Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Dk. Emmanuel Nchimbi ametua Visiwani Zanzibar
leo ambapo amekemea vitendo vya vurugu,akiahidi Serikali kuwachukulia
hatua ikibidi hata kuwavizia nje ya misikiti kwa wale watakaohusika na
uvunjifu wa amani .
Waziri Nchi aliwasili Mjini Zanzibar akiwa na Mkuu wa Jeshi la
Polisi,Inspekta Jenerali Said Mwema kwa pamoja waliitisha mkutano
uliowakutanisha viongozi wa Jumuiya ya Maimamu
Zanzibar(JUMAZA),Mabalozi, Kamisheni ya Utalii, Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar(JUMIKI).
“Suala
la kufuata sheria halina mjadala,lazima kila mmoja wetu afuate na kutii
sheria hatutawavumilia watakaovuruga amani ya nchi…maandamano yoyote
lazima yapate kibali” Aliwaambia wadau katika mkutano huo uliofanyika
Makao Makuu ya Polisi Zanzibar,Ziwani.
Waziri
Nchi alisema busara ya Polisi imefikia kikomo na kwamba atashangaa sana
akiona busara hiyo ikiendelea wakati kuna watu au kikundi kinavunja
amani ya nchi.
“Tutashangaa
busara ya Polisi ikiendelea wakati watu wanaumia kwa watu wengine
kuvunja amani…hatutakubali, tutaendelea kuviziana hata nje ya misikiti
tutawakamata” Alisisitiza Waziri Nchi.
Waziri
huyo alisema kila mtu anawajibika kitunza amani iliyopo ambapo pia
alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yenye mfumo wa Umoja wa Kitaifa
imefanyakazi nzuri katika kipindi kifupi na kuwapongeza Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein, Makamu wa
Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad na Makamu wa Pili wa Rais
Balozi Seif Ali Idd.
No comments:
Post a Comment