TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, January 28, 2015

TBL YATOA MSAADA WA SH. MIL 45 ZA UCHIMBAJI KISIMA CHA MAJI ZAHANATI YA MJI MWEMA KIGAMBONI

Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bi. Dorice Malulu (kulia), akikabidhi mfano wa Hundi ya Sh. Milioni 45, kwa Mganga Mkuu wa Zahanati ya Mji Mwema, Kigamboni, Bw. Richard Mwita, zilizotolewa na TBL kwa ajili ya ujenzi wa kisima cha maji. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Bodi, Bw. Omari Kombe (kushoto), Bi. Upendo Mwabulambo (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa Mganga wa Manispaa ya Temeke, Bw. Shaidi Simba (wa pili kulia). (Na Mpigapicha Wetu)
 Mwakilishi wa Mganga Mkuu  wa Manispaa ya Temeke, Bw. Shaidi Simba (kulia), akimkabidhi Mhandisi Amiri Msangi mfano wa hundi ya milioni 45 zilizotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa ajili ya kuchimba kisima cha maji kwenye Zahanati ya Mji Mwema. Katikati ni Mganga Mkuu wa Zahanati hiyo, Dkt. Richard Mwita, Mwenyekiti wa Bodi, Bw. Omari Kombe (kushoto) na Muuguzi, Bi. Upendo Mwabulambo. (Na Mpigapicha Wetu)

WAFANYABIASHARA MBEYA WAZUA TAFRANI, WAANDAMANA MAHAKAMANI WAKISHINIKIZA MWENYEKITI WAO AACHIWE

 DSC00992Wafanyabiashara  wanaondesha shughuli zao za kibiashara katika masoko zaidi ya  matano yaliyopo Jijini Mbeya, wakiwa nje ya mahakama ya Mwanzo ya Mbeya mjini, wakishinikiza mahakama hiyo kumuachia huru, Mwenyekiti wa Soko la Soweto  Honola Mbogella ambaye alifikishwa mahakamani hapo na halmashauri ya jiji la Mbeya kwa tuhuma za kuzuia watumishi wa umma kufanya kazi zao. DSC00993

DRFA YAWAOMBA WAPENZI WA MPIRA WA MIGUU KUJITOKEZA KWA WINGI MICHEZO YA TAIFA CUP

 2
Uongozi wa chama  cha soka mkoa wa Dar es salaam,DRFA,umewaomba,mashabiki na wote wenye mapenzi mema ya kandanda,kujitokeza kwa wingi kuzishangilia timu za Dar es salaam zinazoshiriki ligi kuu,Daraja la kwanza na michuano ya taifa Cup wanawake ,ili kutoa hamasa kwa wachezaji.
 
Kesho (januari 28) kutakuwa na mchezo mmoja wa ligi kuu kwa timu ya Simba ya Dar es salaam dhidi ya Mbeya City ya Mbeya,mchezo ambao utakaopigwa katika uwanja wa taifa jijini.
Itakumbukwa kwamba katika mechi mbili za ligi msimu uliopita,Simba na Mbeya City hakuna aliyefanikiwa kumfunga mwenzake,na kujikuta wakiambulia sare ya 1-1 kule uwanja wa Sokoine,na ule wa marudiano uliopigwa kwenye uwanja wa taifa nao kwenda sare ya 1-1.
 
Katika michuano ya taifa Cup,Temeke na Ilala zimefanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali baada ya kupata ushindi kila moja katika mechi za robo fainali zilizopigwa leo (januari 27),ambapo Temeke imeiangamiza bila huruma Mbeya mabao 3-0,huku Ilala ikiizodoa Iringa kwa mabao 2-1.
 
Aidha DRFA imeipongeza timu ya Kinondoni ambayo haikufanikiwa kuingia katika hatua ya mtoano,kwa juhudi kubwa na ushindani iliouonesha licha ya kuondolewa katika hatua ya makundi.
 
Viongozi wa DRFA wamekuwa mfano kwa kujitokeza kushuhudia mechi hizo za Taifa Cup,Ligi kuu na zile za Daraja la kwanza,ili kuongeza chachu kwa timu za Dar es salaam kufanya vizuri.

MAZIKO YA MSHAURI WA RAIS UTALII ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dk.Amani Abeid Karume (kulia) na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhaj Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Viongozi wengine na waislamu mbali mbali wakijumuika kwa pamoja kumswalia  aliyekuwa Mshauri wa Rais wa Utalii Marehemu Issa Ahmed Othman katika Masjid Mahfoudh Mazizini, Marehemu alifariki juzi Nchini India na kuzikwa leo Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja,[Picha na Ikulu.] unnamed2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, (katikati)Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dk.Amani Abeid Karume, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhaj Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Viongozi mbali mbali na Waislamu mbali mbali wakijumuika kwa pamoja kumuombea dua baada ya kumswalia  aliyekuwa Mshauri wa Rais wa Utalii Marehemu Issa Ahmed Othman katika Msikiti Masjid Mahfoudh Mazizini,Marehemu amezikwa leo Kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja,[Picha na Ikulu.] unnamed4Baadhi ya Vijana na wananchi waliobeba Jeneza la Marehemu Issa Ahmed Othman aliyekuwa Mashauri wa Rais Utalii Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiupeleka kuzikwa kijijini Kianga Wilaya ya magharibi Unguja leo jioni,marehemu alifariki juzi Nchini India ambako alikwenda kwa matibabu,[Picha na Ikulu.]

TAARIFA YA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA KWA VYOMBO VYA HABARI

index

Tume imesikitishwa na matukio yaliyotokea tarehe 27/01/2015 huko Mbagala Wilaya ya Temeke Dar-es-Salaam, matukio ambayo yameoneshwa na Kituo cha Televisheni cha “Channel Ten” ambayo yameashiria uvunjifu wa haki za binadamu. Mnamo majira ya saa kumi na robo hadi kumi na nusu jioni, Kituo cha TV cha “Channel Ten” kilirusha picha zilizoonesha kupigwa na Polisi baadhi ya wananchi waliokamatwa kwa kile kilichoelezwa kushiriki mkutano wa Chama cha Wananchi (CUF) uliosemekana kuwa si halali. Tume tayari imeanza kuchunguza tukio hilo na taarifa kamili itatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.
Bahame T. M. Nyanduga MWENYEKITI

Maafisa Mawasiliano watembelea Mradi wa Kuchakata Gesi wa Tanzania Mnazi Bay and Songo Songo Gas Processing Plant na kutoa msaada katika hospital ya Ligula

unnamedMkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO Assah Mwambene (kulia) akikabidhi kwa niaba ya Maafisia Mawasiliano Serikalini msaada wa Kitanda cha wagonjwa kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula Mkoani Mtwara Dkt. Mohamed Abraham Gwao walipotembelea Hospitalini hapo leo.
unnamed1Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO Assah Mwambene (kulia) akikabidhi kwa niaba ya Maafisia Mawasiliano Serikalini msaada wa Kitanda cha wagonjwa kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula Mkoani Mtwara Dkt. Mohamed Abraham Gwao walipotembelea Hospitalini hapo leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Innocent Mungy.

ABDULRAHMAN KINANA: WAFUASI WA CHAMA CHA CUF WAKO KIFUNGONI

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana yuko katika ziara ya kikazi ya kisiwa cha Pemba akihimiza na kukagua utekelezaji wa  ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwa ni pamoja na kuhimiza uhai wa chama hicho kisiwani humo. 10 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wengine wakishiriki ujenzi wa tuta la kuzuia maji chumvi katika bonde la Mpunga la Koowe Wingwi Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba , kulia ni Vuai Ali Vuai Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba Ndugu Omar  Khamis Othman.

Tuesday, January 27, 2015

BREAKING NEWS . TUKIO KATIKA PICHA : CLUB OLYMPIA YA SINZA MORI YATEKETEA KWA MOTO

 jijini Dar es Salaam, Asubuhi hii maeneo ya Sinza Club mpya na ya kisasa imeweza kuteketea kwa moto, tukio ambalo limewashangaza wengi na baadhi ya wadau wanasema chanzo bado akijajulikana kuhusiana na moto huo uliopelekea hasara kubwa ya kuungua kwa vifaa vilivyokuwa ndani ya hii club.

UJUMBE KUTOKA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI (NDC) WATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA,

1
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali GS Milanzi(kushoto) akisalimiana na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza walipofanya ziara ya mafunzo Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo Januari 27, 2015(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
2
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali GS Milanzi (kushoto) akisaini katika kitabu cha wageni mapema leo alipowasili Makao Makuu ya Jeshi la Magereza kwenye ziara ya mafunzo kuhusu uendeshaji wa Jeshi la Magereza(kulia) ni Kamishna wa Magereza, Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile.

SHULE YA MSINGI KALOLENI YAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA UZIO WA UKUTA

SAM_0832
Wanafunzi wakiwa wanasukuma mashine kwaajili ya kutengeneza kisima cha maji
SAM_0834
Mwanafunzi mwenye tatizo la utindio wa ubongo akiwa anaosha vyombo shuleni hapo

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YAITAJI AFISA MUANDAMIZI WA CHEO CHA NAIBU KAMISHNA WA MAMLAKA WA MAPATO TANZANIA (TRA)

index
Na Maryam Kidiko/
Kijakazi Abdallah – 
 Maelezo Zanzibar .
    
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema Kuna umuhimu mkubwa Zanzibar kuwa na Afisa muandamizi wa cheo cha Naibu Kamishna wa Mamlaka wa Mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kusimamia ukusanyaji wa Mapato yatokanayo na  ushuru wa Fedha na ushuru wa bidhaa  katika juhudi za  kuimarisha shughuli  za uchumi wa Zanzibar.
Hayo yalisemwa na  Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee wakati akijibu suali la Mh, Jaku Hashim Ayoub Jimbo la Muyuni alietaka kujua kama kuna  ulazima wowote wa TRA kuwa na Afisa muandamizi wa cheo  hicho Zanzibar.
Amesema Mamlaka ya Mapato Tanzania  ni Taasisi ya Muungano iliyoundwa kwa mujibu wa sheria Na.11 ya mwaka 1985 ambapo inapaswa kuwa na  Ofisi yake Zanzibar.
Amesema kuwa kazi ya TRA Zanzibar nikukusanya Mapato ya Muungano yanayotokana na kodi ya Mapato,  Ushuru wa Fordha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini kama ilivyoainishwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

MATUKIO BUNGENI MJINI DODOMA -JANUARI 27, 2015

1
Spika wa Bunge, Anne Makinda akiongozwa na Mpambe kuingia kwenye ukumbi wa Bunge Januari 27, 2015.Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu
2
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama,Bungeni mjini Dodoma Januari 27, 2015.

UN Tanzania Waadhimisha Siku ya Kimataifa ya Maadhimisho ya Wahanga wa Maangamizi Makuu ya Moto dhidi ya Wayahudi

Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania Mh Egon Kochanke akitoa historia fupi ya wahanga wa maangamizi Makuu ya Moto Dhidi ya Wayahudi katika maadhimisho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Utamaduni wa Russia na kuandaliwa na Umoja wa Mataifa Tanzania.
 Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Bi Usia Nkhoma akiwakaribisha wanafunzi wa shule za sekondari za jijini Dar pamoja na wanafunzi wa Vyuo Vikuu vilivyopo Jijini Dar ambavyo Kuna Klabu za Umoja wa Mataifa katika ukumbi wa utamaduni wa Russia wakati wa Siku ya Kimataifa ya Kuadhimisha na kuwakumbuka wahanga wa Maangamizi Makuu ya Moto Dhidi ya Wayahudi.

KAMATI YA TUPA RUFANI YA MWANZA KOMBE LA TAIFA WANAWAKE

mmmmmmmmm   Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetupa rufani ya timu ya Mwanza kupinga uhalali wa wachezaji wawili wa Kigoma kwenye mechi yao ya robo fainali iliyochezwa jana (Januari 26 mwaka huu) Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.Mwanza iliyopoteza mechi hiyo kwa mabao 2-1 iliwalalamikia wachezaji Neema Sanga na Vene Dickson wa Kigoma kuwa waliwahi kuchezea timu ya Taifa (Twiga Stars), hivyo kucheza mashindano ya Kombe la Taifa la Wanawake ni kinyume cha kanuni. Kamati baada ya kupitia rufani hiyo, imeitupa kwa vile timu ya Mwanza haikuwasilisha vielelezo vyovyote kuthibitisha madai hayo dhidi ya wachezaji hao. Pia Kamati yenyewe ilipitia taarifa za Twiga Stars ambapo haikupata kumbukumbu za wachezaji hao katika timu hiyo. Pia Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya TFF imesikitishwa na kitendo cha viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) Mkoa wa Mwanza kugomea uamuzi dhidi ya rufani yao, hivyo imependekeza Mwenyekiti wa TWFA Mwanza, Sophia Tigalyoma na Katibu wake Hawa Bajanguo wapelekwe Kamati ya Nidhamu kwa hatua za kinidhamu.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MHE. GEORGE SIMBACHAWENE NA NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI CHARLES MWIJAGE WAANZA KAZI RASMI KWA KUTEMBELEA MRADI WA UMEME WA KINYEREZI

1
Mtaalamu kutoka kampuni ya Jacobsen Elektro iliyopewa kazi ya kujenga kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi I Clas-Eirik Strand (kushoto) akibadilishana mawazo na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava (kulia) Katikati ni Meneja Mradi wa Kinyerezi kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima.
18
Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene (kulia) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa ziara. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Dk. James Mataragio na Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati) Mhe. Charles Mwijage.

WAIMBAJI WATAKA NAFASI ZAIDI TAMASHA LA PASAKA

images
Na Samia Mussa
 
WAKATI wakazi wa mikoa kadhaa hapa nchini wakiomba Tamasha la Pasaka lipite kwenye mikoa yao, baadhi ya waimbaji wakongwe wa tamasha hilo linalotimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake,  wametoa mapendekezo yao kwa wandaaji Kampuni ya Msama Promotions.
Wakizungumza hivi karibuni wimbaji hao, walianza kwa kuipongeza Kampuni hiyo kufikisha miaka hiyo bila kutetereka huku wakitoa mapendekezo mbalimbali yatakayoboresha zaidi matamasha yajayo.
Moja ya mapendekezo hayo ni pamoja na kutaka kila mwimbaji apate nafasi  angalau ya kuimba nyimbo mbili ukizingatia waimbaji hao wana albamu zaidi ya tatu jambo ambalo kwao linawapa ugumu kwao pamoja na mashabiki.

WIZARA INAYOSIMAMIA VIJANA NA HARAKATI KUWAKOMBOA VIJANA WA RUNGWE.

1
Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa wa pili kushoto akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Eng. Harold D. Sawaki katikati walipofika Wilaya ya Rungwe jana kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana wa Wilaya hiyo. Kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Bw. Ason Nzowa, wa pili kulia ni Afisa Michezo na Vijana Mkoa wa Mbeya Bw. George Mbijima na wa kwanza kushoto ni Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga.
2
Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga kulia akizungumza na vijana wa Wilaya ya Rungwe wakati wa semina ya Ujasiriamali, Stadi za Maisha, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana karika Wilaya ya Rungwe. Katikati ni Mwezeshaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Ester Riwa na kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele.

NSSF, REAL MADRID KUZALISHA VIPAJI VYA SOKA TANZANIA

3
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhani Dau  akifafanua jambo kwa wageni waliohudhuria hafla fupi ya kusaini mkataba  kati ya shirika hilo na timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid wa kuanzishwa kwa kituo cha michezo (sports academy) katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Dk. Dau alisema katika uendeshaji wa kituo hicho, Real Madrid itakua na dhamana ya kushughulikia masuala yote ya ufundi, kuwatambua wachezaji, chakula, wataalamu wa saikolojia na wataalamu wa viungo na kwamba wajibu wa shirika lake utakuwa kwenye kujenga tu.
2 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dkt. Ramadhani Dau (aliyekaa kushoto) na Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya mpira wa miguu ya Real Madrid, Bw. Ruben De la Red Gutierrez (aliyekaa kulia) kwa pamoja wakisaini mkataba wa kuanzishwa kwa kituo cha michezo (sports academy) katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia ni wawakilishi kutoka pande hizo mbili. Kituo hicho kitakua na uwezo wa kupokea wanafunzi 108 kwa wakati mmoja.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

index16
Mtu mmoja mkazi wa kitongoji cha chang’ombe auawa kwa kupigwa na wananchi.
Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha mkutano wilayani momba auawa na kisha mwili wake kutupwa shambani.mtu mmoja mkazi wa ilomba jijini mbeya afariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na semi traller.
KATIKA TUKIO LA KWANZA
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la mwinzala sekele mwenye umri kati ya miaka 40 – 45 Mkazi wa kitongoji cha chang’ombe – mshewe aliuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi.
mwili wa marehemu ulikutwa umetelekezwa mnamo tarehe 26.01.2015 majira ya saa 11:00 Asubuhi huko katika kijiji na kata ya mshewe, tarafa ya bonde la usongwe, wilaya ya kipolisi mbalizi,
                Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni kulipiza kisasi kufuatia marehemu kutuhumiwa Kuhusika katika tukio la mauaji ya sekela kaini mkazi wa kijiji cha mshewe ambaye alikutwa ameuawa na kutupwa katika shamba la mahindi kijijini hapo tarehe 24.01.2015 majira ya saa 15:45 alasiri.

WANACHI WALALAMIKIA UGUMU WA MAISHA LICHA YA KUWA NA RASILIMALI ZA KUTOSHA

WILLIAM MUNGAI ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini akiwa ametoka kumpokea makamu mwenyekiti wa BAVICHA taifa Hon.Ole SOSOPI
 Makamu mwenyekiti wa BAVICHA taifa Hon.Ole SOSOPI akiwahutubia wananchi katika jimbo la mufindi kasikazini