TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, December 14, 2013

Mpango wa Fedha kutoka TASAF wawanufaisha wakazi wa Kongwe Kiona

Diwani wa kata ya kamange, Husein Juma Hading’oka akielezea jambo kwa wanakijiji wa Kongwe Kiona pamoja na Wanahabari , tarehe 13 Decemba, 2013, wakati walipotembelea kijiji cha Kongwe Kiona, ambapo baadhi ya Kaya zimenufaika na Mpango  wa Uhawilishaji Fedha kwa Maendeleo Endelevu ya Kaya, Mpango huu unalenga kunusuru kaya maskini, kwa kutoa ruzuku kwa kaya maskini sana ili ziweze kupata huduma za elimu na afya.

Baadhi ya  waandishi wa habari na wahariri wakiwa pamoja na wanakijiji wa Kongwe Kiona wakimsikiliza Afisa Mtendaji wa kata ya Kamange, Suleiman Jumanne(hayupo pichani) akisoma taarifa fupi, kuhusu manufaa ya mpango wa Uhawilishaji Fedha kwa wakazi wa kijiji cha Kongwe Kiona.


Wanakijiji wa Kongwe Kiona wakimsikiliza Diwani wa kata ya kamange, Husein Juma Hading’oka (hayupo pichani).

Mkazi wa Kijiji cha Kongwe Kiona, Sufiani Juma Sungura akitoa ushuhuda wa jinsi alivyo nufaika na Mpango wa Uhawilishaji Fedha, kutoka  Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Kupitia Mpango huu Ndugu Sungura ameweza kuezeka nyumba yake kwa bati pamoja na kuweza kujikimu dhidi ya njaa kwa kuhifadhi mazao ya chakula.

Mkazi wa Kijiji cha Kongwe Kiona, Bi. Khadija Said Sengwira, akieleza ni kwa kiasi gani mpango wa Uhawilishaji Fedha kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF),umebadili maisha yake, nasasa ni mfugaji wa bata wa biashara.

Mkazi wa Kijiji cha Kongwe Kiona, Said Juma Kwavi akionesha Magunia ya Mahindi aliyoweza kuzalisha na kuhifadhi baada ya kunufaika na Mpango wa Uhawilishaji Fedha, kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)

Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano kutoka  Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Zuhura Mdungi  akifafanua jambo kwa Wanahabari, tarehe 13 Decemba, 2013, wakati walipotembelea kijiji cha Kongwe Kiona, ambapo baadhi ya Kaya zimenufaika na Mpango  wa Uhawilishaji Fedha kwa Maendeleo Endelevu ya Kaya, Mpango huu unalenga kunusuru kaya maskini, kwa kutoa ruzuku kwa kaya maskini sana ili ziweze kupata huduma za elimu na afya. Kwasasa Mpango huu unatekelezwa katika Kaya za wilaya tatu za Mkoa wa Pwani ikiwemo Bagamoyo.

No comments:

Post a Comment