TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Thursday, December 12, 2013

Solly Mahlangu ‘Obrigado’ Kuombeleza kifo cha Mandela uwanja wa Taifa


solly2 
Na Makuburi Ally
WAKATI siku za Tamasha la Krismasi zikikaribia, Muimbaji mahiri  anayeshika kasi katika anga la muziki wa Injili barani Afrika, Solly Mahlangu anatarajia kuombeleza   kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo Nelson Mandela  anayetarajia kuzikwa keshokutwa kijijini Qunu nchini humo.
Baadhi ya waumini watajiuliza maswali mengi kwamba baada ya kifo cha Mandela labda muimbaji huyo hatoweza kushiriki katika Tamasha hilo la kumtukuza na kumuimbia Mungu, lakini ukweli ni kwamba wamtarajie muimbaji huyo ambaye ataimba baadhi ya nyimbo zake kwa lugha ya Kiswahili. 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi  wa Kampuni ya Msama Promotions ambao ni waandaaji wa Tamasha hilo, Alex Msama, muimbaji huyo  ni mmoja wa waimbaji kutoka nje ya Tanzania ambao watashiriki, hivyo waumini watarajie kumuona jukwaani akifikisha neno la Mungu kwa njia ya nyimbo.  
“Ni muimbaji ambaye anashika kasi katika anga ya muziki wa injili barani Afrika ambaye pia anamudu kuimba Kiswahili kizuri kwa  baadhi ya nyimbo zake, hivyo  anafaa zaidi kwenye tamasha la kumtukuza Mungu,” alisema Msama.
Msama anatoa wito kwa waumini kujiandaa na Tamasha hilo ambalo litakuwa na viingilio vya shilingi 2000 kwa watoto, 5000 kwa viti vya kawaida, VIP B shilingi 10,000 na VIP A shilingi 20,000.
Msama anasema kwa mikoani viingilio vitakuwa ni shilingi  5000  kwa  wakubwa  na watoto shilingi 2000.
Alizaliwa miaka 40 iliyopita na aliingia kwenye muziki wa kulipwa miaka minne iliyopita ambaye ameutangaza vilivyo muziki wa injili na kuuweka katika ramani ya muziki wa kumtukuza Mungu nchini Afrika Kusini.
Mbali ya kuwa maarufu katika nyimbo za injili nchini humo ni Mchungaji  ambaye ana uwezo wa kufanikisha muziki wa injili na kanisa lake ambalo ni Word Praise Christian Centre Intenational lililoko Tembisa.
Muimbaji huyo mwenye utajiri wa tuzo mwaka  2009 alipata tuzo ya albam bora ya SABC Gospel Crown, albamu hiyo iliyokuwa kwenye mfumo wa DVD  aliuza kopi 15,000 na CD zaidi ya 20,0000.
Mahlangu kabla ya kuja Tanzania kwenye Tamasha la Krismas hivi karibuni ametokea Harare Zimbabwe ambako alipeleka wimbo wake wa Kiswahili wa ‘Mwamba Mwamba’  ambapo kwenye tamasha hilo aliimba na muimbaji nguli Afrika Oliver Mutukudzi.
Mahlangu  alikuwa  na waimbaji wake wanne ambao wanalitawala vilivyo jukwaa ambao ni Sebastian Magacha, Mathias Mhere, the Charambas na Shiloh.
Mahlangu  amefanikiwa kupata tuzo  nne Afrika Kusini  na moja  Uingereza ambapo tuzo hizo alizipata mwaka 2012.
Mahlangu Obrigado anakuja Tanzania na msafara wa watu 14 ambaye atatoa zawadi ya Krismas kwa watanzania kwa kuimbva nyimbo 14 mfululizo, zikiwemo nyimbo za Kiswahili kama Mwamba mwamba na Eee Baba  ambazo zitafikisha ujumbe wa neno la Mungu kupitia uimbaji katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Krismas litakalofanyika hapa nchini katika mikoa mitano, litawakutanisha waimbaji kutoka nje ya Tanzania ambao ni pamoja na Liliane Kabaganza (Rwanda), Solomon Mukubwa (Kenya), Ephraim Sekeleti (Zambia) na Solly Mahlangu (Afrika Kusini).
Tamasha hilo ambalo litaanzia uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam (Desemba 25), Morogoro ( Desemba 26), Tanga ( Desemba 28), Arusha (Desemba 29) na Dodoma ( Januari 1 mwaka 2014).
 Waimbaji waliothibitisha kushiriki katika tamasha hilo ni pamoja na Obrogado, Liliane Kabaganza (Rwanda), Solomon Mukubwa (Kenya) na Eiphraim Sekeleti (Zambia) huku kwa waimbaji wa Tanzania ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Edson Mwasabwite, John Lissu na New Life Band.

No comments:

Post a Comment