Mratibu
 wa Tamasha la Ujasiriamali, Abdallah Mrisho (wa pili kulia) akiongea 
jambo na waandishi wa habari leo ndani ya ukumbi wa The Atriums Hotel 
iliyoko Sinza, Afrika Sana jijini Dar es Salaam.
Meneja
 Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha (wa pili kushoto) akiongea na 
wanahabari (hawapo pichani). Kulia ni mratibu wa tamasha hilo, Abdallah 
Mrisho na kushoto ni H. Baba.
Abdallah Mrisho akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
Msanii
 wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Fid Q naye akielezea namna 
atakavyolitumia tamasha hilo kuwajenga vijana wa Mwanza katika maisha 
yao kupitia fani yake ya muziki.
Msanii kutoka jijini Mwanza, H. Baba, akielezea namna alivyojipanga kuwafikishia somo la ujasiriamali wakazi wa Mwanza.
Baadhi ya waandishi na wapiga picha (kulia) wakichukua matukio ya habari kuhusu tamasha hilo.
MENEJA
 Mkuu wa kampuni ya Global Publishers Ltd, ambaye pia ni mratibu mkuu wa
 Tamasha la Ujasiriamali linalotarajiwa kufanyika Ijumaa hii hadi 
Jumapili jijini Mwanza, Abdallah Mrisho, leo ameongea na baadhi ya 
waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini na kuwaleleza kuhusu
 tamasha litakalofanyika siku ya Ijumaa katika Viwanja vya CCM Kirumba 
jijini Mwanza ambapo mikakati yote imekamilika.
Mrisho
 alisema tamasha hilo lililodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya 
Tigo, Benki ya NMB na Street University, limeandaliwa kuwawezesha vijana
 na wakazi wa Jiji la Mwanza kutambua mbinu mbalimbali za kujikwamua 
kimaisha. Watoa mada watakuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Global 
Publishers Ltd, Eric James Shigongo, James Mwang’amba, Emmanuel Mgaya 
(Masanja Mkandamizaji) na Mbunge wa Mbeya mjini Mh. Joseph Mbilinyi 
‘Sugu’.
Kwa 
upande wa burudani kutakuwa na wasanii Fid Q, H. Baba, Young Killer, 
Jitta Man na Sugu. Pia kutakuwa na wasanii wa muziki wa Injili ambao ni 
Martha Mwaipaja atakayeimba sambamba na Masanja Makandamizaji na Edson 
Mwasabwite.

No comments:
Post a Comment