazi ya kuandaa vifungashi vya CD, VCD, DVD na kaseti zinazozalishwa ndani ya chumba hicho.

Ofisa huyo wa upelelezi alisema kitu kingine kilichokutwa ndani ya chumba hicho ni wino wa kuchanganya katika kuandaa kava za bidhaa zinazozalishwa.

Alisema mitambo iliyokamatwa ni mitatu ya kudurufu CD na DVD, mitambo sita ya kudurufu kaseti na mitambo mitatu ya kuandaa kava za CD, DVD na kaseti.

Alibainisha kuwa uchunguzi wa awali umebainisha kuwa mitambo hiyo ina uwezo wa kudurufu DVD 10,000 na VCD 30,000 kwa wiki na kwamba mmiliki wa mtambo huo ni miongoni mwa wasambazaji wakubwa wa kazi bandia za sanaa ya muziki.

Alisema kati ya maeneo ya Dar es Salaam yanayoongoza kwa kuwa na wazalishaji wa kazi bandia za wasanii Ubungo ndio eneo mama ikifuatiwa na Kimara na viunga vyake.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, mitambo na vifaa vyote vilivyokamatwa vimehifadhiwa katika kituo cha Polisi Kimara Mbezi kwa Yusufu na mtuhumiwa anashikiliwa kwa tuhuma hizo huku uchunguzi ukiendelea dhidi ya tukio hilo.

Kipindi kilichopita Kampuni ya Msama iliwahi kumkamata kiongozi wa mtandao wa kundi la wanyonyaji wa kazi za wasanii wa muziki wa injili, Francis Kamalamu, aliyekuwa akifanya biashara hiyo katika eneo la Ubungo Maziwa, Dar es Salaam.

Maofisa usambazaji wa kampuni hiyo, wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwabaini wezi wa kazi za wasanii na mbinu mbalimbali zinazotumiwa na wasambazaji na wazalishaji wa kazi hizo zimenaswa na zinatumiwa kuwatia nguvuni na taratibu za kisheria kuchukua mkondo wake.

No comments:

Post a Comment