
WILAYA YA MBARALI – MAUAJI.
MNAMO TAREHE 1.12.2013
 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MPAKANI BARABARA KUU YA 
MBEYA/NJOMBE KATA YA IGAWA TARAFA YA   RUJEWA WILAYA YA MBARALI MKOA WA 
MBEYA.  MTU MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA  KIUME 
MWENYE UMRI KATI YA  MIAKA 37-40 ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUCHOMWA KISU 
KICHWANI NA SHINGONI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA 
KANDO YA  BARABARA HIYO. CHANZO CHA MAUAJI KINACHUNGUZWA. MWILI WA 
MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA MBARALI KWA UCHUNGUZI. 
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA NAIBU KAMISHNA WA POLISI DIWANI ATHUMANI
 ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA YA MAHALI ALIPO MTU/WATU 
WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA 
SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA MOMBA – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA 
                                        KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
 TAREHE 13.12.2013 MAJIRA YA SAA 14:30HRS HUKO MAENEO YA MTAA WA MWAKA  
 BARABARA YA TUNDUMA/SUMBAWANGA KATA YA TUNDUMA, TARAFA YA TUNDUMA, 
WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. GARI T. 904 BXV AINA YA M/CANTER 
LIKIENDESHWA NA DEREVA MAAMZEE S/O MOHAMED, MIAKA 21, MNYIHA, MKAZI WA 
MTAA WA MWAKA – TUNDUMA  LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ASIYEFAHAMIKA JINA
 WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA  KIKE, UMRI KATI YA  MIAKA 25-30 NA 
KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MWILI
 WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA KWA AJILI YA UCHUNGUZI.
 MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA. 
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA NAIBU KAMISHNA WA POLISI DIWANI 
ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA 
MOTO KWA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
 ZINAZOWEZA KUEPUKIKA HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA MWISHO WA 
MWAKA.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI – DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment