TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, December 14, 2013

WAUMINI WAMFUNGUA LOWASSA

Posted: 02 Dec 2013 10:33 PM PST

Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Bw. Edward Lowassa (mwenye suti),akiwaaga waumini wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Mtandi,Wilaya ya Masasi,mkoani Mtwara,baada ya kuendesha harambee ya kuchangia shughuli za maendeleo ya Ushirika wa Mama wa Kikristo (UMAKU),mwishoni mwa wiki ambapo sh.milioni 103 zilichangwa katika harambee hiyo. Kulia kwake ni Askofu wa Kanisa hilo,Dayosisi ya Newala,Oscar Mnung'a.

  •   ACHANGISHA MILIONI 103/-,AMMWAGIA  SIFA MKAPA

Na Mwandishi Wetu, Masasi

  Waziri Mkuu aliyejiuzulu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Bw. Edward Lowassa, amesema yuko tayari kushirikiana na mtu yeyote katika mapambano ya kuondoa umaskini kwenye jamii.

Bw. Lowassa aliyasema hayo mwishoni mwa wiki Mjini Masasi mkoani Mtwara, katika harambee iliyofanyika kwenye Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Masasi, mkoani humo.

Harambee hiyo ilikuwa na lengo la kuchangia shughuli za maendeleo za Ushirika wa Mama wa Kikristo (UMAKI) na kusisitiza kuwa, yeye ni mdau wa mapambano hayo.

“Mtu yeyote anayepambana kuondoa umaskini katika jamii, niko tayari kushirikiana naye katika harambee za harakati hizi,” alisema Bw. Lowassa na kuongeza kuwa, wanawake ni jamii inayochukia sana suala zima la umaskini.

“Wanawake ni wadau wakubwa wa kupambana na umaskini ndiyo maana chama changu CCM, katika rasimu ya Katiba Mpya inataka kuwe na asilimia 50 kwa 50 ya uwakilishi bungeni kati ya wanawake na wanaume kwa sababu kinawapenda,” alisema.

Alisema kwa sababu hiyo, ndiyo maana ameridhia kushiriki harambee hiyo ambapo kufika kwake kanisani hapo kumetokana na Wilaya hiyo kutoa kiongozi makini, mwadilifu na shupavu mkubwa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Bw. Benjamin Mkapa.

“Hapa pana historia ya kutoa kiongozi aliyeiongoza nchi yetu kwa uadilifu na umakini mkubwa, walikuwepo watu waliyojaribu kumsema sema katika vyombo vya habari.

“Mwisho wa siku watu hao wamekiri kuwa Bw. Mkapa alikuwa kiongozio makini,” alisema Bw. Lowassa ambaye wakati kiongozi huyo akiwa madarakani, alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano kabla ya kupelekwa Wizara ya Maji na Mifugo.

Katika harambee hiyo, zaidi ya sh. milioni 103 zilipatikana ambapo Bw. Lowassa na marafiki zake alichangia sh. milioni 10 na kuvuka lengo ambalo lilikuwa sh. milioni 100.

No comments:

Post a Comment